Sitaki dawa

Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,328
23,890
SITAKI DAWA

Jumamosi, 25/06/2016

Nawaza nianzie wapi kuelezea kilichonikuta nashindwa, lakini hasa ni kukosa maneno ya kukielezea. Nimetamani nikae kimya, nisiseme, maana ninafahamika na wengi na itaniharibia picha yangu kwenye jamii. Nimetafakari sana kuchukua maamuzi magumu lakini nfasi yangu haikuumbwa hivo, nimeshindwa. Labda ningezaliwa Mhehe, lakini mchagga mimi hata vidonge vya piriton vilikuwa shida kumeza.

Lakini nimeamua nitasema. Sijui baada ya kusema nini kitatokea, sijui jamii itanichukuliaje, ndugu jamaa na marafiki watasemaje au labda watanitenga…lakini nitasema.

Wazazi wangu – MNISAMEHE! Zaidi ya yeyote yule nimewaangusha. Mlikuwa na mategemeo makubwa juu yangu. Mmenisomesha kwa gharama kubwa na mlikuwa na matumaini ya mimi kufika mbali.

Mlioniita Mentor – MNISAMEHE! Najua ni wengi walioniona kama kijana wa mfano, kaka na ndugu…mnisamehe kwa kuwaangusha. Sitamsingizia shetani wala mtu mwingine yeyote kwa kosa langu.

NIMEATHIRIKA! Na sijivunii…

July, 2015

Naamini ni wakati huu. Kulitangazwa nafasi za masomo nchini Uingereza chini ya ufadhili wa Commonwealth (Common wealth Scholarships 2015). Nami nilikuwa nimejiwekea malengo kuwa hadi mwaka 2016 ni lazima nikasome masomo yangu ya Uzamili (masters) hata ikibidi kwa kujilipia. Nilitembelea tovuti tofauti tofauti nikitafuta ufadhili kwa ajili ya masomo yangu. Hakuna tangazo lililotolewa ambalo sikuliomba. Fulbright, Mwalimu Nyerere, DAAD, World Bank, IMF, n.k n.k niliomba zote. Nilikuwa na malengo ya kwenda kusoma masomo ya usimamizi wa miradi au utungaji sera. Ndoto yangu ilikuwa moja tu: SIKU MOJA NIWE KATI YA WAFANYA MAAMUZI KATIKA NCHI HII.

Nilichoka kuwa mtu wa kuandika programs kila siku halafu aidha fedha zinaliwa au miradi inawekwa kwenye shelfu. Nilichoka kuhusishwa kwenye miradi isiyo na kichwa na miguu, miradi isiyoangalia vipaumbele vya taasisi au nchi. Nilichoka! Nikasema nitaachana na masomo yangu ya sayansi ya kompyuta nikasome masomo yatakayonifanya niwe mtunga sera na mtoa maamuzi. https://jamii.app/JFUserGuide ME!!!! (mnisamehe am so mad at me)

Wakati huu ndipo kulipotangazwa nafasi hii ya Commonwealth. Nakumbuka nililiona tangazo kupitia tovuti ya TCU na ilikuwa imebaki wiki moja au mbili hivi kabla ya tarehe ya mwisho kwa hapa kwetu. Nilijipinda ofisini kuandika insha kama tatu kuelezea kwa nini mimi niipate nafasi hii na si mwingine. Niliandika kutoka moyoni. Nilifanikiwa kumaliza mapema nikatoa nakala kama walivyoelekeza; za kupeleka wizara ya elimu na za kutuma kwa barua pepe.

Siku, wiki na miezi vilipita nami nikaitwa kwenye usaili, nikaenda kufanya mitihani ya Kiingereza ya IELTS pale ubalozi wa Uingereza, nikafaulu vizuri.

Alhamisi, 23 Juni 2016 - Juzi

Nilipewa majibu kuwa nimechaguliwa pamoja na wenzangu wawili kwenda Uingereza (chuo sitokitaja) kwa ajili ya masomo ya Uzamili katika Usimamizi wa Miradi kuanzia mwezi wa tisa. Nilifurahi sana, nikapiga magoti ofisini nikamshukuru Mungu kuwa mwaminifu kwangu. Nilimuomba mwaka huu niende shule na amenijibu. Tena kaniongezea baraka kwa kuwa ninapewa ufadhili wa 100%. Hakuna hata senti yangu nitakayotumia katika maosomo yangu hayo.

Jana asubuhi nilitumiwa mkataba wangu pamoja na fomu za afya ambazo nilitakiwa kuzijaza na kuzirudisha ubalozi wao Jumatatu kwa ajili ya mipango mingine; visa na kuomba ruhusa kwa Katibu Mkuu Kiongozi (serikali ya tano hii!).

Kwa ile hamu niliyokuwa nayo wala sikuweza kubaki tena ofisini nikajiondoa kuelekea mnazi mmoja maana nilijua hilo sio suala gumu. Nilishazoea kibongobongo hakuna kufanya vipimo na kwa kuwa nilishaulizia kuhusu visa za Uingerea nilifahamu huwa hawafanyi vipimo vya afya vingine zaidi ya kile kilichoandikwa kwenye ile fomu. Hivyo niliamini wala lile zoezi lisingechukua zaidi ya nusu saa. Niliingia kwenye ATM ya bwana Kimei pale posta nikachukua fedha ya kutosha kwa ajili ya kumshukuru daktari atakayenisainia fomu zangu.

