Songa - Hisia za moyoni

Quotes kutoka kwenye wimbo.
Imani ni bora kuliko dini..

Meno hayalindi palipo ulimi..
 
Intro...


Beat imenipa hisia mpaka najikuta nasahau pa kuanzia lakini ahsante DOUBLE naitwa SONGA


Verse 1


Imani ni bora kuliko dini inashangaza sana nimekuwa bora kuliko mimi naamini meno ya lindi hulipa ulimi kama kazi yako dhambi unadhani malipo nini. Na hii siwezi kuifanya pasipo ninyi, nipe shavu nirushe kofi kwa ruksa pasipo Mwinyi. Wanauliza “eti, mwisho wa kifo lini?” nawambia kipo hai nadhani mwisho ni chini. Sometimes magonjwa ya hata usipozini, unaweza ukawa bora hata kama usipowin. Na sio fix of course, kwa Mwanza ukimtoa Fid, hakuna kama 6-O'clock. Hii ndo new career Songa ndo mkubwa akisimama hakuna wa kukalia, hakuna wa kusalia. Duniani hakufai ndo maana ukizaliwa tu, unalia.


Chorus...


Polepole ndo mwendo, tunapambana, yaliyo moyoni huwezi kuyatazama. Hisia za moyoni x4...


VERSE. 02


Wanapagawa na mimi, nasikitika kuona vijana wanakufa kwa madawa na UKIMWI. Ukiwashwa hauzimwi, unakunwa na mistari kutoka kwa kichwa ambacho hakijadata na Udini, silaha ni ulimi, ninachotaka ni kuona amani inapatikana Sudan ya Kusini. Kukiwa na vita hata nyumbani haulimi. Kipi kinaongoza, uongo ama dhambi ya kuzini? Songa na BEAT kama uchafu na OMO. Ukijiongeza ghafla utapata ulemavu wa mdomo. Mshono ni rough, tough rap. Hujui kuchana halafu unataka ule shavu la promo. “Eti Songa utaflow wapi?” Jaribu kumuuliza demu wako atakwambia nishafanya show ngapi. Songa nna roho safi, nawashangaa emcees wanaosema akili ni nywele wakati kichwani wana low-cut.


Chorus...


Polepole ndo mwendo, tunapambana, yaliyo moyoni huwezi kuyatazama. Hisia za moyoni x4...


Funny, huh!? Inabidi utoe money bruh, ukapate upepo Unguja kisiwa cha Zanzibar. Mi ni mkali dah, hata ukinitupa Kenya nita-run 2-5-4 muulize Kaligraphy. Kawaida ya mlevi kupata ajali bar, silali njaa nazisaka salary za manispaa. Anayefanya nisimame ndo anayenifaa, amani kwa waliotangulia kwenye ramani ya Africa, amani ni mzaha, maisha sio shida tu utashangaza kama hupati raha. Naam me star, usiulize nipo chimbo milipuko kama Taliban. No swag, nikiwa booth napiga picha na-upload NO TIME (no time...). Demu wako nungunungu NO HUG, Songa ni nchi ya flow bro NO FLY.


Chorus...


Polepole ndo mwendo, tunapambana, yaliyo moyoni huwezi kuyatazama. Hisia za moyoni x4...
 
Songa anajua sana, hii 'Hisia za Moyoni' ni moja ya kazi zake bora zaidi... tatizo la huyu maalim ni uvivu, hachelewi kutoa ngoma ina verse moja tu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom