Hili swali nimejiuliza kwa muda mrefu kidogo.
Kuanzia pale kwenye sherehe za kumuapisha Rais wa Zanzibar, Chama kikawaandaa makada na sare zao kwenda kushangulia.
Kwenye sherehe za kitaifa wanavaa sare zao na kushangilia.
Zinazinduliwa safari za ndege wanavaa kijani na kofia za chama.
Kisha wanatuambia kwamba wananchi wengi wamejitokeza kwenye tukio husika wakiwa na nyuso za furaha.
Hivi huyu (au hawa) jamaa (statergist) wa chama, kwa nini asiandae makada na kuwaambia wavae nguo za kawaida na baadhi yao wavae sare ili kuonesha mchanganyiko (hata kama si wa kweli).
Kwa mfano, mmepanga makada 100, 15 wavae sare na waliobaki wasivae. Ukifanya hivi utaonesha kwamba wananchi wasio na chama au wapinzani wameshiriki tukio husika. Vinginevyo mtaendelea kuwapa credit waongeaji kwamba washiriki ni wanachama tu.