Nilimkuta mmama mmoja!dah nikamsalimia na kumueleza kilichonipeleka pale. Nilishangaa alipochukua kikaratasi chake na kuanza kujaza vipimo ambavyo nilitakiwa kwenda maabara kupima kabla hajanijazia fomu yangu. Nilitamani kuondoka lakini nikakumbuka ameshaichukua fomu yangu na alijua ninataka kuondoka akaiweka kwenye droo na kunikabidhi kile kikaratasi nielekee maabara. Nilijaribu kumuomba kwamba nimetoroka kazini anisainie tu na kupiga muhiri nami ningemshukuru vizuri tu. Alikataa na kunitaka niende kupima.

Niliondoka huku nikisoma kile kikaratasi ila nilipofika kwenye hili neno PITC nikashtuka kidogo. Ufadhili (scholarship) nautaka na vipimo sivitaki nifanyeje sasa, ikanibidi nielekee maabara. Nikaelekezwa kwenye dirisha la kulipia nikalipa (nilisahau kabisa kwamba nina bima ya afya hiyo jana). Nikarudi kwenye kiti changu kusubiri wakati wangu wa kuitwa.

Palikuwa na makelele na kulikuwa na nesi mmoja anaita watu majina. Namkumbuka kwa kuwa alikuwa na sauti kubwa kuliko mwili wake.

MAGRETH! MAGRETH!” aliita kwa nguvu. –kimya

Akaendelea kuita jina lingine, “JACKLINE!” “JACKLINE!

Mh! Haya majina mawili kwa pamoja yakanikumbusha Changanyikeni.

Sikumbuki siku kamili!

Nilikuwa na rafiki yangu tuliyeshibana sana toka utotoni, Arnold. Huyu jamaa ndiye aliyenifundisha ule msemo wa KUPATA UKIMWI MPAKA UWE UMELOGWA. Nami niliuamini maana michezo niliyoicheza ujanani tena pekupeku sikuwa nimeathirika, kweli mpaka uathirike ni lazima ulogwe.

Ndiyo, kuna nyakati nilijua sijaathirika kabisa kwa kuwa mara nyingi mabinti niliokuwa nao kwenye mahusiano walikuwa wakiniambia. Nakumbuka huyu mmoja ambaye alinifuma nikiwa choo cha klabu na mwanamke mwingine ambaye hata jina sikuwa nikimfahamu. Alinikuta nikifanya naye mapenzi pasi na kinga. Nilikuwa nimeshazoea.

Huyu ndo alinifumbua macho siku moja miezi michache baada ya kuachana nami kuwa kitu cha kwanza alichoenda kufanya baada ya usiku ule ni kwenda kupima ambapo alipojikuta hakuathirika alishukuru sana. Ndipo nami nikagundua kumbe sikuathirika. Niliifanya kama mchezo kwamba kila binti niliyeachana naye; kumuacha au mara nyingi yeye kuniacha, baada ya miezi michache nitamuuliza kama amepima na mara ningi huniambia wako poa. Nami hujua niko vizuri.

Ah! Jacky na Mage

Nakumbuka ilikuwa siku niliyotoka ubalozi wa Uingereza ambapo niliambiwa nimepita usaili na nijiandae tu kwa ajili ya mitihani ya kiingereza. Baada ya kufanya utafiti mfupi niligundua mitihani ile si migumu na kwa watu wote tuliopita usaili mimi nisingeweza kukosa ufadhili ule kwa kamtihani kale karahisi ka kiingereza.

Nilimpigia simu Arnold na kumuambia tukasherehekee. Tulienda Samaki samaki ambapo tulikutana na Jacky na Mage, tulisoma nao o-level huko Moshi. Tulipiga stori sana na kwa kuwa nilikuwa nasherehekea mimi ndo nilikuwa mnunuzi. Walikunywa vya kutosha kiasi kwamba wakati wa kuondoka wale mabinti hawakuweza kwenda peke yao. Ilikuwa kazi rahisi sana kuwashawishi twende kwangu Changanyikeni kwa kuwa pia ilikuwa ni siku ya Ijumaa. Tuliingia kwenye kausafiri changu hao mpaka Changanyikeni. Safari moja ikapelekea nyingine na yaliyotokea kule – sijivunii – na sitayaelezea na hatukuwa na kinga yoyote. Na wala siwezi kusingizia ulevi maana mimi huwa situmii kilevi chochote.

Mentor! Mentor!”

Sauti ya nesi yule ikiniita ilinishtua kutoka kwenye dimbwi la mawazo. Ulikuwa ni wakati wangu kwenda kwenye vipimo.

Nilinyanyuka na kuelekezwa kwenye chumba kingine ambapo nilipoingia sikukuta hata dalili za sindano. Kumbe ilikuwa kwa ajili ya vipimo vingine vilivyokuwa kwenye karatasi ile. Nilipima uzito, urefu, pressure, na mengine kama hayo kisha nesi akaniambia nirudi kukaa kwenye benchi.

