Katika pita pita zangu kwenye mitandao ya kijamii na kwenye spaces za Twitter zinazoendelea sasahivi za wanaharakati na wanasiasa wa vyama vya upinzani, nimeshtushwa sana na namna viongozi na wanaharakati wa upinzani wanavyomuunga mkono gaidi Hamza aliyeua Watanzania wenzetu 4 na kuwajeruhi watu wengine 6.
Nimeshangaa kuwaona watu wanaojigamba kuipenda nchi hii kama akina Lema, Fatma Karume, Mbatia na wenzao kumshadadia Hamza na kuonyesha kumuunga mkono kana kwamba kafanya jambo la maana na lenye tija kwa nchi. Leo Hamza anapata uungwaji mkono na watu wa upinzani kwa sababu ya kuua askari na Watanzania na kujeruhi wengine. Hii ni aibu na najisi kwa nchi.
Cha kushangaza watu hawa wa upinzani wanamshadadia Hamza kwa kushikilia maneno ya kubumba ya mitandaoni kwamba Hamza alidhulumiwa na polisi. Sasa kama Hamza alidhulumiwa kama wanavyobumba, njia ya kupata haki kwenye nchi hii ni kuchukua bunduki na kuanza kufyatulia watu?
Viongozi na wanaharakati wa upinzani mnaomshadadia na kumsapoti Hamza mnajiabisha sana mbele ya Watanzania na sasa mnajidhihirisha mbele za umma jinsi msivyolitakia mema Taifa hili.
Watu mnaojigamba mnaipenda nchi hii leo mnaibuka kumuunga mkono mtu aliyeleta taharuki kwa nchi, mtu aliyepeleka simanzi na umaskini kwa kuua Watanzania wenzetu ambao walikuwa wanategemewa na familia zao na Jamii yetu halafu nyie mnamuunga mkono kwa hoja nyepesi na za kusikia tu kwenye mitandao kwamba eti Hamza alidhulumiwa. Wapinzani mnajiaibisha sana mbele za Watanzania.