KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 18,894
- 36,211
Kituo cha Daladala Simu 2000 kimefungwa leo, Septemba 14, 2024, kupisha ujenzi wa karakana ya mabasi yaendayo haraka maarufu kama mwendokasi.
Karakana hiyo ni sehemu ya mradi wa awamu ya nne wa mabasi haya. Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, kupitia Mkuu wa Idara ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji, Mary Mwakyosi, umeeleza kuwa karakana hii itasaidia kuboresha huduma za usafiri na usimamizi wa mabasi hayo.
Mnamo Julai 8, 2024, wafanyabiashara katika stendi hiyo walipinga mpango wa kubadilisha eneo lao la soko kuwa karakana, wakihofia athari kwa biashara zao. Hata hivyo, Julai 13, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, alifanya mkutano na wafanyabiashara hao na kuwaeleza manufaa ya mradi. Aliahidi kuwa watatengenezewa mazingira mazuri ya kuendelea na biashara zao wakati wa ujenzi wa mradi huo.
Awamu ya nne ya mradi wa mwendokasi itahusisha mabasi yatakayotoka Tegeta, Mwenge hadi Ubungo kupitia Barabara ya Sam Nujoma. Karakana hiyo inatarajiwa kukamilika ujenzi wake ifikapo Machi, 2025.