Witmak255
JF-Expert Member
- Feb 5, 2019
- 3,264
- 5,417
Jana mchana ninepigiwa simu na ndgu yangu ambae amemaliza kidato Cha sita hivi majuzi, amerudi kijijini kwa Wazazi wake baada ya kumaliza masomo yake ya advance. Alipigia kuniomba nimsaidie Tsh 15,000/= ambayo ataitumia Kama nauli na malipo ya kuhakiki cheti chake Cha kuzaliwa ili aweze kuomba mkopo wa elimu ya juu mda ukifika.
Binafsi sikujua Kama Kuna japo ni Jambo jema kwa nchi na Wala Sina Sina shaka nalo kabisa, Ilinibidi niingie kwenye website ya hizi taasisi nipate habari zaidi, nikakuta ni kweli.
Kilichonishangaza, unaruhusiwa kuhakiki kwenye ofisi ya wilaya uliyochukulia tu na Kama uko mbali na ofisi uliyochukulia basi unawasilisha nakala yako ya cheti uliyoiscan kwa email ya ofisi husika baada ya kufanya malipo bank kwa account uliyoelekezwa ya Tsh 3000/= then ndio maombi yako yanafanyiwa kazi.
Imebidi niujiulize, Ina maana RITA wameshindwa nini kulink database yao ya majina ya watu waliowapa vyeti bodi ya mikopo? Hawa HELB wao wangeingiza namba za vyeti tu kwenye system, then system inaverify Kama cheti ni chenyewe au feki,... otherwise watuambie Kama hiki pia ni chanzo Cha mapato, haiwezekani ulipie kwenye kuomba cheti halafu waliokupa cheti waitishe UHAKIKI tena wakutoze pesa nyingine?
Kwa ulimwengu wa Sasa nisingetememea mtu aliyepata cheti Cha kuzaliwa NANJILINJI, halafu kimaisha Yuko MWANZA imlazimu tena kusafiri kwenda NANJILINJI kwa kukihakiki, Ina maana RITA hawana database ya vyeti wanavyotoa? Kama wanayo kwa nini asihakiki huko aliko?, Kwa nini tupeane gharama na usumbufu usiokuwa na sababu Wala maana.
Then kwa nini huu uhakiki unatozwa pesa? Kwa nini isiwe bure? Hivi vyeti vinachukuliwa kwenu RITA kwa malipo ya pesa kulingana na umri wa mhusika, why mumtoze pesa tena kuhakiki cheti mlichokitoa kwa malipo? Yaani NECTA au chuo nilichosoma wahitaji kufanya uhakiki wa cheti walichonipa, wanitoze pesa?
Serikali inapaswa kuangalia Sera zake kwa raia, sio kila Kitu kumkamua mnyonge, Uhakika RITA ulipiwe, kuapply mkopo ulipie haijalishi utapata au la..!, Hili zoezi lingeweza kufanywa vizuri Sana hata bila malipo ya aina yeyote na kwa urahisi zaidi, najua kabisa pale RITA na bodi ya mikopo tena wabobezi kabisa wangeweza kufanya hii kazi kwa system tu.. otherwise mumeamua kwa makusudi kuongeza mapato kwa kuwakamua hawa wanyonge wenu.