Hapo akili yangu ikaniambia kuwa kinachofuata sasa ni ukimwi. Nilikaa nikitafakari kama kweli ninaweza kuwa nimeathirika. Akili yangu ikakataa.

Usiku wa Mwaka mpya 2016

Najua wengi mnaonifahamu hamtaamini mkisoma hapa – MNISAMEHE! Wengi walinifahamu kama kijana Mkristo safi ninayeenda kanisani kila Jumapili. Hata kanisani kwangu ni mmoja wa viongozi wa vijana – nafasi ambayo niliitumia vibaya kuendeleza tabia yangu mbaya chini ya kapeti.

Nilienda kwenye mkesha wa mwaka mpya. Tuliimba na kusherehekea sana na moyoni mwangu nilijiwekea malengo kuwa mwaka huu mpya nimtafute binti mmoja nitakayempenda na kutulia naye maana umri nao haunisubiri.

Nilidhamiria kupunguza kwa kiasi kikubwa tabia zangu mbaya hasa ukizingatia mema mengi ambayo Mungu amekuwa akinifanyia bila kustahili kwangu. Ni katika kuwaza huku ndipo macho yangu yalipodondoka juu ya msharika mmoja. Hadi wakati tunatoka ibada usiku ule tulikuwa tumeshafahamiana vya kutosha.

Itoshe kusema tu kuwa hatukufanikiwa kwenda kwenye ibada asubuhi ya tarehe 01/01/2016 kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu. Na hatukutumia kinga. Ni katika kuwaza huku ndipo nilipokumbuka kuwa juzi juzi tu alikuwa akiumwa na hakutaka kuniambia anaugua nini. “Atakuwa ameathirika?” nilijiuliza. Lakini nikajifariji kuwa KUPATA UKIMWI NI HADI ULOGWE. Ni nani wa kuniloga mimi Mentor, mtu wa watu, kwa kosa lipi nililomfanyia?

Jina langu lilitwa tena na kwenda kwa ajili ya vipimo vingine vilivyohusisha damu kuchukuliwa.

Nilitamani kuondoka pale kwani sikuwa nimeomba ruhusa ofisini lakini pia nilitakiwa kuondoka na fomu zile. Ilinibidi kusubiria.

Akili yangu ilikuwa ikisafiri mbali. Nilijiuliza maswali mengi kuhusu afya yangu ambayo sikuwa nimewahi kujiuliza kabla. Nilifanya mambo yangu mengi kwa siri kiasi kwamba ni vigumu mtu yeyote akihadithiwa haya kuyaamini. Lakini kwani UKIMWI unawapata waliofanya kwa wazi? Lakini hapana mimi siwezi kuwa nimeathirika. Kutoka kwa nani labda?

Nikamkumbuka Amina, huyu alikuwa mdada wa usafi ofisini. Kama tabia yangu nimezoea kusalimia kila mtu na huyu dada tulikuwa tukikutana asubuhi wakati naingia ofisini hakukosa salamu yangu.

Pamoja na tabia yangu ya kupenda kuwahi ofisini hakuna siku niliyowahi kwenda ofisini nisikute ameshafika. Tukazoeana sana. Nami kidogo kidogo nikaanza kumzoea na kumchokoza kwa vimaneno vya hapa na pale.

Kuna zile siku unaamka mapema, unajisikia vizuri, unaoga unavaa unaingia kwenye gari unaondoka kwenda kazini mapema ukitegemea kutakuwa na foleni kubwa kumbe unapofika barabarani unatumia robo saa tu kufika ofisini. Hii siku ilikuwa hivyo. Na nilipofika saa kumi na mbili kasoro bado nilikuta Amina amekwishafika. Na kwa bahati zaidi alikuwa akifanya usafi ofisini kwangu. Sitaki kuelezea zaidi lakini itoshe kusema usafi uliishia palepale. Na hatukutumia kinga. Baadaye Amina alikuja kuzushiwa maneno kuwa anatembea na mabosi wangu wengine na eti ameathirika hivyo akafukuzwa na sikumuona tena. Sikuweza kumuuliza kama alipima au la!

Lakini hapana, wakati ninakutana na Amina nilikuwa na rafiki wa kike, Hamida, na Hamida tulipoachana alienda kupima na hakukutwa na virusi. Nilitabasamu kugundua kuwa niko vizuri.

Lindi hili la mawazo lilikatishwa tena na nesi yule yule aliyeniita nyakati zilizopita. Niliangalia saa yangu iliyonionesha kuwa ni saa mbili zimepita tangu nifike pale.

Niliingia kwenye chumba ambacho nilijua tu ni kwa ajili ya ushauri. Nilimwomba nesi aniandikie majibu yangu kwenye kile kikaratasi pamoja na yale majibu mengine niwahi kwa daktari maana natakiwa kurudi ofisini. *sasa ndio naelewa* maana aliniangalia kwa huruma sana huku akivikusanya vikaratasi vile na kuondoka navyo huku akiniambia nisubiri. Alienda kumuita yule daktari aliyeniandikia vipimo.

