Sumu ya panya inaweza kumuua kenge?

Mdumi ashery

New Member
Feb 24, 2017
3
2
Hivi sumu ya panya inaweza muua kenge, nimepaka sumu vipande vitatu vya nyama halafu ni kamuwekea pale anapo pitaga nje ya shimo lake na inavoonekana kala sasa sijui kama atakufa au la vipi sumu ya panya inaweza muua kenge kweli au nimefeli.
 
Hivi sumu ya panya inaweza muua kenge, nimepaka sumu vipande vitatu vya nyama halafu ni kamuwekea pale anapo pitaga nje ya shimo lake na inavoonekana kala ssa sjui kama atakufa au laa vipi sumu ya panya inaweza muua kenge kweli au nimefeli.
Biologically hawa ni mammals na reptiles, wako karibu on the evolutionary tree, most likely itamuua
 
Pengine anakula vifaranga vya kuku! Zamani kulikuwa na story kenge akikukuta nje umeme, anaingiza ulimi wake puani anavuta unakosa pumvi unakufa....
Mhh tumekaa nae Mwanza karibu na tulipokuwa tunaishi sijawahi kuona akiharibu kitu...
Kwanza kenge ni mwoga sana
 
Tengeneza samaki Sato mkaushe vizuri. Mjazie chumvi ya kutosha ,yaani weka chumvi nyingi halafu mtegee anapopita.

Akishamaliza kula koo litamuwasha atapata kiu kisichoisha ataenda kunywa maji hadi atakufa mwenyewe
Is this serious or just a joke? So samaki lazima awe sato tu?!😆😆
 
Tengeneza samaki Sato mkaushe vizuri. Mjazie chumvi ya kutosha ,yaani weka chumvi nyingi halafu mtegee anapopita.

Akishamaliza kula koo litamuwasha atapata kiu kisichoisha ataenda kunywa maji hadi atakufa mwenyewe
Duh!
 
Hivi sumu ya panya inaweza muua kenge, nimepaka sumu vipande vitatu vya nyama halafu ni kamuwekea pale anapo pitaga nje ya shimo lake na inavoonekana kala ssa sjui kama atakufa au laa vipi sumu ya panya inaweza muua kenge kweli au nimefeli.
Mwanangu nyama hiyo dah, ungeniita niweke mtego tumnase bila kumuuwa.
 
Niliwai ona kwa wafugaji magereza wakiwategea kenge mayai ya kuchemsha. Kwa maelezo yao kuwa kenge anapokula mayai hapasulii mdomoni, ulimeza na kulivunjia shingoni, sasa atapomeza yai lililochemshwa na kupoa atapojaribu kuvunja atashindwa. In short litamkaba had kufa.

😌😌 ila umenikumbusha mbali. Mzee wetu enzi zake alikuwa anapambana nao sana. Tulikuwa na mabwawa ya samaki na kuku, kenge na fisimaji walikuwa wasumbufu, basi anawategea usiku sana na mkuki, anawaua. Asubuhi anawatundika kwenye mti, basi watu wanajaa kushangaa yeye kichwa hichoooo 😌

Yani mtu saa 6 usiku katega mtoni kutegea kenge na mkuki na rungu. 🤓🤓 mabanda ya kuku yalizungukwa na kunguru aliowatundika baada ya kuwaua kwa manati.
 
Asante mkuu, huu ushauri wako niliufanyia kazi maana maeneo yangu wapo kenge wengi sana na wanakula sana vifaranga vyangu vya Bata,ninapo sema wengi ,ni wengi hasa .

Nilitega Kwa mayai ya kupika nilikuta wamekula na wameyatapika ,Sasa Mimi nikaamua kuboresha kidogo nikachukua yai bichi na kumimina kile kiini Kwa kutoboa na sindano ,baada ya hapo yai nalijaza sumu hizi za kimiminika za madukani baadaye naziba sehemu nilyoitoboa Kwa super glue,genge huja na kulifakamamia yai na kulitobolea tumboni .kifuatacho ni Mungu tu ndo anajua.

Kwa Sasa nimepumzika kabisa Bado wapo ila hawasumbui Bata wangu nimekusudia kuwamaliza kabisa. Nashukuru sana Kwa wazo hili.
 
Back
Top Bottom