KERO  Stendi ya Mbezi Magufuli hakuna maji siku ya pili leo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mawele

Senior Member
Jul 25, 2023
119
317
Stendi ya Mbezi Magufuli leo siku ya pili hakuna huduma ya maji, hali si hali kwani abiria wanapata tabu, na watu wanaofanya shughuli zao humu ndani na nje ya stendi kadhalika.

Hali imekuwa mbaya kiasi cha watu kuambiwa wajisaidie haja ndogo tu na si haja kubwa kutokana na kukosekana maji licha ya kutoa hela ya huduma ya vyoo lakini wahudumu wa vyoo wanalazimika kuzuia watu watu kwenda haja kubwa kwa kuwa hakuna maji.

Mamlaka ya maji wilaya ya Ubungo tunataka maji myalete Mbezi stendi haraka hali ni mbaya kunaweza tokea mlipuko wa magonjwa kutokana na idadi ya watu eneo hili kukosekana maji ni hatari sana.

1724911989220.jpeg

Pia soma:KERO - Waziri Aweso, DAWASCO Mbezi Mwisho hakuna maji wiki ya pili sasa tatizo nini? Kesho tunaandamana hadi kwa DC wa Ubungo
 
Kwakweli haya mambo yana fikirisha sana sijui na hii stendi tunataka tuibinafsishe eti tumeshindwa kuiendesha?! Hata lift hazifanyi kazi mpaka siku ya ziara ya viongozi, ukienda kule Nyuma mabasi yanaoshwa na kutenegezwa humo badala ya maegesho tu. Siku tukijitambua ya kuwa hizi ni mali za umma na ni kwaajili ya wanadamu wote tutakuta imesha haribika sana na kuikarabati itakuwa gharama kubwa sana.
 
Team Shabani bado ipo kazini kwakweli maji tabu mpaka Mpigi Magoe hata sijui kama wanamtafutia Waziri kiki
 
Na jambo jingine ni rushwa iliyokithiri na kukosa weledi kwa Manager wa hicho kituo.Huyo ndio amekua gonjwa kuu la hicho kituo.Mtu huyo amekua na vyanzo vyake binafsi vya kumuingizia kipato isivyo halali kwa njia ya rushwa.Mfano;Kuna aina ya biashara zilikatazwa ndani ya kituo hicho,lakini yeye amekua akiruhusu biashara Hizo kufanyika kwa mfanyabiasha kumpoza kidogo Manager ndipo aruhusiwe kuingia,amekua akigawa vizimba vya wafanyabiashara walisimamisha biashara zao,ili upate kizimba lazima umpe Tsh 500,000 ndipo akupatie,na amekua akishirikiana na Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa hapo stand kutimiza uovu huo.
Leo hii Ile hadhi ya kuitwa kituo cha kimataifa haipo tena.
Tukamuomba Mh Waziri mwenye dhamana, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo walitupie macho hili
 
Watu humo wanajiidiaje aise

Ova
Huyo meneja ni muongo

TAARIFA KWA UMMA

29.8.2024

UPUNGUFU WA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WA MIKOA YA DAR ES SALAAM NA PWANI

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia Wateja na wananchi wa Mikoa ya Dar es salaam na Pwani kuwa kumekuwa na upungufu wa huduma ya maji kutokana na hitilafu ya umeme katika mfumo wa kupokea umeme kwenye mtambo wa Uzalishaji Maji wa Ruvu Juu.

Maeneo yanayoathirika ni maeneo yote Mlandizi, Msufini, Vigwaza, Chamakweza, Ruvu, Kwa Mathias, Pangani Bokomnemela, Kibaha, Visiga, Picha ya Ndege, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Makabe, Kimara, Msewe, Changanyikeni, Mabibo, Kisarawe, Ukonga, Kinyerezi, Tabata, Temeke, Segerea, Makuburi, Ubungo Maziwa, Mwananchi, Kiwalani, Lumo, Yombo Vituka, Uwanja wa Ndege, Banana, Viwanda vya Barabara ya Nyerere, Jet, Buguruni, TAZARA

Wataalam wa DAWASA na TANESCO wanashirikiana ili kurudisha huduma katika hali ya kawaida.