Jumamosi, 25 Juni 2016

Nimeikatisha ndoto yangu mwenyewe kwa umalaya wangu. Nakumbuka siku ya usaili yule mzungu aliangalia fomu zangu baada ya kunisikiliza na kusoma insha zangu aliniambia, “Young man! If what you have written and have just told us comes from your heart, then I wish you all the best.

Nimeikatisha ndoto yangu kwa kuishi maisha mawili. Nakosa hata ujasiri wa kutubu kwa Mungu. Nakosa ujasiri wa kwenda kanisani kesho. Ni nani aliyeniloga?

Pamoja na kupewa ushauri mwingi jana, nimeamua sitokunywa dawa! Nipo tayari kutumikia adhabu niliyojitakia.

Nilirudi ofisini na kujifanya kama hakuna kilichotokea. Baadaye jioni nilijilazimisha kwenda kuangalia filamu pale LAPF Tower (Movie Night) na kwa maumivu makubwa filamu ile ilikuja wakati wa kuchelewa sana maishani mwangu. Inaitwa ‘God’s Compass’. Baada ya kutoka na kuagana na walionialika tena tofauti na siku zote nilikataa kuwapa lift kwenye gari langu na kuwalazimu wajazane wote kwenye gari lingine la mwenzao na kurudi makwao. Nilirudi kwenye gari langu ambapo nilikaa kwa zaidi ya lisaa limoja pale nikilia jinsi maisha yangu yalivyofikia mwisho haraka.

Nimejitahidi kujifanya kama kila kitu kiko sawa kwenye maisha yangu lakini nimeshindwa, nimeishia kulia machozi siku nzima ya leo. Kwa nini Mungu ameruhusu hili linitokee mimi? Kwa nini asingeninyima scholarship na kunipa afya yangu, ningejilipia mwenyewe. Nilikuwa nimeshapanga kuwa kama ningekosa scholarship ningeenda kujilipia pale IFM nisome masomo ya jioni na kwa hakika ningemaliza Masters yangu.

Hii inaweza kuwa hadithi yangu ya mwisho – sikutaraji ingekuwa hii ndiyo hadithi yangu ya mwisho, na iwe ni ya kweli! Lakini niwaombe wote msamaha. Sikuwahi kuamini kama nami ningekuja kuathirika, walikuwa na afya zao, hawakuonekana wameathirika.

Kwa wadada wote mtakaopima na kukutwa mmeathirika kwa sababu yangu – MNISAMEHE.

Wapendwa, hiki ni kisa changu cha ukweli na ndio maana nimetaja baadhi ya vitu/sehemu za ukweli ili walau muone uhalisia. Kama yote niliyowahi kuyaandika humu yatakosa maana kutokana na nilichokifanya basi naombeni neno langu la mwisho mlizingatie…UKIMWI UPO, NAMI MENTOR NIMEATHIRIKA.

Tafadhali msifuate mfano wangu.

Wasalaam na kwaherini,

Mentor.
 
inatia uchungu! lakini usikate tamaa, kuna watu wengi wanao na wameoa na kuolewa nakuwa na watoto, kuna dada mmoja anao sasa ni mwaka wa 25 na ana afya yake nzuri sana. my friend kukata tamaa ni mwiko kabisa!
MWENYE ENZI MUNGU akupe amani na nguvu ya kuishi kijasiri!
 
pole sana. Unajua watu weng wanafanya makosa ambayo yanawaharibia maisha yao lkn hawaon hilo wanachukulia kawaida. Yakishawatokea puani wanaanza kumlalamikia Mungu. Kwann Mungu wetu tunambebesha lawama tunapokesea? Kbla haujaathirika ukiambiwa unasema shetani alinipitia ila ukipata lawama zote kwa Mungu. Kwann tunamkosea sana Mungu?
Naomba usimbebeshe Mungu lawama hana makosa.
Nenda kanisani uongozwe sala ya toba, umrudie muumba wako. Kisha anza kutumia dawa.
Ukimwi upo lkn watu weng hawalitambui hili mpaka waathirike ndio wanalitambua.
Inashangaza sana tendo la dk 30 linakuharibia maisha.
Unajua km unapenda ngono, oa tu ndio dawa lkn kila mtu unataka kumpalamia, utakuja uumie.
Ona sasa unakufa papuchi unaziacha na watu wanaendelea kula.
Aise dunia hii hebu tutulie HIV KILLS
 
samahani, lakini ilibidi nicheke walahi!
 
SITAKI DAWA

Jumamosi, 25/06/2016

Nawaza nianzie wapi kuelezea kilichonikuta nashindwa, lakini hasa ni kukosa maneno ya kukielezea. Nimetamani nikae kimya, nisiseme, maana ninafahamika na wengi na itaniharibia picha yangu kwenye jamii. Nimetafakari sana kuchukua maamuzi magumu lakini nfasi yangu haikuumbwa hivo, nimeshindwa. Labda ningezaliwa Mhehe, lakini mchagga mimi hata vidonge vya piriton vilikuwa shida kumeza.

