Sumu mwilini na jinsi ya kuzitoa

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
740
485
Sumu mwilini na jinsi ya kuzitoa

Uondoaji wa sumu mwilini hutegemeana na aina ya sumu yenyewe.

1. Sumu kutoka nje ya mwili: Njia ya kwanza ni matumizi ya Dawa za kuivunja nguvu ile sumu husika ambapo kitaalamu hujulikana kwa jina la antidote, hapa ni baada ya uchunguzi kufanyika na kugundua aina ya sumu iliyokuathiri na kisha utapewa dawa kulingana na majibu ya uchunguzi wa kitaalamu.

2. Sumu zinazozalishwa na mwili: Njia ya pili inayoweza kutusaidia kuondoa sumu na hasa zile zinazozalishwa mwilini ni matumizi ya vyakula bora, hivi ni vyakula ambavyo kwa asili yake huwa na virutubisho ambavyo huvunja vunja na kuondoa sumu mwilini, vyakula hivi kitaalamu huwa na vitu vinavyoitwa antioxidants, ambavyo huulinda mwili dhidi ya kemikali hatarishi zinazozalishwa mwilini. Virutubisho hivi ni pamoja na
Vitamin A,
Vitamini C na
Vitamini E.

Vitamini hizi hupatikana katika mboga za majani na matunda, mfano mchicha, spinachi, karoti, matembele, machungwa, nanasi, maembe, machenza pamoja na mafuta ya mimea mfano alizeti.

Ili miili yetu iweze kufanya kazi vizuri na tuendelee kuwa na afya njema, inabidi tuepukane na sumu hizi, pale inapo tulazimu zitumike (mfano zebaki, migodini), basi tuzidishe umakini katika kujilinda afya zetu, na pia tubadilishe aina ya maisha au ulaji wa vyakula, matunda na mboga za majani ni walinzi wakubwa sana wa afya zetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…