Habari
Tunaongozwa na sheria zilizo expire muda wake!
Iko haja sheria ya usalama barabarani ifanyiwe marekebisho kwani ilitungwa zamani enzi hizo Tanzania hatukuwa na barabara za lami na magari ya kutosha!
1. Siyo kila zebra lazima mwenye gari asimame hata kama hakuna mtu,
lakini baadhi ya Trafiki waliowrngi huitumia sheria hii vibaya kujinufaisha na kubambikia watu!
Hii yote inawezekana kwasababu sheria inawalinda trafiki kumkandamiza dereva! Hivyo hiyo sheria imepitwa na wakati kuwepo sasa!
Kama nchi sasa tunatakiwa tuwe na zebra za aina tofauti kuliko sasa vibao vyote ni black and White!
Nashauri Kuwekwe sheria mpya kwa vibao vya alama za wavuka kwa miguu iwe kama ifuatavyo!
1. Zebra za mistari nyekundu na nyeupe hiyo viwekwe kwenye vivuko vya watembea mguu kuonesha ni lazima kwa dereva kusimama (Lazima); na mara nyingi vibao hivyo vitawekwa kwenye maeneo mhimu tu ya msongamano! (Hii itamuamrisha dereva lazima kusimama kupisha watembea kwa miguu)
2. Zebra za mistari nyeupe na kijani itumie kuonesha utahadhari lakini hii iwe rasmi kwa wote kwa mtembea kwa miguu kuonesha atavuka endapo tu kukiwa salama!
(Hii itamuelekeza mtembea kwa miguu kuvuka kwa tahadhari kwa usalama wake)
Je, Endapo kuna kosa na dereva hakubaliani na kosa hilo sheria inasemaje kuhusu adhabu?
Kwa sheria ya sasa kwakweli ni mbovu mno, Endapo traffic akiamua kumbambikia kosa dereva ambalo hakubaliani nalo, huwa kuna fomu maalum ya kujaza na dereva kusaini ili kwenda mahakamani!
Na kama itakuwa hivyo lazima chombo cha moto anachoendesha dereva kishikiliwe police hadi pale mahakama itakapoamua!
Sasa chukulia mfano: dereva anakwenda mbeya, halafu kakamatwa chalinze kwa kosa ambalo hakubaliani nalo, inabidi Apache gari hapo chalinze hadi pale mahakama itakapoamua ( Hii sheria ya muundo huu haitekelezeki na sijui waliotunga walikuwa na akili gani)
Nashauri, endapo kuna mazingira ya dereva kutokubaliana na kosa, uwekwe utaratibu wa kuchukua maelezo ambayo yanakuwa kwenye karatasi kaboneted, polisi aandike maelezo yake, pia dereva naye aandike palepale maelezo yake pasipo kushurutishwa, halafu nakala ya juu achaniwe dereva apewe ili akaripoti kwenye kituo cha polisi kilichokaribu naye ndani ya siku 7 baada ya tukio, then ipangwe Sikh ya kusikiliza hiyo kesi online kupitia ofisi za police traffic na iamuriwe baada ya kusikiliza pande zote (dereva na traffic )
Kwa dereva ambaye hatakwenda kuripo kwa ajili ya kesi hiyo aandikiwe faini kwa maana kesi itakuwa imesikilizwa kwa upande mmoja!
Hii italeta nidhamu kwa trafiki wanaobambikia watu makosa kwasababu, endapo kutakuwa na malalamiko mengi ya dereva kutokubaliana na kosa kwenye database ya polisi na ikionesha trafiki yule yule kufanya kosa kwa wengi basi ASKARI huyo aondolewe barabarani!
Zipo sheria nyingi sana za kufumua lakini kiufupi sheria ya usalama barabarani ifumuliwe!
Usipokuwa mvumilivu barabarani kwa sasa unaweza piga trafiki kwa jaziba barabarani kumbe yeye hana hatia Bali anasimamia sheria mbovu ipasavyo kwa maslahi yake!