Songwe: Ujenzi wa runway, Uzio na Taa za kuongozea ndege, vyakamilika Uwanja wa Songwe

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
526
748
1. UJENZI WA RUNWAY YA SONGWE AIRPORT UMEKAMILIKA.

Mradi wa Ujenzi wa sehemu ya kuruka na kutua Ndege "Runways" ambapo kulifanyika ujenzi wa tabaka la juu la lami KM 3.3 imekamilika kwa 100%

2. UJENZI WA UZIO WA KIWANJA CHA NDEGE CHA SONGWE NA TAA ZA KUONGOZEA NDEGE UMEKAMILIKA , JIJINI MBEYA

Ujenzi wa Uzio kuzunguka uwanja KM 10 na Usimikaji wa taa za kuongozea Ndege, imekamilika kwa 100%

3. MRADI WA UJENZI WA JENGO LA ABIRIA LA KIWANJA CHA NDEGE CHA SONGWE JIJINI MBEYA SASA UMEFIKIA ASILIMIA 97.4 .

Serikali kupitia TANROADS imefanya maboresho, Ukarabati, upanuzi na ujenzi Jengo la abiria la kisasa katika uwanja wa Ndege wa Mbeya "Songwe Airport" ili uwe na uwezo wa kutua na kuruka Ndege kubwa na Ndogo na kurahisisha huduma za usafiri wa anga kwa mkoa huo, maeneo ya Jirani na Mataifa mengine.

Miradi mitatu imetekelezwa katika Uwanja huo ambayo ni Ujenzi wa sehemu ya kuruka na kutua Ndege "Runways" ambapo kulifanyika ujenzi wa tabaka la juu la lami KM 3.3, Ujenzi wa Uzio kuzunguka uwanja KM 10 na Usimikaji wa taa za kuongozea Ndege, miradi yote miwili imekamilika kwa 100%, pamoja na Jengo la kisasa la abiria ambalo ujenzi wake umefikia 97.4.

Akizungumzia miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali mbele ya waandishi wa habari, Meneja wa TANROADS mkoani Mbeya Eng: Masige Matari amesema miradi yote katika uwanja wa Ndege Songwe imegharimu jumla ya shilingi bilioni 33.8 na kwamba kukamilika kwa miradi hiyo ni faida kubwa kwa wananchi wa mkoa huo mikoa ya Jirani na Taifa kwa Ujumla.

"Tunamshukuru Mhe Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha kwa ajili ya kuimarisha uwanja wa ndege Songwe, uwanja sasa hivi ni mzuri Ndege zinaruka na kutua Asubuhi, Mchana na usiku, tunamalizia tu Jengo la abiria ili uwanja ufunguliwe rasmi" ameeleza Meneja huyo wa TANROADS Mbeya.

Naye Msimamizi wa Miradi ya uwanja huo wa Ndege Songwe Eng: Emmanuel Fungo amesema kazi kubwa imeshafanyika ambapo kwenye Jengo la abiria tayari miundombinu muhimu imeshasimikwa ikiwemo mifumo ya maji taka, umeme, Viyoyozi, mifumo ya kisasa ya uzimaji moto, mashine za ukaguzi, lifti, na Vioo [Screen] na kwamba Jengo hilo litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria wa ndani na nje ya Nchi.
1683455026645.jpg
1683455091872.jpg
1683455103139.jpg
1683455118200.jpg
1683455130326.jpg

1683455288458.jpg
1683455311964.jpg
1683455327999.jpg
1683455375222.jpg
1683455400969.jpg
1683455885069.jpg
1683455898716.jpg
1683455913155.jpg
1683455921119.jpg
1683455928964.jpg
1683455938978.jpg
1683455945281.jpg
1683455954174.jpg
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Back
Top Bottom