Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,828
- 13,585
Katika mazungumzo yao, Dkt. Tulia amewasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuishukuru na kuipongeza Serikali ya India kwa kuendeleza ushirikiano wa kiuchumi na kijamii baina ya nchi hizo mbili.
Dkt. Tulia amebainisha kuwa ziara ya Rais Dkt. Samia aliyoifanya nchini humo mwaka jana imeongeza chachu ya kukuza uhusiano kwa kuleta manufaa katika sekta za afya, elimu, ulinzi na maji.
Mara baada ya mazungumzo hayo, Dkt. Tulia pia amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Bunge (Upper House) ambaye pia ni Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Mhe. Jagdeep Dhankhar ambapo pamoja na mambo mengine amelipongeza Bunge hilo kwa kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za IPU, kutunga Sheria ya kuongeza idadi ya uwakilishi wa Wabunge wanawake Bungeni kwa kufikia asilimia 33 pamoja na kupitisha Bajeti yenye kulenga kuinua uchumi na kipato cha vijana, wanawake na makundi maalum.