LGE2024 Songea: Wanachama CCM walalamika mgombea aliyeshinda kura za maoni kutopewa fomu ya kuwakilisha chama Uchaguzi Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Sep 23, 2024
45
24
Kunaendelea kuchangamka uchaguzi serikali za mitaa mkoa wa Ruvuma wanachama mmetuboa.

IMG_20241105_112508~2.jpg

Hii nimeikuta ofisi ya TAKUKURU Chama cha Mpinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma kwa kweli mnatuchosha wanachama kulikuwa na sababu gani yakutupotezea muda kwenda kupiga kura za maoni wakati mna wagombea wenu mmeshawaandaa?

Hiyo ni Halmashauri ya Mdaba wameamua kusambaza barua ya malalamiko kuhusiana na kumteuwa mgombea ambaye hajaongoza kwenye kura za maoni na wanahisi moja kwa moja mchakato ulitawaliwa na mazingira ya rushwa.

Hapa Songea napo janja janja tu , huku kwetu mwengemshindo tuliyemtaka jina lake halikurudi kabisa kwenye kura za maoni hali kadhalika nasikia huko Likuyu fusi mgombe ametishiwa kwingine nako ameteuliwa mwanachama mpya kutoka chama cha upinzani ambaye nae hakupita kwenye kura za maoni na hawamtaki wananchi. Narudia kuuliza kwanini mlitupotezea muda wakati mna watu wenu mlishawapanga?

Mfaranyaki nako aliyekuwa mwenyekiti wa mtaa hakupata kura za kutosha ila kwenye kinyang’anyiro cha kura za maoni kaona mchezo mchafu wote uliofanyika siku ya kupiga kura kama vile sanduku la kupigia kura kukumbatiwa vievile kuletwa makundi ya vijana kupiga kura anasikia kabisa wanavyopewa maelekezo tiki namba Fulani, ila kukata rufaa hakutaka kwa kuhofia Maisha yake “mtu katumia nguvu kubwa na pesa kuhakikisha anashinda, alafu unaenda kukata rufaa anaondolewa unadhani nini kitatokea?”

Wanachama mmetuchosha kura mkapige wenyewe kama mlivyochukua uamuzi wa kuteua wagombea.
 
Back
Top Bottom