Sugu akutana na Mzee Joseph Butiku, atoa ofa kwa Taasisi ya Mwl Nyerere

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
126,274
240,672


Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini, Mwekezaji na Mfanyabiashara wa Kimataifa , Bilionea Joseph Mbilinyi , amekurana na kuchota busara kutoka kwa Mwenyekiti wa Mwl Nyerere Foundation , Joseph Butiku , ambaye alifunga Safari kumtembelea Sugu Jijini Mbeya

Watu hao wazito wamezungumza mambo mengi kuhusu Mustakabali wa Taifa ikiwemo Katiba Mpya .

Mwisho wa Mazungumzo hayo Sugu ametoa ofa kwa Taasisi ya Mwl Nyerere kwamba , ikiwa siku zijazo wataamua kufanya Makongamano yao Jijini Mbeya basi yuko tayari kuwapatia Ukumbi wa kisasa kabisa wenye vifaa vya kisasa kabisa uliomo ndani ya Hotel yake ya nyota 3 bure kabisa kwa kipindi chote cha kongamano hilo hata kama ni mwezi mzima
 
Eti Sugu nae sasa ( siku hizi ) anaitwa Bilionea. Najua kuwa Sugu ana Hela ( GENTAMYCINE simfikii ng'o ) ila bado hana Hadhi ya Kuitwa Bilionea unless labda hatujui maana ya Bilionea au tunahitaji Msaada wa Kiufafanuzi kutoka BAKITA na BOT juu ya maana na dhana nzima ya neno Bilionea na Mtu Kuitwa Bilionea.

Kwangu Mimi Sugu akiitwa Mfanyabiashara au Mjasiriamali mwenye Mafanikio nitakubali tena kwa 100% ila leo hii kumuita Sugu Bilionea ni Kulidharau neno husika na Kuwadharau wale Mabilionea hasa kama akina Bakhressa, Mo Dewji, Rostam, GSM na wengineo baadhi.
 
Kwa tafsiri ya kawaida Bilionea ni yule anayemiliki mabilioni ya Hela , sasa wanazidiana , kuna anayemiliki bil 500 na mwingine bil 5 na wako wa bil 900

Umasikini siyo baraka ni laana
Sidhani kama hata anaelewa anachoongea. Hafahamu chochote kuhusu liquidity.

Hafahamu kuwa kwenye category ya ubilionea, ni kuwa na assets zenye thamani ya bilioni moja. Both cash and cash equivalents, real estate, and business and personal property. Vyote vikiwa na thamani ya bilioni moja na kuendelea ni bilionea.

Back to the real topic, nawakubali wote wenye kupigania katiba mpya.
 
Hata hueleweki unalalamikia nini hasa kwa Joseph Mbilinyi kuitwa bilionea..

Kama utajiri wa Mr Sugu wa fedha + mali + investments uko 1+ bilioni, basi ndugu Joseph Mbilinyi a.k.a Mr Sugu ni miongoni mwa ma - bilionea..

Huhitaji kwenda BAKITA ili uelezewe na kuelewa hili...

Kwa hiyo hakuna kosa la kimantiki kumwita Mr. Sugu kuwa ni bilionea. It's absolutely correct unless uwe na shida zako binafsi za kiufahamu...

Na kama ndivyo, basi ni halali yako kuwaona BAKITA wakuingize darasani...!!
 
Vijana wengi masikini wa Tanzania hawaamini kama mtu ambaye baba yake sio kiongozi ama labda si kutoka familia ya weupe , wahindi au waarabu hawezi kuwa Tajiri
 
Umekurupuka mkuu
Fikiri kabla ya kuandika(FKK)

Bilionea sio physucal cash tu

Utajiri wa mtu au Taifa au Total wealth unapimwa kwa cash and non cash equivalent

Mfano
Hotel ya sugu thamani yake ni USD kiasi gani?
Nyumba anayoishi na kuzimiliki ni USd ngapi?
Biashara zake zina thamani kiasi gani?

Share na Bonds anazomiliki zina thamani kiasi gani?

Pesa zake kwenye mabenk zikiwemo Fixed deposit zina kiasi gani?

Mziki wa sugu,(Nyimbo zake ) yaani property right zina thamani kiasi gani?

Jumlisha yote hayo ndio utapata thamani ya sugu
 
Hata kwenye mafanikio bado hajafikia 100%. Kuna siku alitudanganya ana biashara zake za malori alitaka kuzihamishia nchi jirani. Ila tunavyomfahamu yule bwana hata angekuwa na biashara za bajaj tu kila siku tungeona mitandaoni. Anajaribu kupambana ila anaweka sifa nyingi fake kuliko mapambano yenyewe.

Sent from my SM-A225F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…