Sukari imepanda Bei. Hapo ulipo bei ipoje?

NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
3,862
5,693
Muwe na alasiri njema!

Mtwara kiongozi, nimeshuhudia leo. Naambiwa maeneo ya Lindi nako ni hivyo hivyo ingawa kuna wanaozuga kwa kuuza 4,800/=

Ila nchi za afrika bana,yaani kila duka unakuta kuna sukari inatoka brazil . Sasa najiuliza hivi viwanda vyetu sukari vinaweka wapi baada ya kuzalisha?

Sasa fikiria hata wewe sukari itoke brazil ni kilometer ngapi mpaka hapa? Halafu zingatia na shilingi yetu ilivolegea dhidi ya dollar
Aisee sukari inazidi kupaa kwa kasi kwelikweli sijajua shida ni nini maana binafsi sijasikia taarifa kutoka kwa mamlaka, huku kwetu sukari 4000 Tz shilingi kilo moja
Jana asubuhi nilimtuma mtoto na shillingi 8,400 kununua sukari kilo tatu nikifahamu mteja wangu huwa ananiuzia sukari Tshs. 2,800 kwa kilo.

Mtoto alirudi mikono mitupu akanieleza kuwa sukari imepanda bei na sasa kilo moja ni Tsh. 3,500. Nilishtuka sana na mpaka sasa sijaamini.

Nina maswali yafuatayo kwa Serikali:

1. Ongezeko hili limesababishwa na nini?

2. Je, kama Serikali mlitoa taarifa kwa wananchi kuhusu ongezeko hili?

3. Je, mnajua wananchi wengi hawataimudu bei hii?

4. Je, Serikali haijui kuwa Wananchi tunakosa imani na Serikali yetu?

Ninaomba majibu ya maswali yangu.

Habari zenu,

Hivi ni kweli kwamba sukari 1kg ni 5000 au ni mtaani kwetu tu?

Nilinunua sukari 15kg kwa muda kidogo, leo nimeenda tena kununua aisee nimestaajabu sana.

Bado kuna watu wanazuia maandamano kwenye hii nchi.

====

Moshi/Arusha. Sukari inakwenda wapi? Ni swali linaloumiza wengi, huku wakazi wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro wakitaka vyombo vya usalama kuchunguza biashara hiyo, wakisema licha ya bidhaa hiyo kuingizwa sokoni, bado bei imesimama kati ya Sh3,500 na Sh4,000 kwa kilo.

Katika sakata hilo, Mwananchi limeelezwa kuwa huenda ama inafichwa, kusafirishwa kimagendo au baadhi ya wazalishaji wanaitumia kama ya viwandani.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu alipoulizwa na gazeti hili jana, aliwataka wafanyabiashara wasigombane na Serikali na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watakaokiuka bei elekezi kwa kuwa sukari ipo ya kutosha.

"Sukari ipo na sisi kama Serikali ya mkoa tukimkamata mfanyabiashara yeyote (ameificha) tutachukua na sukari yake. Huwezi kuwaonea wananchi. Tutapita kwenye maduka kuwakagua wanaojipangia bei yao na kuwaumiza wananchi.

"Wafanyabiashara msitake kugombana na Serikali kwa sababu ya sukari," alisisitiza Babu.

Mkoani humo, hali haitofautiani sana na mikoa ya Arusha na Manyara, ingawa bei ya juu ni Sh4,000 kwa kilo katika maeneo machache, kwingineko inauzwa Sh3,500 kwa kilo katika maduka ya rejareja.

Mwajuma Jumanne, mkazi wa Msaranga katika Manispaa ya Moshi alisema haelewi tatizo ni nini, lakini taarifa alizonazo ni kuwa kiwanda cha TPC kinazalisha sukari na kuingiza sokoni, akitaka vyombo vya usalama kuingia kazini kuchunguza.

“Naambiwa kwa majirani zetu hapa (nchi jirani) kuna uhaba wa sukari, maana katika viwanda 15 walivyonavyo kama sikosei, wanasema vilivyokuwa vinafanya kazi ni vitatu tu. Bei yao kilo moja haipungui Sh5,000. Tatizo ndipo linapoanzia,” alisema Mwajuma.

TPC nao washangaa

Mtendaji wa Mkuu wa Kiwanda cha Sukari TPC, Jaffary Ally alipoulizwa jana nini hasa kinasabisha sukari kuadimika mikoa ya kaskazini licha ya kiwanda kufanya kazi, alisema hawezi kulifahamu hilo.

