The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 746
- 2,093
Spika wa Bunge la Kaunti ya Nairobi, nchini Kenya, Ken Ngondi, alionekana kwenye video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, kumlazimisha mwanamke wa kiislamu kumpa mkono na kumkumbatia, katika hafla ya siku yake ya kuzaliwa.
Tukio hilo limezua taharuki kutoka kwa wananchi wakitaka spika afunguliwe mashtaka kwa unyanyasaji wa kijinsia. Zaidi ya hayo, Chama cha Wanasheria wa Kiislamu kimetoa wito kwa Kurugenzi ya Uchunguzi wa Jinai kuanza mashtaka ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya spika wa Kaunti ya Nairobi.
Tukio hilo pia limezuwa gumzo kwenye bunge la Kenya, huku mbunge mmoja akitoa wito wa kujiuzulu kwa spika.
Ingawa Spika huyo alisema video hio imepitwa na wakati, tukio hilo lilitokea Novemba mwaka 2022 na haikuwa na nia ya kumdhalilisha mtu yeyote.
Msaidizi wa Spika Ngondi, Hafsa Hussein alisema Mh. Fatuma alitoa wasiwasi wake kuhusu suala hilo papo hapo, na spika akaomba radhi.
Video hio iliyozua hisia imesambazwa na mwana blogu Cyprian Nyakundi katika mitandao ya kijamii.
Spika Ngondi akittolea ufafanuzi jambo hilo 👇