Songwe: Basi la Kampuni ya Kilimanjaro Express lapata ajali, watu wanne wafariki dunia

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,381
6,945
Bus la kampuni ya Kilimanjaro limepinduka asububuhi hii mkoani Songwe likitokea Tunduma kuelekea Jijini Dar es salaam ambapo taarifa za awali zinaeleza ajali hiyo imesababisha watu kadhaa kufariki na uwepo wa majeruhi, taarifa kamili zitakujia hivi punde.

===================

Basi la Kampuni ya Kilimanjaro Express limepata ajali kwa kupinduka asubuhi ya leo Machi 14, 2022 Mkoani Songwe wakati likitokea Tunduma kuelekea Jijini Dar es Salaam.

Taarifa za awali za mashuhuda waliopo eneo la tukio zinaeleza ajali hiyo imesababisha watu kadhaa kufariki na uwepo wa majeruhi.

Ofisa Mmoja wa Kilimanjaro Express amekiri kutokea kwa ajali hiyo lakini hakuwa tayari kuelezea kiundani kwa madai siyo msemaji wa kampuni. Juhudi za kumpata RPC wa Songwe, Janeth Mgomi zinaendelea ili kupata ripoti kamili.

UPDATES;

Watu wanne wamefariki papo hapo huku wengine 35 wakijeruhiwa katika ajali ya basi la Kilimanjaro Express lililopindukia korongoni eneo la Senjele wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe, Rashid Ngonyani amesema ajali hiyo imetokea saa moja asubuhi baada ya dereva wa basi la Kilimanjaro Express kuwa kwenye mwendokasi na kutaka kuyapita magari mengine yaliyokuwa mbele yake.

Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba amesema majeruhi wote 35 wanaendelea vizuri ambapo kati yao saba wamelazwa Hospitali ya Wilaya ya Mbeya na wengine 28 wakitibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe

Ajali Basi la Kilimanjaro.jpg

Ajali.jpg

Basi la Kilimanjaro.jpg


01f135e7-85f5-47f6-9b4f-e1c9f70a6cbb.jpg

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omary Maumba alimjulia hali miongoni kwa majeruhi wa ajali ya basi kampuni ya Kilimanjaro, Yusuph Ramadhan ambaye yeye na wenzake sita walikimbizwa katika Hospitali Teule ya Ifisi iliyoko mkoani Mbeya. PICHA: Grace Mwakalinga, SONGWE

18272925-7983-4544-bcf2-dc59a807d0e6.jpg
 
Back
Top Bottom