Stori ya Maisha yangu

Vonso_Almeida

Member
Nov 7, 2016
15
28
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 35. Kwenye harakati za utafutaji nilijarbu vitu kadhaa wa kadhaa ili kufikia ndoto. Nilkua mcheza Dance nikaacha nikawa mchoraji nikaacha, nikawa mcheza soka huko sikupata nafasi.

Baada ya kumaliza elimu ya kidato cha 4 nikakosa nafasi ya kuendelea na elimu ya advance kwa maana nilikosa credit 1. Mzazi wangu wa kiume hakutoa support kuniwezesha kurisit. Nikaamua kuachana na Masuala ya elimu.

Brother wangu wa upande wa mama akanishauri nijiunge na Kampuni fulani ya ulinzi. Nikajiunga nikaanza kazi nikiwa na umri mdogo sana. Nikafanikiwa kuanza chuo cha Hotel Management kwa pesa niliokua naipata kupitia kazi ile ya ulinzi, Mama mzazi akachukua mkopo tukaunganisha nguvu nikaanza chuo nikawa naingia usiku lindoni na asubuh naingia chuo, nikafanya kwa miaka 3 mpaka namaliza chuo hapo kati kati baba mzazi hakuni support kwenye harakati za masomo ya chuo akawa ame base kwa mtoto wake ambae ni wa ndani ya ndoa.

Nikaacha na hiyo kazi. Nikamaliza chuo nikaanza kazi kwa takriban miaka 7 kwenye hotel. Balaa likaanza Covid ilipoingia nchini kazi ikaisha. Tukachukua mafao yetu maisha yakaenda. Baada ya Muda nikafanikiwa kupata kazi ya Internship kampun ya SWISSPORT AIPORT. Baada ya miezi kadhaa nikapewa mkataba wa mwaka. Hapa ndio kisanga kilipoanza.

Mwaka 2022 mke wangu akapata ujauzito. Maisha yakawa poa kabisa wakati nafanya kazi Airport. Ghafla nilipo sign mkataba nikadumu miezi 3 nikasimamishwa (Hapa kulikuwa na figisu figisu zilizonipelekea kufutwa kazi). Hii kampuni ya Swissport kwa haraka haraka ndio kampuni ambayo inaongoza kufuta staffs wake kazi we umefanya kosa au umekosea bahati mbaya, hawana neno bahati mbaya).

Nitaelezea kwa undani next Uzi. Nikasimamishwa miezi 2. Baada ya hapo nikafutwa kazi rasmi. Nikapiga benchi kwa miezi kama miezi 4. Nikaibukia Hotel moja maarufu sana mjini Dsm mpya ya waarabu. Pale kuna Uzi wake pia. Nikapiga kazi kuanzia mwez wa 8 mpka kufikia mwezi wa 11. Nikapata incident ambayo ikanifanya kukatishiwa mkataba wa mwaka mmoja. Hapa pia nilifanya kwa miez 3. Yapo mambo ambayo yalitokea kipindi hiki cha kufanya kazi kwenye hii Hotel.

Haikuwa rizki nikarud mtaani tena. Familia inasota kijana nina pambania kombe ili waishi vizuri. Nikaishia kupewa suport na watu baki kipindi ambacho sikuwa na kazi. Mwezi wa 11 2022, Kipindi nafutwa kazi ndio kipindi ambacho nilimpoteza Dada yangu wa damu kabisa. Nilichanganyikiwa.

Nikaitwa kwenye Interview Government chuo cha Open univerisity. Nikaunga unga mtoto wa Marehemu dada akanipa nauli ya Dodoma kupitia rambirambi za msiba wa Mama yake ambae ni Dada yangu, nikasafiri kuelekea Dodoma. Nikapokelewa na mshkaji ambae tulijuana mitandaoni. Nikafikia kwake nikapiga Interview nikageuka Dsm kuendelea kusaka michongo.

Nikaunga unga sana ili home wale. Mpaka mwaka 2022 ukaisha. ULikuwa mwaka tight sana..Mwaka 2023 ukaja na mavumba. Nikapata mchongo kwenye hotel fulani mjini. Mwezi wa 3 nikaanza kazi. Sikudumu pale ndio MUNGU AKATENDA MIUJIZA YAKE..NIKAPATA NAFAS YA KUWA MMOJA KATI YA WALIOCHAGULIWA KWENYE AJIRA ZA SERIKALI (REJEA ILE SAFARI YANGU YA DODOMA MWAKA 2022)..NIKAPANGIWA KWENYE TAASISI FULAN KUBWA NCHINI. SEHEMU AMBAPO ELIMU NDIO INAKUPELEKA, SEHEMU AMBAYO WENGI WANAITAMAN ILA NIKAPATA KWA KUPITIA ELIMU YANGU YA FORM FOUR.

