ngongoti2000
JF-Expert Member
- Nov 20, 2017
- 2,235
- 2,139
Kama muumini wa kanisa katoliki pale St Peters Oysterbay na Mwananyamala kuna mapungufu ambayo(at least machache ninayoyaonaga) ningependa wahusika wayaangazie macho na wayarekebishe ikiwezekana(siyo lazima);
1. Kutokupangwa kwa viti vya ziada pale nje kabla ya Misa:-kwa kawaida karibu jumapili zote waumini huwa hawatoshi ndani ya kanisa(limeshakuwa dogo) hivyo hulazimika kukaa nje.Hali inakuwa mbaya zaidi siku za misa kubwa kama za sikukuu e.g ijumaa kuu,xmas,pasaka nk...lakini pamoja na kuwa viti vipo vya kutosha kule madarasani karibu na ukumbi wa Rugambwa, hakuna juhudi zinazozofanyikaga kuvipanga viti maeneo ambayo watakaa watu waliochelewa kabla ya misa haijaanza.Nasema hivi kwa sababu huwa kuna usumbufu mkubwa wakati misa inaendelea kuona watu wakipishana na kuburuza viti kule nje.Halafu kibaya zaidi kuna watu wengine huwa hawajui kama kuna zoezi hilo la kufuata viti hivyo wanabaki wamesimama ,hakuna mtu anayeshughulika na watu walio nje ya kanisa.Kwa mfano juzi kwenye misa ya Kipaimara na Komunyo ni misa kubwa (nilikuwa sijahudhuria siku nyingi) nilishangaa bado mchezo ni ule ule...nimefika hakuna viti kabisa nje....watu wakaanza kujaa zikaanza pilika pilika za kwenda kubeba viti ,si wazee , si vijana si watoto wote tunakimbizana na viti kama tupo shule ya msingi.....huku askofu Ruwaichi anaendelea na misa...kuna wengine tena watu wazima wallikuwa hawana habari kama kuna viti vya ziada kule madarasani hivyo wakawa wamekaa kwenye majani,mawe,vizingiti,chini nk hakuna maelekezo yeyote....sasa nikawa najiuliza , ninavyojua kila jumapili huwa kuna wasimamizi wa huduma kanisani....hili suakla la kupanga viti vya kutosha kule nje lina vikwazo gani???labda wadau mnieleweshe kama kuna masharti au ni nini?Mbona kanisa la Mwananyamala huwa tunakuta viti vya kutosha kule nje na huwa wanabadilisha idadi ya viti kulingana na ukubwa wa misa?? sijawahi kuona mtu akikosa kiti labda kama vyoote vimekwishachukuliwa na vinatumika lakini huwa vyote vinapangwa kule nje.
2.Maji ya baraka - haya huwa yanapatikana ndani tu ya kanisa. sasa kama kuna watu wengi nje manake misa ikiisha kama ukitaka uchovye maji ya baraka ambayo yapo ndani mnakutana na watu wa ndani wanatoka nje...sasa pale kuna kuwa na chaos/misuguano ambayo sioni kama ni ya lazima..waumini wengine huamua kutochovya maji ya baraka kabisa sababu ya ule msuguano wa jinsi ya kupishana .Ukilinganisha na Mwananyamala, maji ya baraka yanapatikana pia kwa watu wa nje(au siyo sahihi?)...yaani huhitaji kuingia ndani ili upate maji ya baraka.Sasa pia hapa najiuliza kama hili nalo ni kuna masharti au nini kikwazo???
Ofcourse nilishaongeaga na mzee wa kanisa mmoja pale st Peters lakini naoana labda alipitiwa au halikuwa na uzito kwake.
Nawasilisha wadau kwa ajili ya maoni, kunielimisha nk