Spika Tulia ni kweli unatoa mikopo online kupitia Foundation yako au watu wanatumia jina lako kutapeli watanzania?

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
48,808
150,430
Kila nikiingia Facebook, nakutana na tangazo la Tulia Trust Foundation Mikopo online ambapo tangazo hili linatangaza kuwa Foundation hiyo ya Tulia inatoa mikono online.

Sina interest ya kujaribu kuomba mikopo wowote, ila concern yangu ni ukweli wa kilichoandikwa kwani utapeli kwa kutumia majina ya watu maarufu upo sana na haujaanza leo

Swali langu ni kwanini Spika Tulia asitoe ufafanuzi wa hili jambo?

Ni kweli Foundation yake inajihusisha na mikopo ya online?

Waandishi wa habari mtafuteni Tulia mumuhojo juu ya hili.

Wengine wanaotumika kutangaza mikopo ya online ni Mohamed Dewji(MO) ambae nae anadaiwa kuwa na Foundation ya aina hiyo na mwingine ni Maulid Kitenge anaetumika kutangaza App moja ya mikopo ya online na sijawahi kuwasikia wakikanusha au kukubali.

Swali ni kwanini wako kimya?

Screenshot_20240708_203950_Facebook.jpg
Screenshot_20240708_203824_Facebook.jpg
 
Sio Tuiia tuu kuna inayotumia jina la Joketi wa Uvccm na Mo Dewji na TCRA wamelala tuu.
Unajua serikali inapata tozo kwenye hizi transactions za mikopo ya online na huenda ndio maana serikali haichukui hatua zozote.

Hizi za kina Tulia Jokate na MO, watu wanaambiwa waweke hela (akiba) kwanza ndio wapewe mkopo. Je huu si utapeli?

Wahisika wanakaa kimya kwasbabu wanafaidika na hii biashara?

Mtu kama MO, kweli ana shida na hela za aina hii?

Maswali ni mengi sana.

Mpira tunaomba uchunguze na hili jambo na ukirudi tu Bungeni unalinzisha upya mpaka wakome.
 
Matapeli hao Mkuu Salary Slip, Tulia Trust na Kamanda wa Polisi waliwahi kutoa ufafanuzi wa hili

1720471062588.png

Tafadhari epuka udanganyifu!

Account hii Imetumika Kutapeli Watu Pesa Kwenye Mtandao wa Facebook Ikitumia Jina la Tulia Trust Mikopo na Wamejifanya Wao ni Taasisi ya Tulia Trust na Kua Wanajishughulisha na Utoaji wa Mikopo.

Taasisi ya Tulia Trust Haihusiki na Swala la Mikopo Kwa Njia ya Mitandao.

Kupata Huduma Zetu Fika Ofisi za Tulia Trust Zilizopo Tukuyu Mjini, Uyole Makasini, au Kyela Mjini.

Kwamaelezo Zaidi Piga Simu Namba 0767-860-515.

Matapeli hao Mkuu Salary Slip, Tulia Trust na Kamanda wa Polisi waliwahi kutoa ufafanuzi wa hili

View attachment 3036987

Tafadhari epuka udanganyifu!

Account hii Imetumika Kutapeli Watu Pesa Kwenye Mtandao wa Facebook Ikitumia Jina la Tulia Trust Mikopo na Wamejifanya Wao ni Taasisi ya Tulia Trust na Kua Wanajishughulisha na Utoaji wa Mikopo.

Taasisi ya Tulia Trust Haihusiki na Swala la Mikopo Kwa Njia ya Mitandao.

Kupata Huduma Zetu Fika Ofisi za Tulia Trust Zilizopo Tukuyu Mjini, Uyole Makasini, au Kyela Mjini.

Kwamaelezo Zaidi Piga Simu Namba 0767-860-515.

View attachment 3036988
Asante kwa taarifa hii. Ukweli ni kwamba bado wanaendelea mpaka sasa. Hata App zingine za kutoa mikono online nazo bado zinajitangaza Facebook kama vile hii nchi haina serikali.

Cha kushangaza, hizi App zal mitandaoni zinatumia mitandao ya simu kufanya miamala yao ya kutoa mikopo na kupokea marejesho ila tunaambiwa hawa watu ni matapeli na hawana vibali.

Hiii nchi kwa sasa ni kama hamna serikali.
 
Kila nikiingia Facebook, nakutana na tangazo la Tulia Trust Foundation Mikopo online ambapo tangazo hili linatangaza kuwa Foundation hiyo ya Tulia inatoa mikono online.

Sina interest ya kujaribu kuomba mikopo wowote, ila concern yangu ni ukweli wa kilichoandikwa kwani utapeli kwa kutumia majina ya watu maarufu upo sana na haujaanza leo

Swali langu ni kwanini Spika Tulia asitoe ufafanuzi wa hili jambo?

Ni kweli Foundation yake inajihusisha na mikopo ya online?

Waandishi wa habari mtafuteni Tulia mumuhojo juu ya hili.

Wengine wanaotumika kutangaza mikopo ya online ni Mohamed Dewji(MO) ambae nae anadaiwa kuwa na Foundation ya aina hiyo na mwingine ni Maulid Kitenge anaetumika kutangaza App moja ya mikopo ya online na sijawahi kuwasikia wakikanusha au kukubali.

Swali ni kwanini wako kimya?

View attachment 3036891View attachment 3036892
VIGEZO MUHIMU ILI KUPATIWA MKOPO NDANI YA DAKIKA 15 TU

DK. TULIA TRUST FOUNDATION
S L P 941,
Ofisi zetu zipo njia panda ya chamwino dodoma
Info.tulia@gmail.tz.com

1.MUOMBAJI WA MKOPO UNATIKIWA KUWA NI MTANZANIA HALALI

2.MUOMBAJI WA MKOPO UNATIKIWA KUWA NA KITAMBULISHO CHOCHOTE KINACHO TAMBULIKA KISHERIA AU NAMBA YA NIDA

3.MUOMBAJI WA MKOPO UNATIKIWA KUWA NA SABABU YA MAULUMU YA KUOMBA MKOPO

4.MUOMBAJI WA MKOPO NI LAZIMA UWE NA UMRI KUANZIA MIAKA 18 NA KUENDELEA

5.MUOMBAJI WA MKOPO UNATIKIWA KUWA NA KIPATO ANGALAU LAKI MOJA KWA MWEZI ILI UKIPATA MKOPO ILI RAHISI KUFANYA MAREJESHO

6.HATUCHUKUI DHAMANA YA KITU CHOCHOTE ZAIDI YA KITAMBULISHO CHAKO AU NAMBA YA NIDA

7.MUOMBAJI WA MKOPO UWE NA SHUGHULI YA KUFANYA KWA AJILI YA KUJIINGIZIA KIPATO CHA KILA SIKU

KAMA UNA VIGEZO IVO OMBA UTARATIBU WA KUTUMA TAARIFA ZAKO ZA MUHIMU ILI TUZIHAKIKI ILI UPATIWE TARATIBU ZA KUFUATA KABLA HUJAPEWA MKOPO WAKO
 
Back
Top Bottom