Lakini nimeamua nitasema. Sijui baada ya kusema nini kitatokea, sijui jamii itanichukuliaje, ndugu jamaa na marafiki watasemaje au labda watanitenga…lakini nitasema.

Wazazi wangu – MNISAMEHE! Zaidi ya yeyote yule nimewaangusha. Mlikuwa na mategemeo makubwa juu yangu. Mmenisomesha kwa gharama kubwa na mlikuwa na matumaini ya mimi kufika mbali.

Mlioniita Mentor – MNISAMEHE! Najua ni wengi walioniona kama kijana wa mfano, kaka na ndugu…mnisamehe kwa kuwaangusha. Sitamsingizia shetani wala mtu mwingine yeyote kwa kosa langu.

NIMEATHIRIKA! Na sijivunii…

July, 2015

Naamini ni wakati huu. Kulitangazwa nafasi za masomo nchini Uingereza chini ya ufadhili wa Commonwealth (Common wealth Scholarships 2015). Nami nilikuwa nimejiwekea malengo kuwa hadi mwaka 2016 ni lazima nikasome masomo yangu ya Uzamili (masters) hata ikibidi kwa kujilipia. Nilitembelea tovuti tofauti tofauti nikitafuta ufadhili kwa ajili ya masomo yangu. Hakuna tangazo lililotolewa ambalo sikuliomba. Fulbright, Mwalimu Nyerere, DAAD, World Bank, IMF, n.k n.k niliomba zote. Nilikuwa na malengo ya kwenda kusoma masomo ya usimamizi wa miradi au utungaji sera. Ndoto yangu ilikuwa moja tu: SIKU MOJA NIWE KATI YA WAFANYA MAAMUZI KATIKA NCHI HII.

Nilichoka kuwa mtu wa kuandika programs kila siku halafu aidha fedha zinaliwa au miradi inawekwa kwenye shelfu. Nilichoka kuhusishwa kwenye miradi isiyo na kichwa na miguu, miradi isiyoangalia vipaumbele vya taasisi au nchi. Nilichoka! Nikasema nitaachana na masomo yangu ya sayansi ya kompyuta nikasome masomo yatakayonifanya niwe mtunga sera na mtoa maamuzi. **** ME!!!! (mnisamehe am so mad at me)

Wakati huu ndipo kulipotangazwa nafasi hii ya Commonwealth. Nakumbuka nililiona tangazo kupitia tovuti ya TCU na ilikuwa imebaki wiki moja au mbili hivi kabla ya tarehe ya mwisho kwa hapa kwetu. Nilijipinda ofisini kuandika insha kama tatu kuelezea kwa nini mimi niipate nafasi hii na si mwingine. Niliandika kutoka moyoni. Nilifanikiwa kumaliza mapema nikatoa nakala kama walivyoelekeza; za kupeleka wizara ya elimu na za kutuma kwa barua pepe.

Siku, wiki na miezi vilipita nami nikaitwa kwenye usaili, nikaenda kufanya mitihani ya Kiingereza ya IELTS pale ubalozi wa Uingereza, nikafaulu vizuri.

Alhamisi, 23 Juni 2016 - Juzi

Nilipewa majibu kuwa nimechaguliwa pamoja na wenzangu wawili kwenda Uingereza (chuo sitokitaja) kwa ajili ya masomo ya Uzamili katika Usimamizi wa Miradi kuanzia mwezi wa tisa. Nilifurahi sana, nikapiga magoti ofisini nikamshukuru Mungu kuwa mwaminifu kwangu. Nilimuomba mwaka huu niende shule na amenijibu. Tena kaniongezea baraka kwa kuwa ninapewa ufadhili wa 100%. Hakuna hata senti yangu nitakayotumia katika maosomo yangu hayo.

Jana asubuhi nilitumiwa mkataba wangu pamoja na fomu za afya ambazo nilitakiwa kuzijaza na kuzirudisha ubalozi wao Jumatatu kwa ajili ya mipango mingine; visa na kuomba ruhusa kwa Katibu Mkuu Kiongozi (serikali ya tano hii!)

Kwa ile hamu niliyokuwa nayo wala sikuweza kubaki tena ofisini nikajiondoa kuelekea mnazi mmoja maana nilijua hilo sio suala gumu. Nilishazoea kibongobongo hakuna kufanya vipimo na kwa kuwa nilishaulizia kuhusu visa za Uingerea nilifahamu huwa hawafanyi vipimo vya afya vingine zaidi ya kile kilichoandikwa kwenye ile fomu. Hivyo niliamini wala lile zoezi lisingechukua zaidi ya nusu saa. Niliingia kwenye ATM ya bwana Kimei pale posta nikachukua fedha ya kutosha kwa ajili ya kumshukuru daktari atakayenisainia fomu zangu.

