Sumu ya sera ya majimbo ya Dr. Slaa na Mbowe kuwaua wabunge wa CHADEMA

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,569
Wadau, hivi karibuni, viongozi wa CHADEMA chini ya Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dr. Wilbroad Slaa walitangaza mpango wa Tanzania kuongozwa katika Mfumo wa Majimbo. Katika nadharia yao hiyo, ni kwamba nchi ya Tanzania itagawanywa katika Majimbo ili kuharakisha shughuli za maendeleo.

Wametolea mfano kuwa mataifa mengi ikiwa ni pamoja na Marekani yameendelea kwa vile kuna majimbo ambayo yana mamlaka ya kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo katika majimbo yao. Kwa mujibu wa nadharia yao hiyo ni kuwa Tanzania itakuwa na mamlaka mbili za kiutawala.

Kutakuwa na serikali kuu ambayo itakuwa na wajibu wa kushughulikia masuala ya kitaifa ikiwa ni pamoja na ulinzi na usalama sambamba na ushirikiano wa kimataifa. Aidha, kutakuwa na serikali za majimbo ambazo zitakuwa na jukumu la kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo katika maeneo yao.

Katika kutekeleza hilo, CHADEMA wameanzisha kampeni za kueneza hoja yao hiyo kwa wananchi huku ikiwashawishi wakatae raslimali zao kutumika kwa manufaa ya Taifa. Mathalan, baada ya OPERESHENI OKOA KUSINI kutokuwa na mafanikio, viongozi wa CHADEMA waliwashawishi viongozi wa vyama vingine vya upinzani katika mikoa ya Lindi na Mtwara ili waanzishe kampeni ya kupinga mradi wa Taifa wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam chini ya kauli mbiu GESI KWANZA, VYAMA BAADAYE, HAPA HAKITOKI KITU. Kudhihirisha hilo, bendera ya CDM ilipeperushwa wakati wa maandamano yaliyofanyika Desemba 2012 na Januari 2013.


  • Inawezekana kabisa CDM hawana watu wa kutosha wenye sifa za kuunda serikali kwa maana ya Rais, Makamu wa Rais, waziri Mkuu, mawaziri, Makatibu wakuu, wakuu wa mikoa, wakuu wa Wilaya n.k na hivyo kuona kama sera hii ni mwarobaini wa kukidhi idadi ndogo kabisa ya watu wenye sifa hizo ukimwondoa Mwenyekiti wa chama ambaye hata elimu yake ya kidato cha nne haioneshi alisoma shule gani, huku uzoefu wake wa kazi ikiwa ni karani wa benki kuu wakati Baba mkwe wake akiwa Gavana
  • Kwa maoni yangu ni kuwa, kitendo cha viongozi wa CHADEMA cha kuigawa nchi ambayo hawana mamlaka nayo ni uvunjwaji wa katiba na sheria za nchi. Kwamba, nchi ya Tanzania kwa sasa inaongozwa kwa mujibu wa katiba ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake ambapo ndani ya katiba ya sasa hakuna kipengele kinachoelezea sera ya majimbo. Kwa kitendo cha viongozi wa CHADEMA kuigawa nchi wanastahili kuchukuliwa hatua za kisheria na kama ingekuwa Tanzania ni nchi inayoongozwa kimabavu, Dr Slaa na Mbowe hivi sasa wangekuwa wapo ndani ya magereza yetu wanasubiri hukumu ya kifo kwa makosa yao ya uhaini
  • Hapana ubishi kuwa mikoa kama Dar es salaam, Tanga, Pwani, Lindi na visiwa vya Zanzibar waumini wake wengi ni waislamu, huku mikoa kama Mbeya, Kilimanjaro, Arusha na Manyara waumini wake walio wengi ni wakristo. CDM wameamua kwa makusudi mazima kuwagawa watanzania kwa misingi ya udini, hoja ambayo wanajaribu kuwa-preempt CCM kuwa ndiyo wanaeneza udini. Hili linafanyika kwa makusudi hasa ukizingatia kuwa wote wanaopiga kelele za kuwa CCM ni wadini wote wamelelewa na kanisa (SLAA, MBOWE, LEMA, MNYIKA n.k), kwa ushahidi tazameni CV zao kwenye tovuti ya bunge mkajionee, hata machapisho yao ni vitabu vya dini.
  • Kuonesha kwa vitendo kuwa ni wadini kwa kuyaenzi maneno yalioko kwenye vitabu vitakatifu kuwa "KILA MTU ATAUBEBA MSALABA WAKE MWENYEWE" kwani sasa ile mikoa ambayo haina maliasili kama mito, maziwa, milima na madini na iko nyuma kimaendeleo iendelee kuwa maskini na ile yenye maliasili na iko mbele kimaendeleo na iendelee tajiri.