NIkapangiwa Dodoma, Miujiza ikaendelea. Few days baada ya kukutana na Mkurugenzi mkuu akataka kujua profile yangu, alipogundua nimefanya kazi Airport na nimefanya hotel akasema natakiwa kurudi Dsm kusimamia kituo fulani.

Hakika mungu ametenda miujiza niko kazi sasa nimefikisha mwaka mmoja kazini. Subira ndio nguzo kwenye kila jambo gumu unalopitia. Kama una imani ndogo utasema umerogwa au mkono wa mtu ila nilisimama na imani yangu na wachache including mama yangu na mke wangu ambao waliamini sehemu zote nilizofukuzwa sikuwa nimefanya kosa la kudhamilia.

Ila tunajifunza kupitia changamoto. Nimejifunza mengi kwenye hiz hustling za maisha. Kwa uchache huu ndio uzi ambao nilitamani kuweke hapa uishi milele hata nisipokuwepo basi atakaepata nafasi kusoma ajue yapo mambo vijana tunapitia na imani ndio inatuvusha.

Keep pushing your time is coming.
 
Acha kulia lia mtoto wa kiume

Kwanza kabisa kaombe msamaha kwa baba yako sidhani hata wewe mtoto ulipewa muda ukasoma ukafeli amepoteza pesa za wewe kusoma fresh harafu arudie tena kukupa pesa ya kurist tena acha bobu

Usije mlaumu mtu yeyote awe ndugu au jamaa au rafiki ktk maisha yako . Mwambie Mungu, pambana kila mtu anamaswahiba yake anapambana, ukipambana Mungu hakosi kuleta mtu kwenye maisha yako kuwa msaada wako la sivyo kila mtu atakua mbaya kwako .

Hujaweka wazi ulifukuzwa kwa kosa lipi nabusipojua na kujirekebisha ukawa unajipa wewe uko sahihi hao ndiyo waliokosea utaumia sana

Akili yako itulie na kupambana na maisha

Pambana kijana pambana
 
Mswahili hata akiiba akafukuzwa utasikia "nilifanyiwa figisu"
I will hardly hire a worker who have been fired twice.
 
Acha kulia lia mtoto wa kiume

Kwanza kabisa kaombe msamaha kwa baba yako sidhani hata wewe mtoto ulipewa muda ukasoma ukafeli amepoteza pesa za wewe kusoma fresh harafu arudie tena kukupa pesa ya kurist tena acha bobu

Usije mlaumu mtu yeyote awe ndugu au jamaa au rafiki ktk maisha yako . Mwambie Mungu, pambana kila mtu anamaswahiba yake anapambana, ukipambana Mungu hakosi kuleta mtu kwenye maisha yako kuwa msaada wako la sivyo kila mtu atakua mbaya kwako .

Hujaweka wazi ulifukuzwa kwa kosa lipi nabusipojua na kujirekebisha ukawa unajipa wewe uko sahihi hao ndiyo waliokosea utaumia sana

Akili yako itulie na kupambana na maisha

Pambana kijana pambana
Kwenye huu Uzi yapo mengi ambayo niliyaruka ili niskuchosbe msomaji..Issue ya Elimu ilgubikwa na changamoto nyingi sana..Nafas ambayo nilkua nayo facilities za kuwezesha elimu sikupata kulinganisha na ndugu yangu..Hali ya kulelewa na Bimaza pekee ilkua inachangamoto nyingi..So nili feli kwa sababu lukuki na sio issues zingne..Pia kwa niliopitia nimejifunza kutokulaumu mtu sababu hii Dunia kila mtu ana challenges zake..Sina noma na mshua..Hata wakat nasafir kwenda Dom..Nilipata nafas ya kwenda kumuaga..japi hatuna story sababu hakuna love kati yetu..Hiki kitu hakilazimishwi kabsa...All in all mapambano yanaendelea..Kwa matukio mawili ya kufutwa kazi..nimepata somo kubwa sana hapa nilipo kwa sasa
 
Back
Top Bottom