Starlink inasimikwa lini Tanzania? Tuungane kwa pamoja

BICHWA KOMWE -

JF-Expert Member
Jul 21, 2022
6,373
16,071
Wasalaam!

Natoa rai, na niwakumbushe, tunahitaji huduma ya starlink kuliko kitu chochote Tanzania.

Kwa sisi tunaoishi vijijini tutakuwa tumeponywa na ujio wa huu mtandao ukizingatia kwamba makampuni ya simu yameshindwa kufikisha huduma katika maeneo ya mbali.

Nchi karibu zote Afrika tayari wameshasimika mtandao wa starlink tumebaki sisi tu kwa visingizio sijui vya leseni na mambo mengine yasiyo na tija yoyote.

Mtandao ni uchumi, mtandao ni maendeleo! Dunia ya sasa inataka mtandao kwa kila shughuli kwanini mnatuchelewesha? Hizi sio zama za ujima za kujivuta vuta kwa uvivu na visingizio uchwara, tunataka kwenda kwa kasi.

Kuna watu wamekaa tu ofisini wanazungusha viti kwa madoidoi na kufuga vitambi hawajali kuhusu mustakabali wa nchi na watu, wanapokea tu maburungutu na kutoa hewa chafu bila kuwajibika.

Natoa agizo, wanaowajibika na sekta ya mawasiliano watuwekee huo mtandao wa Starlink mara moja, tumechoshwa na blah blah.

Asante.
 
Back
Top Bottom