Money Penny
JF-Expert Member
- Jun 20, 2016
- 17,280
- 16,556
SEHEMU YA 1
A. NINAITWA MTUMISHI PAPA
Mtumishi Papa:
Penny wewe unapenda stori jaman sijakuona sikunyingi ujue!
Money Penny: basi tukasalimiana hapo wee tukajikumbushia ya zamani akyanani sikuamini Patric amekuwa Mtumishi wa Mungu
nakuambia kweli mpenzi msomaji Patric namwelewa kuliko maelezo, ni wale best friend wa zamaaan kabla sijaolewa nikiwa mafiaaaa (mtundu-mkorofi)... huyu jamaa Patric alikuwa ni noumeeer alikuwa na roho ngumu vibaya mnooo... watu wa kwenye shishtimu walishamtumiaga sana mpaka tukahisi yupo huko lakini nahisi yupo ngoja kwanza niendelee na stori utajaza mwenyewe mpenzi msomaji!
Patric Darasani alikuwa Kilaaaazaaaaa namfundishaaa anafeli nampiga pindi anafauluuu... tukamaliza form 6 sikumwona tena mpaka siku moja natoka zangu ofisi moja Posta namwona anapita amevaa suti nyeusi kwasababu nilikuwa nimemzoeaaa nikamwita bila wasiwasii wewe PAPAAAAA, hakugeuka nikarudiaaaa hakugeukaaa nikamwita kwa mara ya mwisho huku watu wananiangalia na walinzi wa ofisi wameshaanza kusogea nikaita we PATRIIIIIIIC PAPAAAA ndio akageuka, aliponiona hakushtuka akaondoka walikuwa na wenzake 3 wamevaa suti nyeusi na miwani meusi ( asomaye na afahamu)
Basi Penny bila mafanikio nikaondoka zangu, kufika nyumbani napokea simu naskia ananiita we PAPA mamboooo?! ulikuwa wapi nyau we nakutafutaa!?
sikuelewa Patric alipata wapi mobile no yangu lakini alikuwa nayo tukaomgeaaaa akaomba anione usiku huo huoooo maana alfajiri anaamsha anaenda KUWAIT
Money penny tena, nikajongea fastaaa Serena Hotel!... tukasalimiana, tunakumbatiaaaanaaaa, tunachekaa kama watotooo!
baada ya kula na kunywa Patric akafungukaaa
Papa: Penny unajua umeniharibia sana pale umeniita nilikuwa kazini, kazini wananiitaga PAPARAZI ila marafkizangu wananiitaga PAPA kwasababu yako Penny, ujue Penny mimi na wewe vilikuwa vinaiva sana tulipokuwa shuleni, mpaka kunipa jina la Papa na kuwaambiwa office mate waniite papa yote ni kwa ajili yako,
Money Penny: i know! enhe niambie unafanya kazi wap umepataje kazi wakati sisi bado tupo IFM tunasoma tunasotaaa na kiadvance diplomaa?!
Papa: we acha si unajua form 6 nilipataga div 0.. nikatoka pale nikaenda kujiunga na jeshi, nikapigaaa nikapata kazi
Money Penny: mbona hauna mavazi ya Jeshi sasa? naona umepiga suti mara Tshirt za form 6 vepee?
Papa: nilipokuwa Jeshi pakanishinda mafunzo magumuu na vile nilikuwaga kimbaombao nikaacha katikati nikasepa, baadae akaja mzee mmoja akaniomba nirudi nikitoka hapo atanipa ajira! basi nikaenda kumalizia kwa heshima na usimamizi wa yule mzee nikafaulu nikarudi uraiani nikasota mwaka yule mzee nikaona kama amenidanganya kumbe sio kweli
Baada ya mwaka nanusu yule mzee akarudi! akaniambia nisamehe mwanangu niliumwa nikapoteza simu ila kwakuwa kwenu napajua ndio nimekuja, kazi yako bado ipo ndioo nimepewaaa nimeanza miezi 6 ijayo... nafanya kitengo maalum uje unisalimie akanielekeza ofisini kwao akaniambia nasafiri naenda KUWAIT nikirudi nakualika uje!
Money Penny: nikachokaa! cha, huyu kilaza amekuwa mtu mkubwa anavuta hela ndefuuu macho yakanitokaaa nikamuomba nikimaliza shule aniweke hata BANK jamaaa njaa inauma si unajua tenaaa!
Papa: akacheka sanaa aaah Penny nimekumiss sana we maliza shule nitakusaidia!
Baada ya usiku ule hatukuonana kweli akasafiri.. ikapita miaka 2 nikapata tena simu ya PRIVATE NO, nikajua tu ni yeye, akaniambia njoo Kempinski nimekumiss mtoto mzuri, ah ngoja kwanza nitakupigia simu ikakatwa, sikumsikia mpaka miezi 6 ilipopita akanipigia na simu ya TTCL we PAPAAA njooo Kanisa flan nakusubiria ukichelewa naondokaaa!
Money Penny: nikajongeaaa! huko ndani ndani dar es salaam silitaji jina kabisaa! dah kufika naona kanisa la udongoo... heee we Papaaa, vepee? mbona upo huku umekuja kuua mtu au?
Papa: akacheeekaaa! Penny bwana, haya karibu, nikapewa kigoda nikakaa nashangaa watu wanakuja wanamsalimia shikamoo Mtumishi shikamoo Pastor, shikamoo Mchungaji
Papa anawakaribisha pale karibuni na maneno ya kilokole
Money Penny: namshangaa huyu muhuni kachanganyikiwaa?
hapo natamani kucheka sina mbavu wai kwani huyu Papa kawa mchungaji saa ngapi?
