Siyo lazima kila alama ya mvuka kwa miguu (zebra) dereva wa gari asimame, Sheria ifumuliwe imepitwa na wakati

Sheria yetu ya usalama barabarani (Road Traffic Act, 1973) hailazilimishi dereva kusimama bila uwepo wa mvukaji. Sheria inamtaka dereva kusimama endapo kuna mwenda kwa miguu anataka kuvuka.
Hata hivyo kuna baadhi ya vivuko vya waenda kwa miguu vyenye alama au mchoro unaosomeka "STOP', hapa ni lazima kusimama hata kama hujaona mvukaji anataka kuvuka. Alama hizi zinawekwa sehemu yenye waenda kwa miguu wenye changamoto kama watoto au wenye ulemavu na kwenye mazingira yenye uoni hafifu.

Pia sheria haitamki gari kuzuiliwa endapo dereva kafanya kosa. Kinachofanyika ni kuzuia gari ili liwe kama dhamana, lakini sheria haitamki hivyo.

Makosa yanayofanywa na askari yasichukuliwe kama madhaifu kwa sheria. Hata hivyo kuna haja ya kuipitia upya RTA ili kurekebisha mambo yaliyopitwa na wakati.

Hata hivyo ili kuleta ufanisi kuna haja ya kufanya mabadilko kwa kikosi cha usalama barabani ili kiwe na askari wenye weledi wa sheria wanayosimamia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
IPO hoja lakini
Takukuru wanaweza pia kuzuia na kupambana na rushwa kwa kubadili sheria,

Sheria mbovu zinashawishi rushwa,
Inamaa dereva ambaye hakubali kosa, hawezi kuondoka na gari lake hadi siku kesi itakapoamriwa!
Swali, ni ninani Huyo anaeweza acha chombo cha usafili kusubili kesi wakati ana safari kwa kutumia chombo hicho?
 
Sheria inasemaje kwa ambaye hakubaliani na kosa ili aendelee na safari pasipo kuzuiliwa chombo chake?

Nani anawajishwa kumkosoa askari anaempa adhabu ya faini dereva sehemu ambayo hakuna kibao cha stop, hakuna mvukaji lakini kwa sababu pana zebra basi dereva anahesabiwa kosa?
 
Hongkong kwenye zebra karibu zote kuna taa ya kuongoza watu wakati wa kuvuka (kama ilivyo Mlimani city pale), kwa bongo taa za namna hiyo zipo lakini nyingi zimewekwa kwenye makutano ya barabara...
 
Hongkong kwenye zebra karibu zote kuna taa ya kuongoza watu wakati wa kuvuka (kama ilivyo Mlimani city pale), kwa bongo taa za namna hiyo zipo lakini nyingi zimewekwa kwenye makutano ya barabara...
Kuna kampeni ya kuweka taa kwenye maeneo ya shule, ila bado ni chache.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kampeni ya kuweka taa kwenye maeneo ya shule, ila bado ni chache.

Kama hiyo kampeni imepigiwa upatu na CCM, ujue haitafanyika...unless kuwe na NGo au wafadhili ambao wanasimamia hilo
 
Usilete hisia kwenye mambo yanayohitaji sheria, hakuna dereva asiyepisha LA sivyo kila siku tungesikia vifo vya watembea mguu,

Tunachosema hapa, hizo zebra hata kama hakuna MTU wa kuvuka, ukipita trafiki anakukamata ,
Ukikamatwa kwa sababu hakuna mtu wa kupita jua wewe sio dereva hata walivyokua wanakamata kipindi hawajakatazwa tuliwatafsiria hiyo sheria kuwa mpaka wawepo watu wa kupita sio unasimama tu unasimama ili iweje bara bara pamoja na alama zake inaongea nilipiata bara bara moja huko Arusha ya East Afrika wamechora naruhusiwa kulipita gari lingine ila sehemu ni hatarishi waliochora walikosea kwa hiyo sio unachoona Road kipo sawa jiongeze pana dereva mmoja Lori broke zimefeli badala ya kuliacha lipite alikua anasimamia sheria ni Mungu ndio alimuokoa maana alikoswa koswa sana baada ya kusimama tukamwambia ukifata sheria sehemu ya ajali utakufa jamaa anapiga honi yupo mteremkoni anakomalia sheria...mimi hata kwenda kuhakiki barua sijui Polisi mambo ya vyeti niligoma hakuna sheria hiyo na niliwaambia kila kitu kipo kwa mujibu wa sheria sio Utashi wa IGP leo kipo wapi yaani kila kitu watoe wao harafu tena nikahakiki kwao huko huko si ujinga huo...
 
