Sumaye: Ningefuta sheria ya kubadili Katiba

mcubic

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
10,310
6,544
Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye ameishauri Serikali ya Awamu ya Tano kufuta Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na kutunga ambayo itaunda timu ndogo ya wataalamu badala ya Bunge la katiba lenye watu zaidi ya 600 ambao hawana ujuzi. Sumaye amesema Bunge la Katiba lenye watu 630 lisingeweza kuandika Katiba nzuri na hivyo akashauri kuundwa kwa timu ndogo ya wataalamu ambayo itachambua Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa chini ya Jaji Joseph Warioba kwa kulinganisha na Katiba ya mwaka 1977.

Akizungumza na gazeti hili kwenye mahojiano maalumu ofisini kwake, Sumaye alisema utaratibu mzima wa kuendesha mchakato ule ulikuwa mbovu na kamwe usingeweza kufanikisha malengo yaliyokusudiwa. Sumaye, ambaye mwaka jana alihamia kambi ya upinzani akitokea CCM, alisema kilichovuruga mchakato mzima ni kitendo cha kuwa na wajumbe wengi ambao wasingeweza kujadili vizuri na kutoka na Katiba bora, na kushauri kuundwa kwa timu ya wataalamu kati ya 20 na 30 kufanya kazi hiyo.

“Kwanza ni lazima Katiba ishughulikiwe. Hilo ni la msingi kabisa kwa sababu hatuwezi kuendelea na hii Katiba. Ukiendelea na hii Katiba, huwezi ukapata demokrasia ya kweli,” alisema alipoulizwa angemshauri nini Rais John Magufuli kuhusu kuendelea na mchakato wa Katiba. “Mimi nina tatizo na katiba zote; ile ya (Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph) Warioba, na ile nyingine (ya mwaka 1977).”

Mchakato wa kuandika Katiba mpya ulikwama kwenye hatua ya kupiga kura ya maoni kuridhia Katiba Inayopendekezwa baada ya Tume ya Uchaguzi (NEC) kushindwa kukamilisha utoaji vitambulisho kwa wapigakura.

Bunge hilo lililoundwa na wabunge wote wa Jamhuri ya Muungano pamoja na wawakilishi kutoka makundi mbalimbali, liliingia dosari baada ya vyama vinne na baadhi ya wajumbe kujitoa kwa maelezo kuwa liliacha hoja za wananchi zilizokuwa kwenye Rasimu ya Katiba iliyoandikwa na Tume ya Warioba.

Kuhusu kukwama kwa mchakato huo, Sumaye alisema kama Bunge lingekuwa halijatunga Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013, angetafuta kikundi cha watu wachache wataalamu ambao wangechambua Katiba ya zamani kwa kulinganisha na Rasimu ya Katiba kuona kama hoja za wananchi zinajibiwa, na pia kulinganisha na katiba za nchi nyingine kabla ya kupendekeza mpya.

“Haiwezekani ukapata katiba nzuri una watu 630 (kwenye Bunge), utapata vipi? Ndio maana nasema wale waliopitisha ile sheria, ambao ni Bunge lililopita, hawakuangalia mbele zaidi,” alisema. “Katiba inatengenezwa na watu wachache wataalamu. Kina Warioba ni watu waliozunguka kupata maoni ya wananchi. Tunayo Katiba (ya zamani). Sasa ilitakiwa kundi la wataalamu wachambue Katiba iliyopo, kasoro zilizopo kama zinajibiwa na hoja za wananchi.

“Hoja nyingine za wananchi kwa zilikuwa na jazba kwa kiasi fulani. Mtu anasema wanaume wasitupige. Sasa hilo unaweza kuweka kwenye katiba? Kwa hiyo ilitakiwa wataalamu wachache, very sober people (watu makini), very experienced (wazoefu).”

Alisema Bunge la Katiba lenye uwakilishi mpana linatakiwa lifanye kazi ya kuhalalisha kile ambacho kitakuwa kimechambuliwa kwa kiasi kikubwa na kupendekeza kitu ambacho kitakuwa kizuri.“(Bunge la Katiba) Si la kwenda kutengeneza Katiba. Bunge la watu zaidi ya 600 na umewapata kutoka kwa wafugaji, sijui makundi gani mengine, nani anajua Katiba?” alihoji. Alisema Bunge la Katiba linatakiwa likutane kwa siku zisizozidi tano kwa kuwa kazi kubwa inakuwa imeshamalizwa.

