Spika Tulia Ackson asitisha Shughuli za Bunge kwa Dharura, awataka wabunge kutoka nje kwa haraka

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,814
13,580
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 56, leo Juni 27, 2023.



===​

UPDATE;
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Tulia Ackson amesitisha shughuli za Bunge asubuhi hii wakati Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi na uchukuzi Mhandisi Godfrey M. Kasekenya akijibu maswali ya wabunge.

Dharura hii imekuja baada ya alarm za Bunge kutoa sauti za kuashiria Wabunge watoke nje kwa haraka.

"Mhe. Naibu Waziri, Waheshimiwa Wabunge nadhani hiyo inaashiria tutoke humu ndani kwa haraka. Kila mtu atafute mlango ulipo karibu naye atoke. Sote twende ile sehemu ya kukusanyikia watu. Naahirisha Shughuli za Bunge mpaka jambo hili litakaporekebishwa." amesema Dr. Tulia.

Wabunge wengi wameonekana wakitoka nje ya Bunge hilo kama walivyoelekezwa.

Bunge limerejea
Bunge limerejea tena saa 10:16 asubuhi baada ya kusimama kutokana na uwepo wa dharura. Kwa mujibu wa Spika wa Bunge Dr. Tulia Ackson, taarifa ya nini hasa kilitokea itatolewa pindi wabunge wote watakaporejea ndani kuendelea na kikao hicho.

Spika Tulia amesema ukumbi wa Bunge pamoja na majengo yote kwa maana ya jengo la utawala, jengo la utawala annex na jengo la bunge (Kwa maana ya ukumbi wa Bunge) kuna vifaa maalum vya kutambua uwepo wa moshi au jambo lingine linaloweza kuleta athari kwenye majengo.

Chanzo cha alarm hizo ilikuwa ni uwepo wa marekebisho yanayofanyika chini ya ukumbi wa Bunge ambapo chumba kimojawapo kilikuwa na hitilafu katika utinduaji wa eneo jambo lililofanya vifaa maalum kunasa vumbi na kusababisha alarm ipige kelele.

Spika Tulia amewahakikishia wabunge kuwa jambo hilo limerekebishwa na amewapongeza wote kwa kuchukua hatua stahiki za kutoka nje kwenye milango iliyo karibu na viti vyao.
 
Spika wa bunge ameahirisha kwa muda shuguli za Bunge baada ya "alarm" ya hatari kulia.

Hivi sasa magari ya Zimamoto yamewasili
 
Yoooooo bwakya bwakya bwakya bwakyaaabyooooooo yooooooo yoooo bwakya bwakya bwakya
 
Back
Top Bottom