Suma JKT, askari wenu wakorofi mitaani

pombe kali

JF-Expert Member
Jun 28, 2014
267
525
Tafadhali bandiko hili liwafikie uongozi wa Suma JKT, hawa askari wanashindwa maadili. Wanapata wakati mgumu wa kuishi huku uraiani.

Kwanza hawalipi nauli kwenye daladala wakiulizwa wanasema wao ni JKT. Ninachojua mimi Suma JKT ni kampuni na wala sio kikosi chochote cha ulinzi na usalama.

Nimeshuhudia zaidi ya mara mbili wakigoma kulipa nauli na kuanzisha fujo. Tukawasiliana na kikosi cha usalama barabarani ambapo walitushauri kuwapeleka kituo cha polisi. Leo tena nimeshuhudia dereva wa daladala akiwakwepa walikuwa kituoni wakisubiri gari ambapo walikimbiza gari mpaka kwenye foleni ila abiria tuliweza kuwadhibiti.

Tafadhali uongozi wa Suma JKT ufuatilie hili ikiwezekana wavae majina au namba ambazo zitawatambulisha kuturahisishia kuripoti matukio.

Asante
 
Hakuna mahali popote au sheria yoyote ya nchi hii inayomruhusu mtu kwa cheo chake au kazi yake kutolipa nauli katika usafiri wa Umma.
Ni mazoea ya kipumbavu tu mtu kutolipa nauli wakati unalipwa mshahara huku mwanafunzi wa darasa la kwanza analipa nauli.Hutaki kulipa nauli use your private transport or your force's transport.
Samahani kwa kuwakwaza watu ,ukweli unauma najua
 
Ni Kweli kabisa. Nadhani wanajidanganya kuwa wao pia ni sehemu ya majeshi yetu. Wakiona hizo herufi JKT ktk mashati yao wanajiona ndio makanali sijui au makamishna? Kuna m1 nusu nimtie makofi juzi juzi tu
 
Hakuna mahali popote au sheria yoyote inayomruhusu mtu kwa cheo chake au kazi yake kutolipa nauli usafiri wa Umma.
Ni mazoea ya kopumbavu tu mtu kutolipa nauli wakati unalipwa mshahara huku mwanafunzi wa darasa la kwanza analipa nauli.
Hahahaha hapa ndo kuna tabu ya kufikiri
 
Kusema ukweli jeshi letu limekosa nidhamu kwa kiwango kikubwa sana....

Vijana wakishavaa yale magwanda yao....wanabadilika wanajiona kama miungu watu.....
 
ni ukweli mkuu..lakini SUMA JKT ni sawa na JKT sema hawa huwa wanaajiriwa kwenye makampuni hivyo ni askari kama askari wengine
 
ni ukweli mkuu..lakini SUMA JKT ni sawa na JKT sema hawa huwa wanaajiriwa kwenye makampuni hivyo ni askari kama askari wengine
Hapana mkuu hawa si km askari wa JWTZ au JKT(VIJANA WAKUJITOLEA AU WA KWA MUJIBU WA SHERIA)hawa nia askari waliokwisha shiriki mafuzo ya JKT wakaajiriwa na JKT SUMA GUARD,hvyo sidhani km wana haki ya kutolipa nauli wanajifananisha na kipindi wakiwa km wapo JKT kumbe walishatoka huko na ss wapo SUMA GUARD kinachotakiwa ni wakuu wao kuwapa miongozo kuwa wao ni sawa na ULTIMATE SEC nk,cuz na uhakika mtu yeyote aliyepitia JKT anaweza ajiriwa SUMA GUARD
 
Tuwagonge, kuanzia police, jeshi na jkt wote wanaotaka kupanda gari bure.
 
Ni Kweli kabisa. Nadhani wanajidanganya kuwa wao pia ni sehemu ya majeshi yetu. Wakiona hizo herufi JKT ktk mashati yao wanajiona ndio makanali sijui au makamishna? Kuna m1 nusu nimtie makofi juzi juzi tu
Then ikawaje usimtie makofi sasa?
Acha kujifurahisha wewe
 
Najiulizaga kwa sauti mbona kwenye ndege hakunaga mbwembwe?
 
Kwanza ukiona sums jkt kavaa uniform ujue hao ni mgambo ndo huwa wanasumbua sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…