“Ingekuwa ni mimi, kwa kweli hii process (huu mchakato), kama unataka kuiendeleza, basi iendelee kwa utaratibu mzuri zaidi. Ninge-repeal (ningefuta) ile sheria, nilete sheria mpya ambayo ingesema sasa process iwe hivi, hivi, hivi,” alisema na kuongeza:

That money is not completely sunk (fedha zilizotumika kwenye Bunge la Katiba hazijapotea zote). Kwa sababu tutatumia zile modules (Rasimu ya katiba na Katiba ya 1977), ingawaje kweli kipindi kile Bunge la Katiba fedha nyingi zilizopotea kuliko kama ingetumika kwa utaratibu huu. Alisema ni kwa sababu hiyo anashauri mchakato wa kupata Katiba mpya uanze kwa kufuta Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ili kuunda timu ndogo ya wataalamu itakayochambua katiba na rasimu.

Chanzo: Mwananchi

 
Well said Sumaye!!

It sounds good and brings a big logic
Bado hajatuambia hilo BMK likikaa kwa siku hizo tano idadi ya wajumbe inatakiwa kuwa wangapi? ili wahalalishe yale yaliyofanywa na wataalamu hap 10-30 anaopendekeza?
 
Bado hajatuambia hilo BMK likikaa kwa siku hizo tano idadi ya wajumbe inatakiwa kuwa wangapi? ili wahalalishe yale yaliyofanywa na wataalamu hap 10-30 anaopendekeza?
Soma paragraph ya pili ya habari hiyo. Paragraph ya pili mwishoni mwishoni.

Amesema angeunda timu ya wataalamu 20-30

Tujenge tabia ya kusoma kwa umakini. Tusiwe tuna-comment bila ya kujiridhisha
 
Soma paragraph ya pili ya habari hiyo. Paragraph ya pili mwishoni mwishoni.

Amesema angeunda timu ya wataalamu 20-30

Tujenge tabia ya kusoma kwa umakini. Tusiwe tuna-comment bila ya kujiridhisha
Sawa, ila amecriticize BMK kuwa na watu zaidi ya 600, badala yake wataalamu 20-30 wafanye kazi ya kuchambua maoni ya wananchi kutoka tume, kisha ndipo BMK likae kwa siku tano.

That's y I'm asking, kwa hizo siku tano hajatumbia idadi......sijui kama na wewe umeisoma habari na kuielewa.
 
Very good Sumaye...!!! Eg unamleta mkulima wa kahawa toka Kagera na mwingine wa Tumbaku toka Tabora, mfugaji wa Kimasai, unawaweka Dodoma kisha unawaambia tungeni KATIBA based on Warioba's constitution proposal...!!! Hao watu hata katiba ya sasa hawaijui... labda ndio wanaona for first time... wamekaa wanashangaa tu, hawajui nn kinaendelea... wala hawajui utofauti wa katiba pendekezwa ya Warioba na ya sasa... so hili ni kosa kubwa sana... Wataalam ndio wanatakiwa kuchambua na kutunga Katiba mpya... Full stop..!!

So, Sumaye kaongea jambo la muhimu sana... na Rais Magufuli i hope atafuata huu ushauri...
 
Jk alikuwa na lengo la kuwafaidisha marafiki zake na VIBAKA KAMA AKINA NAKONDA TU...JKT ni ɓomu....alitaka atumɓue kila shilingi aliikusanya....simply Jk=mchwa wa hazina.
 
Nakubaliana na hoja ya sumaye. Nadhani utaratibu ulikosewa. Kungeanza, Timu ya kukusanya maoni; kisha timu ya wataamu; kisha bunge la katiba na baadae kura ya maoni.

Ila nina tatizo na mfu wa kuunda timu zote hizo.

