Snowden E
JF-Expert Member
- Apr 27, 2018
- 1,586
- 2,694
Alhamisi Novemba 21, 2024: Kamati ya Uchunguzi kuporomoka kwa jengo Kariakoo yazinduliwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezindua Kamati ya Wataalamu ya Uchunguzi wa Jengo lililoporomoka katika eneo la Kariakoo ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia ya kuchunguza chanzo cha tukio hilo pamoja na kufahamu ubora na uimara wa majengo yote yaliyoko Kariakoo.
Novemba 16, 2024, majira ya saa 3 asubuhi, ilitokea ajali ya kuporomoka kwa jengo la takribani ghorofa tatu lililopo Mtaa wa Agrey, Kata ya Kariakoo Jijini Dar es Salaam na kusababisha athari kubwa kwa watu na mali katika eneo hilo.
Jumatano Novemba 20, 2024: Rais Samia atembelea eneo la ajali ya ghorofa Kariakoo, asema vifo vimefikia Watu 20
Rais Samia Suluhu Hassan amewasili hivi punde Kariakoo, Dar es Salaam, ambapo jengo la Gorofa liliporomoka Jumamosi na kusababisha vifo vya watu na wengine kujeruhiwa.
Alipofika eneo la tukio, Mkuu wa Nchi alikagua jengo lililoporomoka kabla ya kuhutubia wananchi.
Rais Samia Suluhu Hassan aliyekuwa nchini Brazil kwenye Mkutano wa G20 ametua jijini Dar es Salaam leo na moja kwa moja kuelekea eneo lilipoporomoka jengo Kariakoo. Amesema taarifa aliyopewa, Watu 20 wamepoteza maisha kwenye jengo hilo
Jumatatu Novemba 18, 2024, Saa 3 Alasiri: Shimo mpja lina watu 9, tunawasiliana nao
Kamishna wa Zimamoto John nchini CGF John Masunga amemweleza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwamba **** shimo moja lina watu 9 na wanawasiliana nao na wamefanikiwa kuwaingizia mipira ili kusakuleti Oxygen.
Jumapili Novemba 17, 2024, Saa 8 Mchana: Idadi ya manusura waliotolewa kwenye Vifusi yafikia 77
Idadi ya Watu waliokuwa wamefukiwa na vifusi vya jengo lilioanguka Kariakoo, imefikia 77 baada ya watu wengine 7 waliokuwa kwenye 'basement' kuokolewa leo, huku operesheni ya uokoaji bado ikiendelea
Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila, amethibitisha uokoaji huo akisema “Hawa watu 7 waliokolewa leo walikuwa kwenye basement, na familia zao zimethibitisha walikuwa na mawasiliano nao, jambo linalodhihirisha mafanikio ya operesheni inayoendelea,”
Mapema leo, Novemba 17, 2024, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, John Masunga, alisema changamoto kubwa wanayokutana nayo katika Uokoaji ni muundo wa jengo kuwa na kuta nyingi, zinazowalazimu kuzivunja ili kuwafikia manusura
Jumapili Novemba 17, 2024, Saa 5 Asubuhi: Zimamoto: Walioko chini ni Wazima, tutahakikisha wanatoka Salama
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, John Masunga, amesema bado kuna watu wako chini na mawasiliano yanafanyika na watu hao ni wazima na wanaendelea kuwapatia huduma.
“Shughuli ya uokoaji imeendelea kwa muda wote tangu jana, kuna watu wako chini mawasiliano yanafanyika na watu hao ni wazima, tumefanikiwa kuwapatia maji, glucose pamoja na kuwapa faraja kuwa vyombo vyote vya ulinzi na usalama viko hapa, na tutahakikisha wanatoka wakiwa wazima, tumefarijika sana kwamba tumeweza kuwapatia hizo huduma wakiwa ndani ya shimo,” amesema Jenerali Masunga.
Jumapili Novemba 17, 2024, Saa 3 Asubuhi: Watu 7 wengine waokolewa
Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Albert Chalamila amezungumza na Waandishi wa Habari asubuhi ya leo na kusema kuwa Wamefanikiwa tena kuokoa watu saba (7) ambao walikuwa kwenye Floor ya Chini kabisa ya Jengo lililoporomoka ambapo wote wamepelekwa hospitali.