Nilimkuta mmama mmoja!dah nikamsalimia na kumueleza kilichonipeleka pale. Nilishangaa alipochukua kikaratasi chake na kuanza kujaza vipimo ambavyo nilitakiwa kwenda maabara kupima kabla hajanijazia fomu yangu. Nilitamani kuondoka lakini nikakumbuka ameshaichukua fomu yangu na alijua ninataka kuondoka akaiweka kwenye droo na kunikabidhi kile kikaratasi nielekee maabara. Nilijaribu kumuomba kwamba nimetoroka kazini anisainie tu na kupiga muhiri nami ningemshukuru vizuri tu. Alikataa na kunitaka niende kupima.

Niliondoka huku nikisoma kile kikaratasi ila nilipofika kwenye hili neno PITC nikashtuka kidogo. Ufadhili (scholarship) nautaka na vipimo sivitaki nifanyeje sasa, ikanibidi nielekee maabara. Nikaelekezwa kwenye dirisha la kulipia nikalipa (nilisahau kabisa kwamba nina bima ya afya hiyo jana). Nikarudi kwenye kiti changu kusubiri wakati wangu wa kuitwa.

Palikuwa na makelele na kulikuwa na nesi mmoja anaita watu majina. Namkumbuka kwa kuwa alikuwa na sauti kubwa kuliko mwili wake.

MAGRETH! MAGRETH!” aliita kwa nguvu. –kimya

Akaendelea kuita jina lingine, “JACKLINE!” “JACKLINE!

Mh! Haya majina mawili kwa pamoja yakanikumbusha Changanyikeni.

Sikumbuki siku kamili!

Nilikuwa na rafiki yangu tuliyeshibana sana toka utotoni, Arnold. Huyu jamaa ndiye aliyenifundisha ule msemo wa KUPATA UKIMWI MPAKA UWE UMELOGWA. Nami niliuamini maana michezo niliyoicheza ujanani tena pekupeku sikuwa nimeathirika, kweli mpaka uathirike ni lazima ulogwe.

Ndiyo, kuna nyakati nilijua sijaathirika kabisa kwa kuwa mara nyingi mabinti niliokuwa nao kwenye mahusiano walikuwa wakiniambia. Nakumbuka huyu mmoja ambaye alinifuma nikiwa choo cha klabu na mwanamke mwingine ambaye hata jina sikuwa nikimfahamu. Alinikuta nikifanya naye mapenzi pasi na kinga. Nilikuwa nimeshazoea.

Huyu ndo alinifumbua macho siku moja miezi michache baada ya kuachana nami kuwa kitu cha kwanza alichoenda kufanya baada ya usiku ule ni kwenda kupima ambapo alipojikuta hakuathirika alishukuru sana. Ndipo nami nikagundua kumbe sikuathirika. Niliifanya kama mchezo kwamba kila binti niliyeachana naye; kumuacha au mara nyingi yeye kuniacha, baada ya miezi michache nitamuuliza kama amepima na mara ningi huniambia wako poa. Nami hujua niko vizuri.

Ah! Jacky na Mage

Nakumbuka ilikuwa siku niliyotoka ubalozi wa Uingereza ambapo niliambiwa nimepita usaili na nijiandae tu kwa ajili ya mitihani ya kiingereza. Baada ya kufanya utafiti mfupi niligundua mitihani ile si migumu na kwa watu wote tuliopita usaili mimi nisingeweza kukosa ufadhili ule kwa kamtihani kale karahisi ka kiingereza.

Nilimpigia simu Arnold na kumuambia tukasherehekee. Tulienda Samaki samaki ambapo tulikutana na Jacky na Mage, tulisoma nao o-level huko Moshi. Tulipiga stori sana na kwa kuwa nilikuwa nasherehekea mimi ndo nilikuwa mnunuzi. Walikunywa vya kutosha kiasi kwamba wakati wa kuondoka wale mabinti hawakuweza kwenda peke yao. Ilikuwa kazi rahisi sana kuwashawishi twende kwangu Changanyikeni kwa kuwa pia ilikuwa ni siku ya Ijumaa. Tuliingia kwenye kausafiri changu hao mpaka Changanyikeni. Safari moja ikapelekea nyingine na yaliyotokea kule – sijivunii – na sitayaelezea na hatukuwa na kinga yoyote. Na wala siwezi kusingizia ulevi maana mimi huwa situmii kilevi chochote.

Mentor! Mentor!”

Sauti ya nesi yule ikiniita ilinishtua kutoka kwenye dimbwi la mawazo. Ulikuwa ni wakati wangu kwenda kwenye vipimo.

Nilinyanyuka na kuelekezwa kwenye chumba kingine ambapo nilipoingia sikukuta hata dalili za sindano. Kumbe ilikuwa kwa ajili ya vipimo vingine vilivyokuwa kwenye karatasi ile. Nilipima uzito, urefu, pressure, na mengine kama hayo kisha nesi akaniambia nirudi kukaa kwenye benchi.

Hapo akili yangu ikaniambia kuwa kinachofuata sasa ni ukimwi. Nilikaa nikitafakari kama kweli ninaweza kuwa nimeathirika. Akili yangu ikakataa.

Usiku wa Mwaka mpya 2016

Najua wengi mnaonifahamu hamtaamini mkisoma hapa – MNISAMEHE! Wengi walinifahamu kama kijana Mkristo safi ninayeenda kanisani kila Jumapili. Hata kanisani kwangu ni mmoja wa viongozi wa vijana – nafasi ambayo niliitumia vibaya kuendeleza tabia yangu mbaya chini ya kapeti.

