Soko la Madini lazinduliwa Dodoma

mamayoyo1

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,011
1,019


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Binilith Mahenge amewataka wadau wote wa madini mkoani humo, kuacha vitendo vya utoroshaji wa Madini kwani yeyote atakaye kamatwa akitorosha madini atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo utaifishaji wa madini atakayokuwa akiyatorosha.

Dk. Mahenge ameyasema hayo Leo wakati akifungua Soko hilo ambapo amesema uanzishwaji wa Soko ni kufuatia dhamira nzuri ya Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa wachimbaji wadogo hivyo kuwataka wadau mbalimbali kulitumia vizuri ili kuwanufaisha.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya madini nchini Profesa, Idris Kikula yeye amesema kufuatia ufunguzi wa masoko hayo hapa nchini mapato yameongezeka kwa kiasi kikubwa tofauti na ilivyokuwa hapo awali na kuwasisitiza wanunuzi kuyatumia maduka hayo ipasavyo kwani kinyume na kufanya hivyo yatawagharimu.

Akitoa taarifa ya soko la madini katika mkoa wa Dodoma Afisa Madini wa Mkoa,Jonas Mwano amesema katika soko hilo madini yote yatauzwa pamoja na tozo za Serikali zote zitachukuliwa mahali hapo pasipo kuwasumbua wachimbaji wadogo.

Soko hilo la Madini lililopo katika Ofisi ya zamani ya Mkuu wa Mkoa limeanza kufanya kazi rasmi May 04 mwaka huu.
 
Vitu vinavyoanzishwa kisiasa huwa havidumu. Mark my words baada ya miaka miwili hakuna soko apo. Itakuwa plaza za kuuza nguo, simu na vitu vya electronics.
 
Back
Top Bottom