Saa 2:55 Usiku: Majeruhi 63 kati ya 70 waruhusiwa, 7 wanaendelea kupokea matibabu, uokozi bado unaendelea, zoezi halijasitishwa
Mpaka muda huu wamekwisha okolewa watu 70, ambapo wamepata matibabu katika hospitali ya Amana, Muhimbili na Mnazi mmoja, muhimbili walikuwa watu 40 ambapo 35 wameruhusiwa na 5 bado wanaendelea kupata matubabu, na katika hospitali hizo mbili wameruhusiwa wote na kubali watu 2, hivyo waliobaki wakiwa wanaendelea kupokea matibabu mpaka sasa, na waliofariki mpaka kufikia saa kumi na moja jioni kwa taarifa zilizothibitishwa na madaktari waliofariki ni 4.
=====
Saa 1:47 Jioni: Waziri Mkuu afika Hospitali ya Muhimbili kuwaona Majeruhi wa ajali, 33 waruhusiwa 7 bado wanatibiwa
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amefika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuongea na majeruhi wa ajali ya ghorofa Kariakoo iliyotokea leo November 16,2024.
PM Majaliwa amesema taarifa iliyopo ni kwamba walikuwepo Wagonjwa 40 ambapo 33 wameruhusiwa na saba bado wanaendelea kupatiwa matibabu.
======
Akiongea akiwa eneo la tukio leo amesema "Zoezi la maokozi linaendelea tangu tupate taarifa saa tatu asubuhi, mpaka sasa hivi Watu 42 wameokolewa na walipoteza maisha ni watano"
====
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewatoa hofu na kuwahakikishia Watanzania na Wanajamii ya Kariakoo kwamba kazi kubwa ya uokoaji inaendelea ili kuwaokoa Watu waliofukiwa baada ya jengo kuporomoka Kariakoo ambapo amesema juhudi za kupeleka oksijeni chini zinafanyika ili wapate hewa safi.
Akiongea na Wananchi baada ya kukagua zoezi la uokoaji leo PM Majaliwa amesema ““Mh. Rais anatoa pole sana kwa Ndugu wa Familia ambazo ni Waathirika wa tukio hili, Wafanyabiashara wengi ambao biashara zenu zipo kwenye jengo na zimeangukiwa na jengo hili pamoja Jumuiya yote ya Kariakoo, pokeeni salamu hizi za pole kutoka kwa Rais na Serikali kwa ujumla, tunajua wakati kazi inaendelea na nimeenda kuona Makamanda wetu wa uokoaji wanaendelea tumeona tuwaache waendelee”
“Lugha nzuri ya sasa ni kuwahakikishia Watanzania na Wanajamii ya Kariakoo kwamba kazi kubwa ya uokoaji inaendelea, Vyombo vya Ulinzi vyote vipo hapa, Wizara mbalimbali zipo hapa, tuombe Mungu wanaookolewa wawe hai, nimeona Mtu ametoka anasema wenzangu wapo chini kwahiyo tuhakikishe hatutumii nguvu bali tunatumia akili ili kuwaokoa kule chini, jitihada za kuwapelekea oksjeni kule chini zinaendelea ili watoe wakiwa hai”
=====
Nimesikitika kupokea taarifa ya ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa katika Kata ya Kariakoo, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam.
Nimeuagiza Uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, na Idara ya Menejimenti ya Maafa kufanya kila linalowezekana kufanikisha zoezi la uokoaji na tiba kwa majeruhi.
Wakati hilo likiendelea na tukimuomba Mwenyezi Mungu awape pona ya haraka majeruhi, tuwaombee pia utulivu na subra ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wenzetu wanaotafuta riziki zao katika eneo hili muhimu kibiashara nchini ambao kwa namna mbalimbali wameathiriwa na ajali hii."
=====
Saa Muda huu mtaa wa Congo Kariakoo uokoaji unaendelea.
