Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,147
- 21,165
Wala haihitaji akili kubwa sana kuona kwamba Spika wa Bunge Tulia na jopo zima la uongozi wa serikali wametambua kwamba Mpina amewaumbua kwa kuweka wazi uongo wanaoufanya kuwahadaa Watanzania. Na sasa wanataka kubadilisha uzito wa tuhuma za uongo wa Waziri Bashe na kuelekeza fikra kwa ukiukwaji wa utaratibu wa Mpina.
Tuseme ukweli, mbele ya macho ya Watanzania, nani mwenye kosa kubwa na baya zaidi kati ya Bashe na Mpina? Na kama Tulia anaona Mpina haheshimu u-Spika wako wa Bunge la Tanzania dunia, anaona Bashe anauheshimu zaidi ya Mpina kwa kusema uongo huku akimwangalia bila hata kupepesa macho?
Kosa la Mpina, kama ni kosa, ni kuanika uongo wa Bashe hadharani. Kosa la Bashe ni kuwadanganya Watanzania katika jambo ambalo lina kila dalili za ufisadi na uvunjaji sheria. Sasa kwa nini Tulia kama Spika anaweka nguvu nyingi dhidi ya Mpina kuliko mtuhumiwa wa uongo Bashe? Kosa la Mpina ni kosa dhidi yako kama Spika wa Bunge, na kosa na Bashe ni kosa dhidi ya Watanzania wote. Sasa nani mhalifu zaidi kati ya hawa wawili? Nani anapaswa kwenda kamati ya Bunge ya maadili kwa haraka iwezekanavyo?
Pendekezo langu kama Mtanzania alieyedanganywa ama mtoto na waziri Bashe, ni kwamba hili la Mpina kukiuka taratibu za Bunge tuliweke pembeni kwanza. Tumalize lile lililotangulia na lililo jambo kuu hapa - uongo wa Bashe kwa Bunge na kwa Watanzania. Tukimaliza kushughulika na Bashe, basi ndio tuje turudi kwa Mpina - kama kweli alichofanya ni kosa kubwa kiasi ambacho Spika Tulia anataka kutuambia. Bunge ni la wananchi, sio la Spika na Raisi, kwa hiyo sisi kama wananchi tuna haki ya kupata ufafanuzi wa Mpina dhidi ya uongo wa Bashe kwa Bunge letu.
Sisi kama Watanzania, tuko tayari kuvumilia na kusamehe Tulia anachoona ni kosa la Mpina kuliko kosa la Bashe.
Halafu jambo jingine kwa Tulia - heshima hailazimishwi, inakuja yenyewe tu kutokana na matendo na personality yako. Unaweza kuwa Spika wa Bunge la Tanzania na dunia au hata ulimwengu, sasa kuheshimiwa na watu si jambo la kulazimisha. Hii philosophy ya "unanijua mimi ni nani" ni ya kitoto sana, na inatumiwa na watu ambao hawajaelimika hata kama ni maprofessor, watu wasiojiamini au watu waliotoka katika maisha duni na kufikia kuwa maarufu.