ukwaju_wa_ kitambo
Senior Member
- Sep 15, 2024
- 141
- 147
MOVEMENT YA HIP HOP KUPITIA MEDIA ZA MWANZA.
Mwanza kupitia Radio Free Africa na Kiss FM walifanya mapinduzi makubwa sana kwenye kuiendeleza Hip hop na hii waliifanya makusudi ili kutoa ile dhana kwamba ukiwa Dar ndio utatoka kimuziki.
Kwenye harakati hizi za kuhakikisha Hip hop inafika mbali Radio Free Africa na Kiss FM kwenye vipindi vyao walikuwa na "segment" mahsusi kwa wasanii wa hip hop.
Mfano kwenye kipindi cha RFA kulikuwa na kipindi ambacho kilikuwa kina rushwa weekend kilikuwa kinaitwa "Weekend Freever" kikiwa hosted na Sandu G au Kid Bway humu kulikuwa na Interviews za wasanii wapya na malengo yao ya kukuza game hii ya hip hop.
Kwenye Kiss FM kulikuwa na kipindi kilikuwa kinaitwa "Top Ujazo" kipindi kilikuwa hosted na Dee 7 au Hasan Wibonela kwasasa ni marehemu kilikuwa kinaanza saa 12 jioni huku nako kulikuwa ni moto ngoma mpya za watu wa hip hop na Interviews kibao.
Kwa hiyo game ilikuwa imechangamka sana kwa hiyo Kiss FM,RFA kulikuwa na ushindani wa kupiga ngoma mpya kati ya radio za Mwanza na Dar halafu kukawa na ushindani wa kutoa wasanii kutokea ukanda wa Mwanza.
Kid Bway alienda mbali zaidi alivyokuja na studio yake TETEMESHA RECORDS (kuna story yake) ambapo hii record label ilikuwa imebeba asilimia kubwa up coming artist.
Hawa wakina Joh Makini,Bonta Maarifa,Q the Don,Nako 2 Nako,Rama D,Fid Q,Rado Kiraka K na D Wa MaujanjaSaplayaz Roho 7,Geez Mabovu, Teddo TZ, Yaki, Mad P na wengine kutoka mikoa mbali mbali kimbilio lao ilikuwa ni Radio Free Africa na Kiss FM huku ngoma zilikuwa zinagongwa sana kwenye hizi radio.
Na kwa kipindi hicho kuliwa na ushirikiano mzuri sana baina ya wazalishaji wa music mfano Amba,Roy,Q The Don na Kid bway walikuwa na lengo la kuhakikisha Hip hop inafika mbali.
Wasanii wengi wa Dar walivutiwa sana na movement zilizokuwa zikifanyika na RFA na Kiss FM kwani zilikuwa na lengo la kuufikisha mbali mziki wa hip hop.
#funguka
Ukwaju wa kitambo
0767 542 202