Tuwaombee wenzetu wapone
Ghorofa moja katika Mtaa wa Congo na Mchikichi limeporomoka , hadi sasa hali ya majeruhi au vifo haifahamika lakini kwa mujibu wa mashuhuda kulikuwa na watu katika ghorofa hilo
UPDATES
PIA SOMA
- Rais Samia atoa pole kwa waathirika Kariakoo. Aagiza kufanywa kila linalowezekana kufanikisha zoezi la uokoaji na tiba kwa majeruhi
- Ujenzi wa maeneo mengi ya Kariakoo hauzingatii usalama wa Watu na mali zao, hatua zichukuliwe tusisubiri majanga
- ZIMAMOTO: Watano wamefariki, zaidi ya watu 40 wameokolewa ajali ya ghorofa Kariakoo
- Waziri Mkuu Majaliwa awasili lilipoporomoka jengo Kariakoo, uokoaji waendelea
- Ghorofa laendelea kushuka, zoezi la uokoaji lasimama, mwananchi watawanywa
- Sauti za waliofukiwa na Ghorofa Kariakoo: "Tuko hai lakini tunateseka, tusaidieni tutakufa"
- Waziri Mkuu Majaliwa aagiza Polisi kumtafuta mmiliki wa Jengo lililoporomoka Kariakoo
- Dar: Rais Samia atembelea eneo la ajali ya ghorofa Kariakoo, asema vifo vimefikia Watu 20
- Kamati ya Uchunguzi kuporomoka kwa jengo Kariakoo yazinduliwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezindua Kamati ya Wataalamu ya Uchunguzi wa Jengo lililoporomoka katika eneo la Kariakoo ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia ya kuchunguza chanzo cha tukio hilo pamoja na kufahamu ubora na uimara wa majengo yote yaliyoko Kariakoo.
Novemba 16, 2024, majira ya saa 3 asubuhi, ilitokea ajali ya kuporomoka kwa jengo la takribani ghorofa tatu lililopo Mtaa wa Agrey, Kata ya Kariakoo Jijini Dar es Salaam na kusababisha athari kubwa kwa watu na mali katika eneo hilo.
Jumatano Novemba 20, 2024: Rais Samia atembelea eneo la ajali ya ghorofa Kariakoo, asema vifo vimefikia Watu 20
Rais Samia Suluhu Hassan amewasili hivi punde Kariakoo, Dar es Salaam, ambapo jengo la Gorofa liliporomoka Jumamosi na kusababisha vifo vya watu na wengine kujeruhiwa.
Alipofika eneo la tukio, Mkuu wa Nchi alikagua jengo lililoporomoka kabla ya kuhutubia wananchi.
Rais Samia Suluhu Hassan aliyekuwa nchini Brazil kwenye Mkutano wa G20 ametua jijini Dar es Salaam leo na moja kwa moja kuelekea eneo lilipoporomoka jengo Kariakoo. Amesema taarifa aliyopewa, Watu 20 wamepoteza maisha kwenye jengo hilo
Jumatatu Novemba 18, 2024, Saa 3 Alasiri: Shimo mpja lina watu 9, tunawasiliana nao
Kamishna wa Zimamoto John nchini CGF John Masunga amemweleza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwamba **** shimo moja lina watu 9 na wanawasiliana nao na wamefanikiwa kuwaingizia mipira ili kusakuleti Oxygen.
Jumapili Novemba 17, 2024, Saa 8 Mchana: Idadi ya manusura waliotolewa kwenye Vifusi yafikia 77
Idadi ya Watu waliokuwa wamefukiwa na vifusi vya jengo lilioanguka Kariakoo, imefikia 77 baada ya watu wengine 7 waliokuwa kwenye 'basement' kuokolewa leo, huku operesheni ya uokoaji bado ikiendelea
Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila, amethibitisha uokoaji huo akisema “Hawa watu 7 waliokolewa leo walikuwa kwenye basement, na familia zao zimethibitisha walikuwa na mawasiliano nao, jambo linalodhihirisha mafanikio ya operesheni inayoendelea,”
Mapema leo, Novemba 17, 2024, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, John Masunga, alisema changamoto kubwa wanayokutana nayo katika Uokoaji ni muundo wa jengo kuwa na kuta nyingi, zinazowalazimu kuzivunja ili kuwafikia manusura
Jumapili Novemba 17, 2024, Saa 5 Asubuhi: Zimamoto: Walioko chini ni Wazima, tutahakikisha wanatoka Salama
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, John Masunga, amesema bado kuna watu wako chini na mawasiliano yanafanyika na watu hao ni wazima na wanaendelea kuwapatia huduma.
“Shughuli ya uokoaji imeendelea kwa muda wote tangu jana, kuna watu wako chini mawasiliano yanafanyika na watu hao ni wazima, tumefanikiwa kuwapatia maji, glucose pamoja na kuwapa faraja kuwa vyombo vyote vya ulinzi na usalama viko hapa, na tutahakikisha wanatoka wakiwa wazima, tumefarijika sana kwamba tumeweza kuwapatia hizo huduma wakiwa ndani ya shimo,” amesema Jenerali Masunga.