Tatizo hata wavuka barabara nao hwajitambui, gari inasimama mtu anaendelea ongea na simu, wanapita wachache akiona wamevuka na yeye ndo anataka vuka
 
RTA haisemi kwamba askari azuie gari kwa kosa la dereva (hapa sizungumzii kwamba gari ni bovu au limehusika katika ajali).
Pengine wanatumia sheria nyingine au utashi wa askari husika, ila kumlazimisha dereva kutekeleza jambo fulani. Kuna mazingira hata dereva mwenyewe anaweza kuzuiliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa hauoni hapo sheria inamwachia askari kuamua vyovyote atakavyo ikiwa pamoja na kuzuia gari LA dereva ..hata kama ana safari zake jambo linaloshurutisha rushwa au faini ?
 
Haya bado tunaendelea kuonesha uafrika wetu kuwa ni laana

Aslimia 20 ya ajali za barabarani hutokea Afrika, huku ikiwa na asilimia 2 tu ya magari yote duniani.
 
Lakini wana mamlaka ya kukupokonya leseni kwa kisingizio kwamba hujafuata alama za barabarani!

Tena wakiamua wanaweza kukubandulia kabisa na plate namba za gari wakang'oa wanasema sheria inawaruhusu kufanya hivyo wakigundua kuna kosa
 
Lakini wana mamlaka ya kukupokonya leseni kwa kisingizio kwamba hujafuata alama za barabarani!

Tena wakiamua wanaweza kukubandulia kabisa na plate namba za gari wakang'oa wanasema sheria inawaruhusu kufanya hivyo wakigundua kuna kosa
Aisee hakuna sheria hiyo Mkuu mbona mnaishi kwa mazoea ya kijinga na kusema ndio sheria mmesomea wapi trafiki aje kuchukua ignition switch yako bila ridhaa yako useme ni sheria aisee...
 
Uko sahihi. Mimi nimekuwa napigwa faini mpaka nashangaa. Yaani hata faini Kwa spidi 55 sehemu ya 50! Ni vigumu gari kutembelea 50 lazima ipande kidogo unajitahidi kuishusha tena. Ila hakuna namna. Akiomba leseni anaandika faini na huna Cha kufanya. Kwa kweli wanafikiri kumiliki gari wewe ni tajiri na pesa ipo mfumo wa shati bila matumizi maalum.
 
Haya bado tunaendelea kuonesha uafrika wetu kuwa ni laana

Aslimia 20 ya ajali za barabarani hutokea Afrika, huku ikiwa na asilimia 2 tu ya magari yote duniani.
Tujadili sheria ya usalama barabarani inasemaje kama dereva hakubaliani na kosa anatakiwa kusikilizwa na nani pasipo kuharibu safari yake kwa kushikiliwa chombo chake?

Mfano mwingine, kunaweza kukawa na kasoro ndogo tu ya kreki ya kioo ambayo mathalani kioo kimekreki wakati huo, Sheria kwanini isiweke utartibu wa kuonya - Pre-offense! Kwamba dereva aandikiwe onyo liliso na faini kwenye database yao halafu baada ya siku saba ikipita ..popote akija kukamatwa askari mwingine akikagua na kuikuta hiyo taarifa anaaandika faini kamili?

Hii ya kumwandikia faini dereva papohapo pasipo kuonya ...ni sheria za kikoloni sana kwasababu baadhi ya ubofu hutokea ghafla ikiwemo kioo, taa za breki n.k
 
Hapa bongo ajali nyingi watu hugongewa kwenye zebra kifup mtu akiwa nachombo chamoto bongo kusimama anaona kero sana we unataka tena sheria zilegezwe mbona watembea kwamguu mtawamaliza
 
Aisee hakuna sheria hiyo Mkuu mbona mnaishi kwa mazoea ya kijinga na kusema ndio sheria mmesomea wapi trafiki aje kuchukua ignition switch yako bila ridhaa yako useme ni sheria aisee...
Bro sheria haipo, lakini sheria iko wazi kumwachia trafiki ombwe LA mamlaka ya kipolisi kumdhibiti dereva asitoroke!
Moja ya njia hizo ni kuchomoa funguo, kushikilia leseni, kung'oa vibati vya plate namba. Na sheria IPO kimya kuhusu maamuzi hayo mabovu ya askari!

Tena wanaweza kukubambikia na kosa jingine la ukaidi na ulitaka kuwagonga walipokuamuru hukutii!

Wakakusweka ndani maana sheria imenyaza kimya juu yao!
Ndiyo maaana nasema TUFUMUE HII SHERIA YA BARABARANI IMEPITWA NA WAKATI IMEKAA KIKORONI SANA!
 
Hapa bongo ajali nyingi watu hugongewa kwenye zebra kifup mtu akiwa nachombo chamoto bongo kusimama anaona kero sana we unataka tena sheria zilegezwe mbona watembea kwamguu mtawamaliza
Siyo kweli, weka takwimu ! Ndiyo maana nikasema ziwepo zebrà nyekundu kuonesha ulazima, na nyingine ziwepo kuonesha tahadhali kwa wote dereva na mpita njia ambayo mtu anavuka tu kukiwa salama/ siyo lazima kusimama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…