Tume hizi zote ziwe huru ili kukwepa mihemuko ya kisiasa, na kuingiliwa na dola au mtu yeyote.

Bunge la katiba litokane na wananchi, sheria iweke wazi kuwa wabuge na serikali iliyo madarakani wasiwe sehemu yenye ushawishi wa moja kwa moja ktk maamuz km ilivyokuwa kwa BMK liliopita.

Tume ya uchaguzi itakayosimamia zoezi la kura ya maoni napendekeza nayo iwe huru.

Namna hivyo twaweza pata muafaka wa kitaifa kuandika katiba mpya.
 
Hilo la kutumia timu ya watu 20 mpaka50 kina Tundu Lissu walilipinga na kutishia umwagaji damu,walisema katiba ya watu milioni 50 haiwezi kuandikwa na kigenge cha watu wasiozidi 20 tena nusu yake toka zanzibar,
Ikabidi professor asikilize mapendekezo ya ukawa ndio wakaja na sheria na muundo huu wa bunge la katiba
Mawazo haya ya sumaye akiwapa ukawa watasema ni msaliti
 
Tuseme tu ukweli Magufuli akiwa na nia njema na nchi hii , aangalie upya namna ya kutengeneza katiba mpya. Lakini akiendeleza pale BMK lilipoishia atakuwa anafuata utashi wa chama chake na historia itamhukumu

Ili kusiwe na MAJIPU ni vizuri Rasimu ya Warioba iletwe mezani na si ya Nyoka makengeza
 
Sumaye yuko sahihi, katiba ni suala la kitaalam na siyo populist issue
Naungana aslimia mia kwa mia na Sumaye maoni ya wananchi yalikwishatolewa wataalamu wakae wauyaanalyse , wathesesize watuletee Katiba. Tena Sumaye asiwe na wasiwasi eti kwa kuwa yuko Upinzani kwa hili Mh. Magufuli atalipokea kwa mikon miwili kutokana na sababu mbalimbali. Moja aliyoiesema Mh. Sumaye na uzuri Mh. Magufuli antrust na wasomi wala hana inferiority complex as yeye mwenyewe ni kicwa. Atachukua wasomi wachache waliobobea wenye uzalendo ( na hili mh. analizingatia sana) waiandike katiba based on maoni ya wananchi. Wale wana siasa wanaojidai wanawakilisha wananchi kumbe wako kwa ajili ya maslahi yao, tupa kule!
 
Sumaye bwana wakati yupo ccm hakuyaona haya......
Hilo alishalikiri, ukiwa CCM unazibwa mdomo na macho inaachiwa vitundu vidooogo vya kuingiza pumzi tu! Ila ukijaribu kutanua hivyo vitundu basi wanaviziba kabisa, una rest in peace!
 

..uteuzi wa Dr.Mwakyembe unaweza kuonyesha Raisi ana msimamo/mtizamo gani kuhusu suala la katiba mpya.

..Mwakyembe naye amehojiwa anasema suala la katiba siyo kipaumbele cha Raisi.

..anadai eti katiba mpya haiwezi kuwaletea wa-Tz chai na mkate wakiwa kitandani!!

..kwa hiyo mpaka hapo utaona kwamba tayari tumeshakwama ktk suala hili la katiba mpya.
 

Hivi kwani huo mchakato wa katiba ndo utasababisha mambo mengine yote yasimame?

Huyo Mwakyembe ni bure kabisa!
 
Hivi kwani huo mchakato wa katiba ndo utasababisha mambo mengine yote yasimame?

Huyo Mwakyembe ni bure kabisa!

..mimi sikutegemea waziri yeyote yule ktk serikali hii azungumze utumbo aliozungumza Mwakyembe.

..tukikubaliana na Mwakyembe, basi tusije tukalalamika siku Prof.Muhongo naye akisema umeme siyo kipaumbele cha Raisi.

..Prof.Mbarawa naye anaweza kuja kusema barabara na reli siyo vipaumbele vya Raisi.

..waziri wa ardhi naye anaweza kusema migogoro ya ardhi siyo kipaumbele, kipaumbele ni elimu bure na kukusanya mapato.

..etc etc.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…