Jumapili Novemba 17, 2024, Saa 3 Asubuhi: Watu 7 wengine waokolewa
======
Jumapili Novemba 17, 2024, Saa 1:00 asubuhi: RC Chalamila - Hakuna aliyefariki kwa kukosa hewa, zoezi la uokoaji halikusimama
Akizungumza akiwa katika eneo la tukio lilipo anguka ghorofa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema "Kwa wale wachache waliopata madhara ya Kifo hadi sasa inavyoonekana walifariki kwenye tukio lenyewe, yaani wakati wa kudondoka [jengo] wamedondokewa na jiwe, au wamechomwa na nondo au namna nyingine. Lakini mpaka muda huu, waliokufa kwa suffocation bado hatujaipata taarifa hiyo, kwa hiyo ile ni taarifa [ya vifo] ya papo kwa hapo wakati tukio llinatokea. Niwaombe sana, tuendelee kushirikiana na hasa kurejesha confidence kwa watu ili madhara yake yasiweze kuwa makubwa zaidi."
Pia, ameongeza kuwa "Jana nilipita kwenye mitandao nikaona kwamba opereshi ya uokoaji imesitishwa. Ukweli ni kuwa operesheni ya uokoaji haijasitishwa. Jengo hili sasa hivi tunavyoongea karibu saa moja au saa moja kasoro, kuna watu tunaowasiliana nao na wapo chini kwa upande wa basement na tumeshawafikia kwa kuwapatia oxygen, maji na glucose. Tumewasihi waendelee kuwa wastahimilivu tunapoendelea kutumia akilli kubwa ili tusidhuru jengo zima na kuweza kuwadhuru wenzetu waliopo pale chini. Kwa tunaamini tumeshawapata wenzetu wachache na wanaendelea kuzungumza tunaamini pengine Mungu aatendelea kutuzaidia ili wenzetu waweze kutoka na wao wakiwa hai. Baadhi ya Wananchi wanasema mbona mnaenda taratibu sana, labda chini haina vifaa vya kusaidia, angalia kuna wheeloader, excavator lakini vifaa hivi hatujavitumia kwani jengo hili tunaogopa kulitikisa tunatumia njia nzuri tuweze kuwafikia wenzetu vizuri zaidi."
Jumapili Novemba 17, 2024, Saa 1:00 asubuhi: RC Chalamila - Hakuna aliyefariki kwa kukosa hewa, zoezi la uokoaji halikusimama
Akizungumza akiwa katika eneo la tukio lilipo anguka ghorofa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema "Kwa wale wachache waliopata madhara ya Kifo hadi sasa inavyoonekana walifariki kwenye tukio lenyewe, yaani wakati wa kudondoka [jengo] wamedondokewa na jiwe, au wamechomwa na nondo au namna nyingine. Lakini mpaka muda huu, waliokufa kwa suffocation bado hatujaipata taarifa hiyo, kwa hiyo ile ni taarifa [ya vifo] ya papo kwa hapo wakati tukio llinatokea. Niwaombe sana, tuendelee kushirikiana na hasa kurejesha confidence kwa watu ili madhara yake yasiweze kuwa makubwa zaidi."
Pia, ameongeza kuwa "Jana nilipita kwenye mitandao nikaona kwamba opereshi ya uokoaji imesitishwa. Ukweli ni kuwa operesheni ya uokoaji haijasitishwa. Jengo hili sasa hivi tunavyoongea karibu saa moja au saa moja kasoro, kuna watu tunaowasiliana nao na wapo chini kwa upande wa basement na tumeshawafikia kwa kuwapatia oxygen, maji na glucose. Tumewasihi waendelee kuwa wastahimilivu tunapoendelea kutumia akilli kubwa ili tusidhuru jengo zima na kuweza kuwadhuru wenzetu waliopo pale chini. Kwa tunaamini tumeshawapata wenzetu wachache na wanaendelea kuzungumza tunaamini pengine Mungu aatendelea kutuzaidia ili wenzetu waweze kutoka na wao wakiwa hai. Baadhi ya Wananchi wanasema mbona mnaenda taratibu sana, labda chini haina vifaa vya kusaidia, angalia kuna wheeloader, excavator lakini vifaa hivi hatujavitumia kwani jengo hili tunaogopa kulitikisa tunatumia njia nzuri tuweze kuwafikia wenzetu vizuri zaidi."
