Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,685
- 119,325
Wanabodi,
Utangulizi
Kwanza niungane na Watanzania wenzangu kutoa pole kwa Watanzania wenzetu waliopoteza maisha katika tetemeko hili, kuwatakia uponaji wa haraka wa majeruhi na kuunganisha nguvu zetu kama taifa kuwasaidia kwa hali na mali wahanga wa tukio hilo ambapo kesho asubuhi, naamini rais wa JMT, Mhe. Dr.John Pombe Joseph Magufuli, atadamkia Mwanza na kuelekea Bukoba kushuhudia na kutoa pole kwa karibu.
Tanzania Kama Nchi Tujifunze Nini na Kwanini?.
Tanzania kama nchi tunapaswa kujifunza kuwa na preparedness ya haraka kwa majanga kama haya, japo hayatabiriki ni lini yanaweza kutokea, na hayana dalili yoyote ya kabla ili kutoa tahadhari watu wajiandae kabla, lakini kuna maeneo prone kwa matetemeko, yanajulikana na yanalocetika kabla, hivyo it is a high time sasa, serikali itoe standards za ujenzi katika maeneo yote ya Rift Valley, ambayo ndiyo pekee huweza kukumbwa na matetemeko yenye madhara, ili kuepusha impact ya majanga kama haya!.
Kwa Nini Tujifunze kwa Japan Ambayo ni Nchi ya Matetemeko.
Nchi ya Japan imekuwa ikikumbwa na matetemeko ya mara kwa mara, hivyo ujenzi wa nyumba zote Nchini Japan unazingatia viwango fulani vya ubora kama tahadhari ya kutokea matetemeko wakati wowote! .
Tukichukulia somo la matetemeko makubwa kutoka Japan, matetemeko yakitokea huweza kujirudia rudia na kuja kwa nguvu zaidi, hivyo it is high time, Tanzania tujiandae kwa majanga kama haya na hatua ya kwanza ni kwa kuainisha maeneo yake yote yaliyo katika ukanda wa Bonde La Ufa, ambalo ndilo eneo prone kwa matetemeko ya ardhi na kuweka standards fulani za ujenzi ili hata kukitokea matetemeko makubwa ya aridhi kama yale ya Japan, madhara yatakuwa ni kidogo! .
Matetemeko ya Kupita na Tetemeko la Kutokea.
Nakumbuka toka nikiwa mtoto mdogo mjini Mwanza sii mara moja au mbili kusikia kumetokea matetemeko madogo madogo ya aridhi na kusababisha nyufa katika majengo yenye ubora hafifu, ila kumbe matetemeko hayo hayajawahi kutokea nchini Tanzania, bali yalikuwa yanatokea sehemu nyingine, na kupitia tuu Tanzania, hili tetemeko la Bukoba, ndio tetemeko langu la kwanza kusikia limetokea Tanzania na kusababisha madhara makubwa vikiwemo vifo!. This time limetokea katika eneo la Nsungu, lililopo km. 43 kutoka mji wa Bukoba.
Historia ya Matetemeko Tanzania.
Kwa mujibu wa US Geological Survey, chanzo cha tetemeko hilo ni umbali wa kilometa 10 chini ya ardhi na lilikuwa na Magnitude ya 5.7 ambacho ni kiwango kikubwa ukaribu wa Ziwa Victoria kumesaidia sana kupunguza impact! .kubwa lolote lililosababisha nyumba kubomoka na kusababisha maafa!. Tetemeko jingine la kiwango cha M 4.3 lilitokea eneo la Ziwa Victoria December 2013. Tetemeko la kwanza kubwa la kihistoria kurekodiwa nchini Tanzania ni la kiwango cha M 7.2 lililotokea mwezi July 1919, Ziwa Tanganyika na jingine la kiwango cha M 6.8 lilitoke Ziwa Tanganyika tena Mwezi December 2005 ambayo yote yalisababisha vifo!.