Sera ya Majimbo imeanzishwa kama sehemu ya kuingilia tu mwelekeo halisi ni kuigawa nchi kimkoa. Katika maandalizi ya hilo, CHADEMA wameanzisha Tovuti za kimkoa kama vile Mbeya Yetu, Katavi Yetu, Iringa Yetu, Lindi Yetu, Mtwara Yetu, Dar es Salaam Yetu, Arusha Yetu na Zanzibar Yetu. Mitandao hiyo imeratibiwa na kuendeshwa na CHADEMA kwa lengo la kuhamasisha vijana ambao ndio watumiaji wakubwa kuichukia serikali na kujitambua kimkoa chini ya dhana ya WAGAWE UWATAWALE.

  • Katika kuonyesha kuwa dhana yao hiyo haitekelezeki, viongozi wa CHADEMA na hasa FREEMAN MBOWE na dr WILBROAD SLAA wamekuwa wakitumia mapato ya kitaifa ya CHADEMA kuendeleza majimbo yao ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za kijamii kama vile maji na afya huku akina MNYIKA wakitegemea hoja binafsi bungeni na maandamano kuondoa matatizo yanayowakabili hususan tatizo la maji ubungo. Kutokana na hali hiyo, wabunge wengi wa CHADEMA watapoteza majimbo yao katika uchaguzi wa 2015 kwa vile wananchi wanatambua kuwa wabunge hao hawana uwezo wa kuwaletea maendeleo
  • DR SLAA na MBOWE wamekuwa wakihamasisha maandamano katika maeneo mbalimbali nchini kama mkakati mmojawapo wa kutekeleza sera hiyo ya majimbo. Kwa kutambua athari za maandamano, viongozi hao hawajawahi kuitisha maandamano hata siku moja katika majimbo yao. Mathalan, siku chache zijazo, MBOWE ataitisha maandamano mkoani Mbeya kushinikiza DR KAWAMBWA ajiuzuru. Maandamano pia yanafanyika kwenye wilaya moja ya kanda ya ziwa kupinga kitendo cha nguzo za umeme kuanguka wakati wa mvua nyingi.
 
Hawa ndiyo aina watu tunaowataka humu JF, wenye uwezo wa kupembua na kuchanganua mambo, kuna haja kubwa ya kutafakari kwa kina kuhusu hawa wanasiasa wanakotaka kuipeleka nchi.
 
Duh kweli MUNGU katuumba topfauti, hivi ingekuaje wote tungekuwa na uelewa mmoja? MANI
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: jyn
hahahaaaaa, kumekucha. kumbe ndiyo mwelekeo wao? hawa watu ni hatari sana.vyombo vya dola vichukue hatua dhidi yao. na hayo maandamano ya mbeya polisi chukueni hatua zinazofaa kuyadhibiti ikiwa ni pamoja na kumkamata mbowe na kumfikisha mahakamani kwa kuhamasisha vurugu. mbona yeye hakuandamana alipofeli mtihani wake wa form four
 
Sera ya Majimbo CHADEMA sasa yaanza kukikunja CCM kila kona ya nchi hii sawa yake na jinsi gani watu hukunja jamvi msibani mara baada ya maziko.

