Swali chokonozi: Mbona miili ya majambazi 4 waliouawa hatukuiona?

Azim Sokoine

JF-Expert Member
Aug 20, 2014
1,443
2,643
habar wakuu,

Ni masaa kadhaa yaliyopita Jeshi la Polisi limetupatia taarifa kuwa wale majambazi waliowaua polisi 8,jeshi hilo limefanikiwa kuua majambaz 4. Lakini cha ajabu miili hiyo ya hao majambazi hakuna aliyefanikiwa kuiona.

Nini kimejificha nyuma ya pazia juu ya hili! sio kwamba jeshi la polisi wanataka kuecolize kwa kuwahadaa watanzania?
 
Mkuu acha hizo basi,! Wataondoka sasa hivi wakawinde watu wengine wasio na hatia waje waoneshe hiyo miili ohooooooo si unawajua bongopolisi lakini??
Hiyo ni sinema kama sinema zingine tu mjomba!
 
Mkuu, hoja yako ipo wapi sasa? Kwani ni mara ngapi Polisi wanatangaza wameua majambazi na picha zao hazisambai? Kwanza si ubinadamu kusambaza mitandaoni picha za marehemu
Anayo hoja hujaiona hapo hoja?Ebu watanzania muwe mnatafakari mambo kwa kina.Kuna propaganda huwa zinaudwa kuweka mambo sawa huenda jeshi la polisi limeunda propaganda ili kuweka usawa fikilieni mara mbili sio kila siku mnawaza kuitetea ccm tu.
 
Wewe ni mgeni na taarifa za geshi letu hapa bongo?
 
uzalendo ni tatizo sugu vichwani mwa vijana..kila kitu siasa.
Uzalendo upi unaouzungumzia??? Isijekua ule wa kuparalyse reasoning centre??? Huo uzalendo unaouzungumzia ww hauji hv hv labda mpka upewe limbwata na watawala mpka ushndwe kabisa kufkiria kingne beyond ya kile unacholishwa kutoka kwao
 
Mkuu, hoja yako ipo wapi sasa? Kwani ni mara ngapi Polisi wanatangaza wameua majambazi na picha zao hazisambai? Kwanza si ubinadamu kusambaza mitandaoni picha za marehemu
Mkuu hivi aliyeua ni yule master wa kupiga kichwani tu?.yule jamaa ni mbaya ni bora Bashite akamteke yule kuliko kuvamia studio
 

Acha waendelee ' kutudanganya ' na kumdanganya Commander in Chief ili tu ' asiwatumbue ' na waonekane kuwa wapo vizuri na wamefanya bidii ILA wenye AKILI tena zilizotukuka vizuri mno tunajua kuwa kwa aina ya ' training ' kali ya ' Snipers ' wote duniani huwa ni ' vigumu ' sana kushindwa ' mission ' yoyote ile pale wakiamua na ya mfano halisi ni hiyo ya juzi.

Ili kujua kuwa huyo ' Sniper ' ni highly trained halafu yeye kama yeye pia ana akili nyingi za ' kuzaliwa ' angalia tu hata alivyoweza kupanga vizuri ' mashambulizi ' yake na ' yakapangika ' kama alivyotaka. Kwanza alianza na Dereva akiamini kabisa kuwa ' akimtungua ' yeye ataweza kuliangusha lile ' Gari ' kisha wale wenzake mule ndani ' watahamaki ' hivyo kutokana na hiyo ' ambush ' na wataanza kupiga hovyo hovyo bila kujua ' ramani ' ya pale kisha yeye kazi yake ya ' kuwadungua ' inakuwa rahisi sana kama ambavyo ilitokea na aliweza kufanya ile majuzi.

Personally siwezi kuamini na nakataa ' kata kata ' kuwa Police wameua hao ' Majambazi ' na pia wameweza kupata sehemu ya zile Silaha ambazo zilichukuliwa na ' Mdunguaji ' au ' Sniper ' ILA nikiambiwa kuwa Police wameuwa tu Wavuta Bangi wa huko Mkuranga na pengine hata kuchukua tu Silaha zao kutoka ' ghalani ' kwao na kusema kuwa wamezipata kutoka kwa hayo ' Majambazi ' uwongo huu naweza kuuamini bila shaka yoyote.

Nimalizie tu kwa kusema kwa aina ya ' Training ' ya Jeshi letu la Police la Tanzania na jinsi hata tunavyowaona na kukaa nao huku ' Kitaani ' hakuna Police yoyote mwenye ' ubavu ' wa kupambana ama na ' Gaidi ' au ' Sniper ' na katika hili tusitake ' kudanganyana ' hapa tafadhali.

Nadhani sasa ni wakati muafaka kabisa kwa Jeshi letu la Police ama kuanza kupewa ' Mafunzo ' makali na ya uhakika kama ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ ) au kile Chuo cha Police Mkoani Kilimanjaro kivunjwe na sasa Askari Police wote wawe wanatokea katika Jeshi la Kujenga Taifa ( JKT ) ambako naamini huko ' hupikwa ' kisawasawa na ' kuiva ' kuja kuitetea nchi.

Pasaka njema nyote na niseme tena R.I.P kwa Askari Police wote nane ( 8 ) waliopoteza maisha yao juzi usiku huko Mkuranga.
 
Mr nice point leo umechokonoa adi nimekuelewa haiwezekani masaa machache eti mpata majamba wanne na kuwaua wakati walisema jambazi alikuwa mmoja
Sasa hao wanne waliowaua mbona kama kuna changa la macho asee au ndo kufuta aibu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…