Nilienda kwenye mkesha wa mwaka mpya. Tuliimba na kusherehekea sana na moyoni mwangu nilijiwekea malengo kuwa mwaka huu mpya nimtafute binti mmoja nitakayempenda na kutulia naye maana umri nao haunisubiri.

Nilidhamiria kupunguza kwa kiasi kikubwa tabia zangu mbaya hasa ukizingatia mema mengi ambayo Mungu amekuwa akinifanyia bila kustahili kwangu. Ni katika kuwaza huku ndipo macho yangu yalipodondoka juu ya msharika mmoja. Hadi wakati tunatoka ibada usiku ule tulikuwa tumeshafahamiana vya kutosha.

Itoshe kusema tu kuwa hatukufanikiwa kwenda kwenye ibada asubuhi ya tarehe 01/01/2016 kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu. Na hatukutumia kinga. Ni katika kuwaza huku ndipo nilipokumbuka kuwa juzi juzi tu alikuwa akiumwa na hakutaka kuniambia anaugua nini. “Atakuwa ameathirika?” nilijiuliza. Lakini nikajifariji kuwa KUPATA UKIMWI NI HADI ULOGWE. Ni nani wa kuniloga mimi Mentor, mtu wa watu, kwa kosa lipi nililomfanyia?

Jina langu lilitwa tena na kwenda kwa ajili ya vipimo vingine vilivyohusisha damu kuchukuliwa.

Nilitamani kuondoka pale kwani sikuwa nimeomba ruhusa ofisini lakini pia nilitakiwa kuondoka na fomu zile. Ilinibidi kusubiria.

Akili yangu ilikuwa ikisafiri mbali. Nilijiuliza maswali mengi kuhusu afya yangu ambayo sikuwa nimewahi kujiuliza kabla. Nilifanya mambo yangu mengi kwa siri kiasi kwamba ni vigumu mtu yeyote akihadithiwa haya kuyaamini. Lakini kwani UKIMWI unawapata waliofanya kwa wazi? Lakini hapana mimi siwezi kuwa nimeathirika. Kutoka kwa nani labda?

Nikamkumbuka Amina, huyu alikuwa mdada wa usafi ofisini. Kama tabia yangu nimezoea kusalimia kila mtu na huyu dada tulikuwa tukikutana asubuhi wakati naingia ofisini hakukosa salamu yangu.

Pamoja na tabia yangu ya kupenda kuwahi ofisini hakuna siku niliyowahi kwenda ofisini nisikute ameshafika. Tukazoeana sana. Nami kidogo kidogo nikaanza kumzoea na kumchokoza kwa vimaneno vya hapa na pale.

Kuna zile siku unaamka mapema, unajisikia vizuri, unaoga unavaa unaingia kwenye gari unaondoka kwenda kazini mapema ukitegemea kutakuwa na foleni kubwa kumbe unapofika barabarani unatumia robo saa tu kufika ofisini. Hii siku ilikuwa hivyo. Na nilipofika saa kumi na mbili kasoro bado nilikuta Amina amekwishafika. Na kwa bahati zaidi alikuwa akifanya usafi ofisini kwangu. Sitaki kuelezea zaidi lakini itoshe kusema usafi uliishia palepale. Na hatukutumia kinga. Baadaye Amina alikuja kuzushiwa maneno kuwa anatembea na mabosi wangu wengine na eti ameathirika hivyo akafukuzwa na sikumuona tena. Sikuweza kumuuliza kama alipima au la!

Lakini hapana, wakati ninakutana na Amina nilikuwa na rafiki wa kike, Hamida, na Hamida tulipoachana alienda kupima na hakukutwa na virusi. Nilitabasamu kugundua kuwa niko vizuri.

Lindi hili la mawazo lilikatishwa tena na nesi yule yule aliyeniita nyakati zilizopita. Niliangalia saa yangu iliyonionesha kuwa ni saa mbili zimepita tangu nifike pale.

Niliingia kwenye chumba ambacho nilijua tu ni kwa ajili ya ushauri. Nilimwomba nesi aniandikie majibu yangu kwenye kile kikaratasi pamoja na yale majibu mengine niwahi kwa daktari maana natakiwa kurudi ofisini. *sasa ndio naelewa* maana aliniangalia kwa huruma sana huku akivikusanya vikaratasi vile na kuondoka navyo huku akiniambia nisubiri. Alienda kumuita yule daktari aliyeniandikia vipimo.

Jumamosi, 25 Juni 2016

Nimeikatisha ndoto yangu mwenyewe kwa umalaya wangu. Nakumbuka siku ya usaili yule mzungu aliangalia fomu zangu baada ya kunisikiliza na kusoma insha zangu aliniambia, “Young man! If what you have written and have just told us comes from your heart, then I wish you all the best.

Nimeikatisha ndoto yangu kwa kuishi maisha mawili. Nakosa hata ujasiri wa kutubu kwa Mungu. Nakosa ujasiri wa kwenda kanisani kesho. Ni nani aliyeniloga?