Saa 2:55 Usiku: Majeruhi 63 kati ya 70 waruhusiwa, 7 wanaendelea kupokea matibabu, uokozi bado unaendelea, zoezi halijasitishwa
Mpaka muda huu wamekwisha okolewa watu 70, ambapo wamepata matibabu katika hospitali ya Amana, Muhimbili na Mnazi mmoja, muhimbili walikuwa watu 40 ambapo 35 wameruhusiwa na 5 bado wanaendelea kupata matubabu, na katika hospitali hizo mbili wameruhusiwa wote na kubali watu 2, hivyo waliobaki wakiwa wanaendelea kupokea matibabu mpaka sasa, na waliofariki mpaka kufikia saa kumi na moja jioni kwa taarifa zilizothibitishwa na madaktari waliofariki ni 4.
=====
Saa 1:47 Jioni: Waziri Mkuu afika Hospitali ya Muhimbili kuwaona Majeruhi wa ajali, 33 waruhusiwa 7 bado wanatibiwa
PM Majaliwa amesema taarifa iliyopo ni kwamba walikuwepo Wagonjwa 40 ambapo 33 wameruhusiwa na saba bado wanaendelea kupatiwa matibabu.
======
Saa 11:19 Jioni: ZIMAMOTO wasema atano wamefariki watu 42 tumewaokoa
Kamanda wa Mkoa wa Kizimamoto Kinondoni ambaye ndio Kamanda oparesheni wa tukio la kuanguka kwa ghorofa Kariakoo leo November 16,2024, Mrakibu Peter Mtui, amesema hadi kufikia sasa Watu watano wamefariki na wengine 42 wameokolewa kutokana na tukio hilo.
Akiongea akiwa eneo la tukio leo amesema "Zoezi la maokozi linaendelea tangu tupate taarifa saa tatu asubuhi, mpaka sasa hivi Watu 42 wameokolewa na walipoteza maisha ni watano"
====
Saa 9: 05 Mchana: Waziri Mkuu afika eneo la Tukio Kariakoo, aagiza Oksijeni kupelekwa chini
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewasili Kariakoo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujionea hali ya uokoaji inavyoendelea katika jengo la ghorofa liliporomoka leo Jumamosi Novemba 16, 2024 asubuhi.
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewatoa hofu na kuwahakikishia Watanzania na Wanajamii ya Kariakoo kwamba kazi kubwa ya uokoaji inaendelea ili kuwaokoa Watu waliofukiwa baada ya jengo kuporomoka Kariakoo ambapo amesema juhudi za kupeleka oksijeni chini zinafanyika ili wapate hewa safi.
Akiongea na Wananchi baada ya kukagua zoezi la uokoaji leo PM Majaliwa amesema ““Mh. Rais anatoa pole sana kwa Ndugu wa Familia ambazo ni Waathirika wa tukio hili, Wafanyabiashara wengi ambao biashara zenu zipo kwenye jengo na zimeangukiwa na jengo hili pamoja Jumuiya yote ya Kariakoo, pokeeni salamu hizi za pole kutoka kwa Rais na Serikali kwa ujumla, tunajua wakati kazi inaendelea na nimeenda kuona Makamanda wetu wa uokoaji wanaendelea tumeona tuwaache waendelee”
“Lugha nzuri ya sasa ni kuwahakikishia Watanzania na Wanajamii ya Kariakoo kwamba kazi kubwa ya uokoaji inaendelea, Vyombo vya Ulinzi vyote vipo hapa, Wizara mbalimbali zipo hapa, tuombe Mungu wanaookolewa wawe hai, nimeona Mtu ametoka anasema wenzangu wapo chini kwahiyo tuhakikishe hatutumii nguvu bali tunatumia akili ili kuwaokoa kule chini, jitihada za kuwapelekea oksjeni kule chini zinaendelea ili watoe wakiwa hai”
=====
Saa 6:44 Mchana: Rais Samia atoa pole kwa waathirika Kariakoo
Nimesikitika kupokea taarifa ya ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa katika Kata ya Kariakoo, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam.Nimeuagiza Uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, na Idara ya Menejimenti ya Maafa kufanya kila linalowezekana kufanikisha zoezi la uokoaji na tiba kwa majeruhi.