Kutokana na idadi kubwa ya abiria wa moshi kuelekea Dar es salaam , tiketi zinauzwa kiholela huku nauli ya daraja la kawaida ikiwa ni tsh elfu 30 badala ya elfu 20 iliyopendekezwa , nimeshuhudia wakiwaambia abiria nauli iliyochapishwa ni elfu 20 ila wanatakiwa kutoa elfu 30 na iwe ni siri yao , abiria wanalipa kwani idadi ya abiria hapa ni kubwa sana , tafadhali SUMATRA KILIMANJARO tunaomba mfanye kazi yenu kama inavyotakiwa kwani huu ni wizi.