Tunawaomba wananchi wawe wavumilivu wakati Wataalam wanaendelea na jitihadi za kurudisha huduma!

Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja
0800110064 (bure) au
0735 202-121 (WhatsApp tu)

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano
 
Na wajinga hao
Stendi ya Mbezi Magufuli leo siku ya pili hakuna huduma ya maji, hali si hali kwani abiria wanapata tabu, na watu wanaofanya shughuli zao humu ndani na nje ya stendi kadhalika.

Hali imekuwa mbaya kiasi cha watu kuambiwa wajisaidie haja ndogo tu na si haja kubwa kutokana na kukosekana maji licha ya kutoa hela ya huduma ya vyoo lakini wahudumu wa vyoo wanalazimika kuzuia watu watu kwenda haja kubwa kwa kuwa hakuna maji.

Mamlaka ya maji wilaya ya Ubungo tunataka maji myalete Mbezi stendi haraka hali ni mbaya kunaweza tokea mlipuko wa magonjwa kutokana na idadi ya watu eneo hili kukosekana maji ni hatari sana.

View attachment 3081854

Pia soma:KERO - Waziri Aweso, DAWASCO Mbezi Mwisho hakuna maji wiki ya pili sasa tatizo nini? Kesho tunaandamana hadi kwa DC wa Ubungo
Na wajinga hapo utakuta kutwa nzima ni Mada za yanga na Simba
 
Kwakweli haya mambo yana fikirisha sana sijui na hii stendi tunataka tuibinafsishe eti tumeshindwa kuiendesha?! Hata lift hazifanyi kazi mpaka siku ya ziara ya viongozi, ukienda kule Nyuma mabasi yanaoshwa na kutenegezwa humo badala ya maegesho tu. Siku tukijitambua ya kuwa hizi ni mali za umma na ni kwaajili ya wanadamu wote tutakuta imesha haribika sana na kuikarabati itakuwa gharama kubwa sana.
Hizo ni akili za CCM zikiwa sapoted na asilimua 98 ya wajinga wa hili Taifa
 
  • Thanks
Reactions: BBJ
Bora hapo maji yamekata siku Moja tu.huku misumi,msakuzi,makabe na mpigi maji hayapo kabisa.yaani hakuna bomba la dawasa hata moja.watu wa kule kipindupindu wamekizoea.
 
Stendi ya Mbezi Magufuli leo siku ya pili hakuna huduma ya maji, hali si hali kwani abiria wanapata tabu, na watu wanaofanya shughuli zao humu ndani na nje ya stendi kadhalika.

Hali imekuwa mbaya kiasi cha watu kuambiwa wajisaidie haja ndogo tu na si haja kubwa kutokana na kukosekana maji licha ya kutoa hela ya huduma ya vyoo lakini wahudumu wa vyoo wanalazimika kuzuia watu watu kwenda haja kubwa kwa kuwa hakuna maji.

Mamlaka ya maji wilaya ya Ubungo tunataka maji myalete Mbezi stendi haraka hali ni mbaya kunaweza tokea mlipuko wa magonjwa kutokana na idadi ya watu eneo hili kukosekana maji ni hatari sana.

View attachment 3081854

Pia soma:KERO - Waziri Aweso, DAWASCO Mbezi Mwisho hakuna maji wiki ya pili sasa tatizo nini? Kesho tunaandamana hadi kwa DC wa Ubungo
Boss SGR now

Njoo tusome

Short course

Tracking and Developing Fraud and Corruption Indicators

Venue: Mombasa - Kenya

US$ 1600 + Ticket $399

Chuo

The Eastern and Southern African Management Institute, ESAMI

View: https://youtube.com/shorts/cfduceGYgRI?si=UCMC2MbBSVcmlIQx
 
Back
Top Bottom