Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 126,227
- 240,557
Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini, Mwekezaji na Mfanyabiashara wa Kimataifa , Bilionea Joseph Mbilinyi , amekurana na kuchota busara kutoka kwa Mwenyekiti wa Mwl Nyerere Foundation , Joseph Butiku , ambaye alifunga Safari kumtembelea Sugu Jijini Mbeya
Watu hao wazito wamezungumza mambo mengi kuhusu Mustakabali wa Taifa ikiwemo Katiba Mpya .
Mwisho wa Mazungumzo hayo Sugu ametoa ofa kwa Taasisi ya Mwl Nyerere kwamba , ikiwa siku zijazo wataamua kufanya Makongamano yao Jijini Mbeya basi yuko tayari kuwapatia Ukumbi wa kisasa kabisa wenye vifaa vya kisasa kabisa uliomo ndani ya Hotel yake ya nyota 3 bure kabisa kwa kipindi chote cha kongamano hilo hata kama ni mwezi mzima