Papa: Penny bwana mimi ni mchungaji msaidizi kwenye hili kanisa la Waenda Mbinguni
Money Penny: kwa mshangao nikamjibu naonaa! kwanini?
Papa: Penny ile kazi nilishaiacha stress kibao nikaamua kumrudia Mungu, riziki popote penny, Mungu atanitunza
Money Penny: aisee! hongera sana kwahiyo sasa mama mchungaji hapa yupo wapi? namaanisha mkewako
Papa: hilo ndio nimekuitia best wangu najua unazo akili, kuna demu nimemwona hapa nimempenda sana, nisaidie kumchunguza tafadhali, ila niletee details za ukweli, ukinidanganya tutagombana sana! akaingiza mkono mfukoni akatoa picha huyu hapa anaitwa ANITA!
Money Penny: nikachokaa! heee huyu demu nae kaokoka au? mbona mzuri sana?
Papaa: ndio nataka umfuatilie kama kweli kaokoka au la! kabla sijaoa binti nataka kujua sanaaa nimchunguze sana, wewe fanya upande wako na mie nafanya wangu.. akaingiza mkono mfukoni akatoa ATM card ya benki akanipa, tumia hii bank card password ni **** fanya urafiki na ANITA mpe anachotaka mfanye awe rafiki yako wa karibu akupe siri zako za zamani na mpaka sasa, tutakuwa tunawasiliana kwa namba hii akanipa business card imeandikwa Pastor Patric!
hapa usiwe unakuja plz plz maana nitaonekana vibaya si unajua walokole walivyo! na haya mavazi yako ya jeans na vimini huku usije nayo katafute mashuka uvae ukija huku!
kwaheri mimi naingia kwenye ibada... fanya kazi yangu kama nilivyokuagiza plz usiniangushe maana haukuwahi kuniangusha sikuwahi kufeli mitihani ila wa form 6 tu! plz nenda tutawasiliana
akainuka akaingia ndani mimi nikasimama kwenye ukuta wa majani ya nazi pembeni kuna dirisha namwangalia mwenyewe anaongoza ibada ananena kwa lugha! nilichoka Penny huyu muhuni kawa Mchungaji tena?! uuuuwi kichwa kiliniumaaa nikajikaza nikaondoka... nikiwa njiani nikapitia bank nijaribishe nione kama hii kadi ya kweli au feki
kuangalia Yeeeesu wangu na mariaaaa... akaunt ina milioni 80 cash, mpaka nikaogopa, hapo naangalia ilikuwa mwaka wa 95... mwaka wa 95 mtu anamiliki milion 80 niligandaaa! nikatamani nizipige zile hela nisepe akinifuata nitamwomba msamaha lakini nikakumbuka shule yangu iko ukingoni kuisha huenda akanisaidia kupata ajira sio kwa hela hizi
nikarudi nyumbani kichwa chamoto nikalala!
Jioni akaingia dogo mmoja dogo wangu sanaaa, namkubali sanaa dogo ana akili kinyama ila yeye hakufanikiwa kusoma aliingia kwenye biashara, dogo ana pesa zake ana biashara zake mtu mzuri sana,
tukaongea ongea palee nene, mambo kibao ananitania Penny ukimaliza tu shule nakuajiri kwenye kampuni zangu me namcheka wai huna hela ya kunilipa bwana acha kelele... tukaongea hapo weee akaniambia Penny tena nimekumbukaa, naomba unisaidie kitu kimoja
kuna demu nimemzimia nataka kumuwooowaa! nilikutana nae wakati na deposite hela bank, yeye alikuwa receptionist!
nikampenda ghafla mzuri sanaa!
nimemfukuzia sana lakini naona hatuelewani anasema sijui kaokoka sijui hataki kuchezewa dah ananichanganya sana....ngoja nitoe picha yake nikuonyeshe... akatoa picha akanionyeshaaa kuangalia tobaaa ndio yule yule ANITA nilipopewa na Pastor Papaaa! nikachoka ndani kwa ndani heee
yule dogo akaniambia huyu hapa Penny unahisi ataweza kunikubali? mimi sina mvuto ila nikizaa na huyu mrembo watoto watatoka vizuri sana sana... sasa unanisaidiaje? nimejaribu kila njia nimeona haiwezekani ananichomoleaaa,
Money Penny: nikajikaza nikamwuliza wewe Aloyce, huyu dada hana mtu kweli mbona mzuri sana?
Aloyce: hana bwana nimemfuatilia mpaka polisi nimemcheki ila kwao mambo safi flan hivi, babake maarufu flan hivi, huenda ndio inampa kiburi au sijui ndio huo ulokole, we nisaidie Da Penny nakuombaa! nakuachia namba yake ya simu, na anapofanya kazi adress anapoishi na majina ya marafiki zake! plz nyie wanawake mnajuana wenyewe mnavyoweza kutoana taarifa nisaidie kama ananifaa nimuwowe fasta nisije nikawahiwa!
Money Penny: nikachokaaa hii ya leo ni Mungu kanishukia au Malaika ananitafutia neema ... uuuuwi mbona sheedah
Kwani wewe Aloyce baada ya kuonana na huyu demu, ulitumia njia gani ya kumtongoza?! labda kuna sehemu unakosea nikusahihishe unajua urafiki na huyu demu bwana staki shida tayar nina shida za kunitosha,
Aloyce: akaanza kuniadithia jinsi show ilivyokuwa
TUONANE TAR 17 MARCH 2018 SAA 2 USIKU YA TZ KUJUA JINSI GANI ALOYCE ALIVYOMFUKUZIA ANITA
glass amo