Studio ya bunge kikaangoni kwa Kusambaza Clip ya Kitwanga akiwa amelewa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,717
55,819
Maafisa wa bunge waingizwa matatani, studio ya bunge nayo kikaangoni. NI Suala la kuonyesha 'clip' ya aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani chales kitwanga na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Hivi karibuni, Waziri wa mambo ya ndani alivuliwa uwaziri, kwa kile kilichodaiwa ameingia bungeni akiwa amelewa.

Baadae Kwenye mitandao ya kijamii, ikaonekana video liyodaiwa inamuonesha Waziri aliyetimuliwa akiwa amelewa.

Sasa wanatakiwa watajane aloisambaza hiyo video.
 
Maafisa wa bunge waingizwa matatani, studio ya bunge nayo kikaangoni. NI Suala la kuonyesha 'clip' ya aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani chales kitwanga na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.
HEBI IWEKE HAPA TUAMINI
 
Charles kuingia bungeni bila kunywa Kitwanga huwa anakosa confidence
 
Mbuzi wa bwana kheri kala shamba la bwana kheri wakiwa wanachungwa na mtumishi wa bwana kheri katika mtaa wa bwana kheri na hiyo ni kesi itaamuriwa na bwana kheri mapema kwenye uwanja wa bwana kheri. Kuna kesi hapo???
 
hawa jamaa wa bunge ni wakupongeza sana maana wapo upande wa wananchi.

Kufunua siri ya kilichosababisha bunge lisirushwe live.

Kumbe ni hili jamaa wapige viroba vyao.
 
Hivi hawa wataacha lini kuficha maovu ya viongozi...hivi taifa hili litaponaje kama ukweli kwao ni kosa na kosa kwao ndo ukweli?
 
Hii habari inanipa mashaka, ni clip gani unazungumzia? Kama ni clip ya kuwasilisha budget au ya waziri kujibu swali hapo kuna kipi cha kumtia mtu matatani?
 
Binafsi siamin sana kama video ya kitwanga kuonesha kuwa amelewa ilionwa mh rais lazma kuna mashushushu mule ndio wamemtonya na ndio ilikuwa inatafutwa sababu tu ikapatikana maana bunge halioneshwi live ni recorded muda huo presidar lazma awe amepumzika
 
Na kama angekuwa dereva wa bus je au askari katika lindo hao waliorecord si wangepongezwa!
 
Kuna sura nyingine hazihitaji kipimio cha kitwanga ukimwangalia tu unajua kakitwanga, mfano yule waziri wa starehe aliepita do
 
Wameacha kudili na walevi bungeni sasa wanatafuta aliyetoa habari, baadaye watamtafuta aliyepeleka taarifa kwa Raisi mpaka Mlevi mwenzao akaondolewa kwenye uwaziri, nchi hii bana haina ukame wa vituko
 

sio mashushu...ilikuwa ni aibu na wabunge wote waliona...sasa kwani hujui kuwa waziri mkuu yupo pale bungeni na yeye anaona....aliiaibisha serikali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…