“Ninachojua sisi tumewauzia (sukari) distributors (wasambazaji wakubwa) ili nao waisambaze, sasa mimi nafikiri hao ndio waulizwe. Sisi tumetimiza wajibu wetu na bei ya kiwandani hapa haijafika Sh2,100 kwa kilo,” alisema Jaffary.

“Kwa siku 30 mahitaji ya mikoa mitatu ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara ni tani 8,100 na sisi tumeingiza tani 8,200, sasa upungufu unasababishwa na nini? Naomba uchunguzi ufanyike sukari inaelekea wapi,” alisisitiza.

Inapelekwa kwenda nje

Wakati mtendaji huyo wa TPC akieleza hayo, uchunguzi unaonyesha kumekuwepo na upungufu wa sukari ya viwandani na kuna baadhi ya viwanda vinatumia kwa siri sukari ya kawaida badala yake.

“Mimi nahisi na hili naomba vyombo vitusaidie. Nina wasiwasi na mambo mawili hapa. Moja kuna viwanda vinatumia hii badala ya ile nyeupe au kuna inayosafirishwa kimagendo kwenda nje,” alidai Marysiana Charles.

Mkoa wa Kilimanjaro unakadiriwa kuwa na mipaka isiyo rasmi zaidi ya 300 katika maeneo ya Kamwanga, Tarakea, Useri, Mashati, Machimbo ya Pozorana, Madarasani na Kitobo.

Mwananchi mwingine anayeishi karibu na njia hizo, alilidokeza gazeti hili kuwa sukari ya Tanzania imekuwa ikisafirishwa kwa wingi kwenda nchi jirani kupitia njia hizo na usafiri pekee unaotumika ni bodaboda.

“Hata kama una tani moja, wewe mwite kiongozi wa bodaboda mmoja mwambie nataka hii sukari ivuke mpaka. Mbona rahisi tu. Yaani shehena yote itavushwa kwa pikipiki. Huu sasa hivi ni mradi mkubwa,” kilidokeza chanzo chetu.

“Sasa hivi biashara hapa ni sukari, inaenda kimagendo kwenda nchi jirani na huku wanaingiza mafuta ya kula. Hizi ndizo biashara kubwa za magendo kwa sasa,” kilieleza chanzo hicho, kikidokeza kuwa baadhi ya mgambo ni washiriki wa magendo hiyo.

“Mkimlaumu RPC (Kamanda wa Polisi mkoa) au RCO (mkuu wa upelelezi) au watu wa usalama mtakuwa mnawaonea. Hii ni syndicate (njama) ya baadhi ya wafanyabiashara, viongozi wa vijiji, mgambo na askari polisi, wanawazunguka hao wakubwa,” ilielezwa.

Askari mmoja mstaafu, alisema ili kudhibiti uvushaji huo wa sukari, vyombo vya usalama viwabane viongozi wa vijiji na mgambo endapo sukari itapita katika maeneo yao.

Wananchi wafunguka

Wakizungumza na gazeti hili jana, baadhi ya wananchi jijini Arusha walisema sukari inauzwa kati ya Sh3,500 hadi Sh4,000 kwa kilo, huku baadhi ya wafanyabiashara wakieleza kuadimika kwa bidhaa hiyo wakishuku wenzao kuificha.

Amina Ahmed, ambaye anafanya biashara ya duka la jumla na rejareja, alisema kwa sasa bei imeshuka kutoka Sh5,000 mwezi uliopita hadi Sh4,000 na kuwa bidhaa hiyo bado haipatikani kwa wingi.

"Kiukweli hatuelewi kwa nini imekuwa hivi, sukari inapatikana japo si kama awali. Inapatikana kiasi tu na ndiyo inasababisha bei kuwa juu nje ya bei elekezi. Hii hali si Arusha tu, hata Moshi na Manyara," alisema Ahmed.

Kwa upande wake, Joachim Kimario, anayefanya biashara katika soko kuu la Arusha, alisema sukari haipatikani kwa wingi kama ilivyokuwa inapatikana awali kabla ya viwanda kusitisha kwa muda uzalishaji.

"Tunaamini kuna baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu wanaficha sukari, hili linatupa hasara na tunaumizana kwa kupandisha bei hadi ilifika hatua tunauza sukari zaidi ya Sh3,000 ambayo ndiyo ilikuwa bei ya kawaida," alisema Kimario.

Jitihada za kumpata mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongela ili azungumzie hali ilivyo mkoani mwake zilishindikana baada ya simu yake kuita bila kupokewa.

Credit: Mwananchi

Pia soma: Sukari yafika shilingi 5,000 kwa kilo moja
 
Back
Top Bottom