Swali ambalo wanaotetea kikokotoo kipya Huwa hawataki kujibu

Mlalamikaji daily

JF-Expert Member
May 19, 2014
694
1,489
Najua Kuna nyuzi nyingi kuhusu kikokotoo kipya vs kile Cha zamani,

Lakini ili kuondoa utata naomba mods waache huu uzi,
Kwani hili swali likijibiwa utata wote utaisha..

Hili ni maalum kwa WALE WANAODHANI KIKOKOTOO KIPYA NI KIZURI,


SWALI:
mwalimu YASINI amestaafu akiwa na mshahara basic tsh 1,500,000 (milioni Moja na nusu) amefanya kazi miaka 25
Je atapata kiasi gani (kiinua mgongo) na atapata kiasi gani Kila mwezi kwa..

1. Kikokotoo Cha zamani
2. Kikokotoo kipya

Tafadhali mods naomba swali langu lijibiwe
N.b hesabu ziwekwe wazi hapa na formula iliyotumika
 
Mimi sijui jibu,
Lakini nipo kwenye WANAODHANI Bora kurudia kikokotoo Cha zamani ,
Kuliko hiki kipya
Nikwambie kitu Hofu-less hakuna binadamu asiyejua kuwa kikokotoo cha zamani ni bora. Kwa taarifa yako tu hata Jenista Muhagama anajua fika kuwa kikokotoo kipya ni uhuni tu.

Ni vile serekali ime imechukuwa hela kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii na mifuko haina tena uwezo kuwalipa wastaafu hela zao kwa jumla sababu hela zilishatoka zikaenda kugharamia kampeni za ccm.

Hakuna hata punguani mmoja anaeamini kwenye kikokotoo kipya. Ni lugha za kisiasa tu
 
Hiki kikokotoo kipya kiwaguse na wabunge. Yaani wenyewe walipwe mafao yao baada ya kufikisha miaka 60! Na siyo kila baada ya miaka 5 wanalamba kirahisi tu milioni 250+.

Na wakifikisha hiyo miaka 60, wapewe mafao yao kwa mfumo wa hiki kikokotoo cha 33% kama wanavyofanyiwa watumishi wengine.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™Œ

Kwamba kikokotoo kipya mfanyakazi anapata pesa ndefu zaidi??
1. Kipya kwa walio kuwa PSPF na LAPF Kiinua Mgongo ni kidogo kuliko cha zamani.

2. Kipya kwa walio kuwa PSPF na LAPF pensheni ya kila mwezi ni kubwa kuliko cha zamani.

3. Kipya mstaafu akifariki tegemezi wake watalipwa Γ—36 yakile alicho kuwa anakipata kwa mwezi.

4. Kipya hakitumii Last Salary, kinatumia Wastani wa mishaara bora ya miaka mitatu ndani ya miaka 10 kabla ya kustaafu.. Amboyo ni faida kubwa kwa mtu ambaye alikuwa na kitengo alafu kabla ya kufikia kustaafu akapunguzwa mshaara.

5. Kipya kwa wanachama walio kuwepo LAPF na PSSSF kimepunguza Umri wa kuishi baada kustaafu hii ni kutokana na living standard ya nchi yetu, kwa Wanachama wa NSSF, GEPF na PPF umri wa kuisho baada ya kustaafu ni ule ule.

6. Kipya kimepungaza kikokotoo limbikizi kwa wanachama wa LAPF na PSPF kwa NSSF, GEPF na PPF kimebakia vilevile

7. Kipya kinafanya mfuko uendelee kujiendesha kikamirifu, na kuendelea kuwepo vizazi na vizazi

Haya yote inatakiwa uelewe zana ya Hifadhi ya jamii ni nini...!? Hifadhi ya jamii Haipo kwaajili ya kukupa utajiri, pesa ya kujengea nyumba kununua gari n.k hifadhi ya jamii ipo kwaajiri ya kukupa income security pale unapo poteza kazi/kipato iwe kustaafu, kuondolewa kazini, kuugua nk
 
Walau kidogo umejibu.
Na kwa majibu haya advantages nyingi zipo kikokotoo Cha zamani
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…