Je Tujiandae Kwa Natural Disasters Au Kwa Vile ni Kazi Mungu, Tumuachie Mungu?.
Tena speaking of natural disasters, tusijiandae kwa matetemeko ya ardhi pekee, bali pia tujiandae kwa kuchukua tahadhari dhidi ya natural disasters nyingine zote zinazo husiana na kwenda sambamba na matetemeko ya ardhi!, hizi ni tahadhari za milipuko ya volcano kwenye mlima ambapo Volcano iliyopo chini ya Milima kama Mlima Kilimanjaro na Mlima Oldonyo Lengai ni volcano hai, (active) ambayo bado iko hai ila imepoa tuu lakini siku ya siku ikifika, inaweza kulipuka wakati wowote! .Volcano ya Mlima Meru ni volcano mfu,(dormant) , haiwezi tena kulipuka!.
Uhusiano Kati ya Matetemeko ya Ardhi na Milipuko ya Volcano
Kuna uhusiano kati ya matetemeko ya ardhi na milipuko ya volcano kwa sababu vyanzo vya matukio yote mawili ni kile kile, ambapo husababishwa na mgandamizo mkubwa wa hewa ya moto iliyo chini ya ardhi kuyeyusha miamba kugeuka uji wa magma ya moto ambayo kutokana na pressure hulipuka huko huko chini ya ardhi na kutafuta upenyo wa kutoka huko huko chini kwa chini, mlipuko wa volcano hiyo, yaani, magma ya moto ukifika nje ya uso wa dunia ndio hutoa milipuko wa volcano, na kutengeneza milima isipofika ya volcano kama Mlima Kilimanjaro, Mlima Meru, Mlima Oldonyo Lengai etc .
Mara nyingi milipuko hiyo huishia huko huko chini ya ardhi au kulipukia ndani ya vyanzo vya maji kama baharini na kwenye maziwa hivyo kusababisha mawimbi makubwa kama El Nino, au hubakia huko huko chini ya ardhi.
Chanzo Cha Matetemeko ya Ardhi.
Sasa eneo ilipokuwe hiyo magma ya moto iliyotoka hubakia tupu na ardhi ya upande huu na ule hujisogeza kujaza lile eneo la wazi, ni katika kujisogeza huko ndiko tetemeko la ardhi hutokea kwa ardhi kutembea kujaza nafasi wazi chini ya ardhi husika kwa pande la ardhi kuzama chini kujaza nafasi wazi kwa kutengeneza Bonde La Ufa au pande la ardhi kupanda juu kutengeneza table mountain kama Milima ya Kipengere au kusongamana juu ya ardhi na kutenge folding mountains kama Usambara na Uluguru.
Tetemeko Limeishatokea, Watu Wamekufa, Uharibifu Umetokea!, What is A Way Forward?.
Kwa vile tetemeko hili ni kama la kwanza kubwa hivi nchini mwetu kwa miaka ya karibuni, tusikae na kujibweteka kudai ni kazi ya Mungu tuu and there is nothing we can do! . No hata kama ni natural disaster lakini sasa na sisi lazima tuanze kujiandaa kwa kuwa na preparedness ya kuzuia madhara kwa natural disasters ambazo tayari tumeisha jua zipo na zitatokea ila hatujui ni lini, kama vile kila nyumba yenye umeme hatakikiwa kuwa na earth rod kuzuia madhara ya radi, vivyo hivyo nyumba zote kwenye ukanda wa Bonde La Ufa ziwe na preparedness ya kuhimili matetemeko ya ardhi, na maeneo yote ya milima ya volcano active yaani volcano hai , yawe ni maeneo ya hifadhi kusiruhusiwe makazi ya watu ili siku ya siku, kusiwepo madhara makubwa! .
Kwa leo nawatakia Jumapili Njema na kesho nawatakia Eid Mubarak njema!.
Pasco