Spika Ndugai, una nini na Mbunge Halima Mdee wa CHADEMA?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Kwa uzoefu wangu wa kisiasa ndani ya CCM na Serikalini, nimetafakari sakata la Spika wa Bunge Job Ndugai na kuliona katika mtazamo mwingine na tofauti kabisa. Mtazamo mpya. Mtazamo ambao wengi hawakuuona. Sakata lote la CAG kuitwa Bungeni kwa mahojiano kwa kulidhalilisha Bunge limesababishwa na Mbunge Halima Mdee wa CHADEMA.

CAG alipoitoa kauli yake juu ya utekelezaji wa Ripoti za CAG Bungeni, Spika hakujitokeza kumuita. Wananchi mbalimbali, hasa mitandaoni, walipomuunga mkono au kumpinga CAG kuhusu kauli yake kulihusu Bunge, Spika hakujitokeza. Alipochangia Mbunge Halima Mdee, ikawa nongwa. Spika akajitokeza na kuwaita: mmoja Jumatatu na mwingine Jumanne ijayo. Wakajieleze.

Spika akazuga kumuandama na kumtisha CAG. Watu wakajaa kingi. Lengo si CAG,lengo ni Mbunge Halima Mdee. Lengo ni kumshughulikia ipasavyo Mbunge Halima Mdee na yeyote awaye wa upinzani katika kutimiza 'ahadi' ya pale Ikulu. Lengo ni kumuadhibu Mbunge Halima Mdee kila mara na kwa mambo ambayo wengine husamehewa au kukaliwa kimya.

Mbunge Halima Mdee aliwahi kusimamishwa kuhudhuria vikao vilivyosalia vya bajeti mwaka 2017(?) huku Mbunge Freeman Mbowe akisamehewa. Wote waliomba msamaha Bungeni. Akaadhibiwa Mbunge Halima Mdee. Amini nawaambia, hata pingu zitamhusu Mbunge Halima Mdee wa Kawe kwa tiketi ya CHADEMA kama hatakwenda Bungeni Jumanne ijayo. Ole wake!

Ndiyo maana nauliza Spika Ndugai ana nini hasa na Mbunge Halima Mdee hadi 'kutamani' kumshughulikia kila mara? Afanyaje ili mambo yake yatulie?

Uhakiki wa mashamba ya korosho umetufunga kamba huku wengine wakitamba!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Mtwara)
 
Aache kujifanya anajua sana, Pia awe na nidhamu. Sio kufanya bunge kama uwanja wa mipasho. Hayo mambo ya mipasho zilipendwa.
 
Back
Top Bottom