Suala la Mali za waislam linawezakua kama mahakama ya kadhi!

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Hii ahadi aliyoitoa Mheshimiwa inanipa shida mno kila nikifikiria kuhusu ile ahadi ya mahakama ya kadhi kwa waislam nchini. Linaweza kuchukuliwa kama suala dogo lakini ni jambo zito mno.

Kama kweli mheshimiwa mkubwa ana dhamira ya dhati juu ya hilo basi mimi nina wasi wasi mkubwa kuibuka kwa mijadala mikubwa na mizito kuhusu mambo haya. Hii ilikua dhamira ya dhati kwa Mh au maneno ya kisiasa? nini impact yake katika taifa?

Sizifahamu mali za waislam wala sijawahi kuziona, wao ndio wanaozifahamu lakini nikiikumbuka ahadi ya mahakama ya kadhi ilivyoibua hisia na mijadala kwa baadhi ya watanzania sina la kuongea zaidi.
 
Huyu bwana mkubwa naona ameanza kampeni za 2020. Huko ameingia chaka au amechokoza nyuki. Amefufua mambo yaliyo lala na yakiamka si rahisi kuyalaza tena. Kama ni kutafuta sifa basi ametafuta sehemu siyo.
 
Asaidie na kanisa katoliki kurejeshewa Mali zake
Asaidie na KKKT kurejeshewa Mali zake
Asaidie watu wenye asili ya India kurejeshewa Mali zao
Asaidie watu wote kurejeshewa Mali zao maana yeye ni rais wao wote.
Kila la kheri Mh.rasi
 
Neno moja tu la kiongozi mkubwa linaweza kuzua taharuki kubwa. Masuala mengine hua hayatolewi majibu pale pale.
 
Asaidie na kanisa katoliki kurejeshewa Mali zake
Asaidie na KKKT kurejeshewa Mali zake
Asaidie watu wenye asili ya India kurejeshewa Mali zao
Asaidie watu wote kurejeshewa Mali zao maana yeye ni rais wao wote.
Kila la kheri Mh.rasi
Dah, ni pagumu sana hapa kuliko tunavyofikiria.
 
Hapa Ukweli Kila Upande Una Dai Chake Kwa Serikali
Kama Anataka Kutenda Haki Asaidie Wote Bila Shinikizo
 
Hapa Ukweli Kila Upande Una Dai Chake Kwa Serikali
Kama Anataka Kutenda Haki Asaidie Wote Bila Shinikizo
Ndipo ugumu ulipo mkuu! Kama atatekeleza ahadi yake aliyoahidi, nashindwa kutazama mbele itakavyokua.
 
Hivi huyu magufuli anajua maana ya Mali za waislamu kweli? Mali za waislamu ni roho zetu mi naanza kuwaogopa mana wameruhusiwa warudishe Mali zao. Tutaanza kuchinjwa kama mbwa
 
Hivi huyu magufuli anajua maana ya Mali za waislamu kweli? Mali za waislamu ni roho zetu mi naanza kuwaogopa mana wameruhusiwa warudishe Mali zao. Tutaanza kuchinjwa kama mbwa
Usipotoshe umma. Kama huelewi kaa kimya
 
Wewe Gujalati, acha kuweka maneno ambayo hayana msingi wowote kama huyui mali za waislam kaa kimya tu. Ni muislam gani ambae atakuchinja eti kisa mali zao. Wenyewe wanajua mali zao ni zipi ndo maana.
 
Huyu bwana mkubwa naona ameanza kampeni za 2020. Huko ameingia chaka au amechokoza nyuki. Amefufua mambo yaliyo lala na yakiamka si rahisi kuyalaza tena. Kama ni kutafuta sifa basi ametafuta sehemu siyo.
Tunataka mahakama yetu ya Kadhi
 
Hii ni moja ya kauli ambayo haikufanyika tafakuri ya kina kabla ya kuitamka.Kwa kauli hii serikali ya ccm inakiri kuifahamu dhurma iliyofanyika dhidi ya mali za waislamu,sasa kama iliufahamu uharamia huu dhidi ya mali za waislamu,kwa nini ilimtesa,kumdharirisha na kumuweka kizuizini Sheikh Ponda ambaye alijipambanua kuwa mtetezi wa mali za waislamu ambao Magufuli amekiri kuifahamu dhurma hiyo dhidi ya Mali za waislamu alizokuwa anazipigania sheikh Ponda na wenzake?

Mheshimiwa Sheikh Ponda aliteswa,kudharirishwa na kufungiwa kizuizini huku akisafirishwa na idadi kubwa ya vikosi vya kijeshi kupelekwa Mahakamani kusikiliza shauri lake mithiri ya gaidi wa kimataifa?Kwa nini waendesha mashtaka wa serikali waliamua kumsingizia mtetezi huyu wa Mali za waislamu kosa la uchochezi na ugaidi?

Kama kiongozi mkubwa kabisa wa nchi amekiri kukifahamu kile alichokuwa anakipigania Sheikh Ponda na ameahidi "kuvaa viatu"vya Sheikh Ponda katika kuzirudisha Mali za waislamu zilizoporwa,sasa ni muda muafaka kwa wale wote waliothusika na uteswaji na udharirishwaji wa Sheikh Ponda kutoka hadharani wamsafishe,wamuombe radhi na kumlipa fidia kwa mateso waliomfanyia huku wakijuwa kuwa anachokisimamia ni hoja za msingi ambazo jana kwa kinywa chake Rais ametamka kufahamu dhurma zote zilizofanywa dhidi ya Uislamu na mali zake.
 
Dah maeneo mengi ya kanisa katoriki yamemegwa na kuwekwa makazi ila kwa busara ya viongozi wa kanisa hili wameamua kuwaachia wananchi na kuyalinda yaliyopo sasa.. pamoja na kuwa na hati miliki mfano nyegezi mwanza parokia ya nyegezi pamoja na chuo kikuu cha saut lote ni eneo la kanisa mpaka karibia barabara kuu yaani pale nyegezi kona wakiambatana na jeshi.. lakini viongozi wameamua kuwaachia wananchi huku mengine yakiwa yametapeliwa kwa kuwa lilikuwa eneo kubwa..

Sasa najiuliza kanisa katoriki parokia ya nyegezi na kwingineko wakimpelekea mheshimiwa rais nyaraka za umiliki wa maeneo haya anaweza kuwasaidia..maana ni sehemu nyingi za kanisa hili zimevamiwa na kuwekwa makazi.
 
Ukiwa umekosea kuna njia za kujirekebisha. Nadhani kuna vitu vinarekebishwa sasa njia inayotumika sio nzuri.
 
wapewe ya kadhi...si watakua wanaigharamia na wanahukumiana wenyew....
 
Nadhani mali zinazoongelewa hapa ni zile ambazo zimekwenda mikononi mwa watu binafsi kwa njia za ulaghai na sio vinginevyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…