SSP Solomon: Ukilewa na kushindwa kufika nyumbani, Polisi tutakulinda na kukufikisha salama

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,447
3,760
Wakuu

Ukilewa na huna usafiri waombe jeshi la polisi wakupeleke home chap 😂

==

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kinondoni (RTO), SSP Solomon Mwangamilo, amewashauri wananchi wanaojikuta wamelewa kupita kiasi na hawana usafiri wa kuwaomba msaada Jeshi la Polisi wakiwa katika hali hiyo.

"Kama ukalewa uko chakali, na ukapepesuka, ukashindwa kufika nyumbani ukiwa unatembea kwa miguu sisi kama jeshi la polisi kazi yetu ni kulinda raia na mali zao, tutakuchukua, kama unaweza kujieleza utatuambia unakaa mtaa fulani tutakufikisha kwasababu wewe sio mhalifu"
 
Yani nikilewa naweza muamini kibaka mkabaji kunisindikiza nyumbani na sio polisi.

Kibaka ataishia kuniibia nilichonacho lakini ataniacha na uhai wangu.

Ila majambazi polisi, wataniibia, watanipiga na kuniua kabisa huku wakinipa na kesi ujambazi.

Bora kufa kuliko kuamini POLISI wa Tanzania, ukijipeleka kwao ni bonge la fursa umewapelekea.
 
Wakuu

Ukilewa na huna usafiri waombe jeshi la polisi wakupeleke home chap 😂

==

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kinondoni (RTO), SSP Solomon Mwangamilo, amewashauri wananchi wanaojikuta wamelewa kupita kiasi na hawana usafiri wa kuwaomba msaada Jeshi la Polisi wakiwa katika hali hiyo.

"Kama ukalewa uko chakali, na ukapepesuka, ukashindwa kufika nyumbani ukiwa unatembea kwa miguu sisi kama jeshi la polisi kazi yetu ni kulinda raia na mali zao, tutakuchukua, kama unaweza kujieleza utatuambia unakaa mtaa fulani tutakufikisha kwasababu wewe sio mhalifu"
View attachment 3180111
Sijui kama utafika na wallet yako.
 
Nakumbuka Arusha maeneo ya Shivas kule nimetoka pale Picnic mbili tatu zipo kichwani naelekea rift valley nilipofikia, namaliza barabara ya kwanza nikakutana na jamaa wakaniuliza unaenda wapi usiku huu ,ilikuwa kama saa saba hivi siku hiyo kulikuwa na ngumi kwenye luninga...nikawaambia naenda kulala,wakaniuliza saa hizi ukivamiwa,nikawauliza na nani mbona Watu bado wapo kibao tu..mbona wao wasivamiwe..au hao ni mbu sio Watu?nilikuwa nafanya kama mzaha nikijua wananizengua tu..mmoja akaniambia unaleta utani sio..akatoa pingu,mwingine akasema twende ukalale ndani..na upande mwingine kule naiona difenda..ndio nikaona ohoo hapa kimenuka..nikaona isiwe tabu nikazama nikatoa kaki nikawaambia Wazee niacheni nikalale kesho nina safiri asubuhi...wakaniachia kwa mkwala haya fanya chap tunakulinda hapa mpaka uingie getini..ikabidi tu niondoke huku nawatukana kimoyomoyo kupoza machungu ya kaki yangu..yaani kuna Watu kibao muziki bado unadunda pale Picnic,Bodaboda kibao,Madada poa kibao na Watu wengine lakini wakanichagua mimi tu.Nikafika rift valley nikamuelezea yule muhudumu akaniambia ni kweli wangeweza kunipeleka kituoni hao Wajinga.
 
Kutokana na pilika pilika nyingi za kusherehekea Christmas na mwaka mpya polisi wameamua kutoa msaada kwa ye yote atakayezidiwa na furaha. Wananchi wote mnashauriwa kutumia fursa hii adimu!
Screenshot_20241219-123813.jpg
 
Back
Top Bottom