Naam, hongereni sana waheshimiwa hapo CDM makao makuu kwa ubunifu huo wenye viashiria vyote vya kuchangia kuharakishia wananchi maendeleo mashinani kwa kasi ajabu bila ya kulazimika kuwaachia MAFISADI hatima ya maisha yao na kubakia tu kuomba kuonewa huruma, kwa mtaji wa kodi zao wenyewe, toka jijini Dar es Salaam.
 
yaani mnatapatapa nyie mapovu yanawatoka leo hili kesho lile sisi tumebuni sera yetu ambayo tukiingia madarakani tutaitumia sasa tatizo liko wapi..tumejigawa chama kwa maana ya majimbo ili kurahisisha ilani yetu itekelezeke vizuri na tukiingia madarakani itatumika na wala hatujaigawa nchi kwani sisi ndo serikali mpaka tugawe nchi.......na kwa taarifa yako kazi ya mbunge ni kuisimamia serikali sio kujenga barabara wala mabomba ya maji ukitakata kufanya hivyo huo ni uwezo wako hukatazwi.....mnyika ndo mbunge anaengoza kwa kufatilia kero za jimbo lake na kuzipeleka sehemu husika hizo ndo kazi za mbunge na tunaziona mabomba kutoa maji na barabara ni kazi ya serikali
 
Mkuu, naona umejitahidi kuunga unga stori yako lakini mwisho wa yote, kichwa cha habari na habari yenyewe haviendani kwa kiasi kikubwa tu. Binafsi nimeshindwa kukupata kabisa labda kama lengo lako ni upotoshaji wa sera ya majimbo. Kwa nini useme chadema wameigawa nchi kinyume cha katiba na wanastahili kuwa jela kwa kosa la uhaini? Hebu nidadavulie hapo mkuu!
 
dah! kama ulivyosema ni maoni yako nadhani ni sawa ni maoni yako . Hapo umejitutumua ukaona umeandika kitu cha maana sana. Ngoja nikwambie maneno matatu tu. ambayo pia ndo yamesababisha uandike huu uharo wako hapa: CHADEMA FOR LIFE. Mtataga mwaka huu magamba
 
Mmejaribu kuwatebganisha Mbowe na Slaa kila mara mmegonga mwamba, ulichoandika ni mawazo yako juu ya hofu kubwa ya watz kutambua vizuri dhima ya ari mpya, kaz mpya na nguv mpya inavyowatafuna
~ Mazao juu
~Umeme hakuna
~ Barabara nzur zipo mjini tu
~ Rasilimali zinaibiwa kupitia dar bandarin na airport
~ Madiwan weng darasa la saba ambao hawajui kuhoji
~ Gap kubwa la mashiki na matajiri
~ Den la taifa kuwa juu
~ Makao makuu ya kila kitu dar

Alaf watu wanaweka utaratibu wakila jimbo linufaike na maliasili yake kwanza unaleta ushoga hapa.
 
Sera ya CHADEMA au ya Dr. Slaa na Mbowe?

attachment.php
 
Sera ya Majimbo CHADEMA sasa yaanza kukikunja CCM sawa yake na jamvi msibani mara baada ya maziko.

Hongereni sana CDM makao makuu kwa ubunifu huo wenye viashiri vyote vya kuharakishi wananchi maendeleo mashinani bila kuwaachia MAFISADI hatima ya maisha yao na kuomba kuonewa huruma toka jijini Dar es Salaam.

Watu wameshtukia sera hii chafu ya kuwagawa watanzania kwa misingi ya udini, ukabila, raslimali na maendeleo.

Wote kwa pamoja tuseeme Umajimbo sasa baaassz
 
Back
Top Bottom