Madawati kitu gani bana kwa nchi kubwa kama Tanzania, me ningewashauri kwanza wafanye assessment kujua upungufu uliopo yan yanahitajika madawati mangapi nchi nzima then wajue gharama kwa kila dawati na jumla, then waangalie namna ya kuraise hiyo hela, mfano wanaweza kuangalia watumiaji wa simu wako wangapi na matumizi yao kwa wiki, then ipitishwe tarrif ya kimya kimya unaweza kukuta mtu mwenye matumiz ya kawaida akakatwa hata sh. 100 tu, bila kelele lakin, au waende kwenye sekta ya elimu watafute pa kuraise hiyohela, hii sio issue ya mkuu wa nchi ku adress, au waruhusu halmashauri ziwe zinauza hisa watu wawekeze kwenye halmashauri zao, hii nchi haipaswi kuangaliwa kutokea dar es salaamu tu, inahitajika devolution japokuwa ina madhara kisiasa ambayo jamaa zetu hawako tayar kuachia.