Pamoja na kupewa ushauri mwingi jana, nimeamua sitokunywa dawa! Nipo tayari kutumikia adhabu niliyojitakia.

Nilirudi ofisini na kujifanya kama hakuna kilichotokea. Baadaye jioni nilijilazimisha kwenda kuangalia filamu pale LAPF Tower (Movie Night) na kwa maumivu makubwa filamu ile ilikuja wakati wa kuchelewa sana maishani mwangu. Inaitwa ‘God’s Compass’. Baada ya kutoka na kuagana na walionialika tena tofauti na siku zote nilikataa kuwapa lift kwenye gari langu na kuwalazimu wajazane wote kwenye gari lingine la mwenzao na kurudi makwao. Nilirudi kwenye gari langu ambapo nilikaa kwa zaidi ya lisaa limoja pale nikilia jinsi maisha yangu yalivyofikia mwisho haraka.

Nimejitahidi kujifanya kama kila kitu kiko sawa kwenye maisha yangu lakini nimeshindwa, nimeishia kulia machozi siku nzima ya leo. Kwa nini Mungu ameruhusu hili linitokee mimi? Kwa nini asingeninyima scholarship na kunipa afya yangu, ningejilipia mwenyewe. Nilikuwa nimeshapanga kuwa kama ningekosa scholarship ningeenda kujilipia pale IFM nisome masomo ya jioni na kwa hakika ningemaliza Masters yangu.

Hii inaweza kuwa hadithi yangu ya mwisho – sikutaraji ingekuwa hii ndiyo hadithi yangu ya mwisho, na iwe ni ya kweli! Lakini niwaombe wote msamaha. Sikuwahi kuamini kama nami ningekuja kuathirika, walikuwa na afya zao, hawakuonekana wameathirika.

Kwa wadada wote mtakaopima na kukutwa mmeathirika kwa sababu yangu – MNISAMEHE.

Wapendwa, hiki ni kisa changu cha ukweli na ndio maana nimetaja baadhi ya vitu/sehemu za ukweli ili walau muone uhalisia. Kama yote niliyowahi kuyaandika humu yatakosa maana kutokana na nilichokifanya basi naombeni neno langu la mwisho mlizingatie…UKIMWI UPO, NAMI MENTOR NIMEATHIRIKA.

Tafadhali msifuate mfano wangu.

Wasalaam na kwaherini,

Mentor.
Tafuta pesa nipate kukutibia hayo maradhi yako ya Ukimwi na utapona kwa muda wa miezi 7 .
kwa Mawasiliano MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App +905344508169 Au Ni add Kwa Facebook tumia jina hili mzizimkavu. Au boonyeza hapa.Mzizi Mkavu
 
I AM SORRY TANZANIA..I AM SORRY GUYS!

I AM SORRY JF AND ALL WHO CALLED ME MENTOR.

ADIOS...

Kama hadithi uliyoleta ni kweli ilitokea kwako,basi nakushauri yafuatayo;

1.Unaoekana kuwa na uelewa wa mambo mengine lakini hili la HIV/AIDS(ambalo ni feki) hulijui,hivyo utayari wako wa kufuatilia ili kujua kwanini na kwa vipi HIV/AIDS ni feki ndio utakaokuokoa.HIV/AIDS ni feki na ndio maana kuna watu wengi wana claim kuwa na dawa na wana claim kuponesha watu,na ni kweli wapo watu wengi waliopima HIV+ halafu wakaja kupima HIV- baadaye,haya yote hutokea kwa kuwa HIV/AIDS ni feki.HIV/AIDS is not real,but rather it is a MINDSET disease.

2.Endelea kufuata uamuzi wako wa kutokunywa ARVs kwa kuwa ARVs ndio kitanzi na ndio zinazosababisha vifo kwa wale wanaozitumia baada ya muda mrefu,kama hutumii ARVs hutakufa kwa hiko kitu kinachoitwa 'HIV'(ambacho ni feki).Matatizo yote unayoyaona kwa wale ambao umeambiwa wameathirika na wanatumia ARVs yamesababishwa na ARVs,kama mtu hatumii ARVs lakini anaumwa,basi lazima ukimpima utamkuta na ugonjwa unaofahamika ambao unatibibika kabisa kama atapewa matibabu mapema,mfano TB,pia ugonjwa huo unampata mtu yeyote bila kujali kama amepimwa HIV+ au HIV-.Nywele kudhoofika/kunyonyoka,ngozi kufubaa/kutoka vipele/vidonda,ini kufeli,figo kufeli,ugonjwa wa moyo,upungufu wa damu,cancer yoyote na kisukari ni baadhi ya matatizo makubwa yanayowaua wale wanaotumia ARVs,wale wasiotumia ARVs huwezi kuwakuta na matatizo haya hata kama wamepimwa HIV+ na hawajatumia ARVs kwa zaidi ya miaka 40(ie their lifetime).Hapa unatakiwa kujua kwamba ARVs ndio mambo yote,HIV ni scaring tactic tu.Unajengewa woga uogope HIV then unajengewa MINDSET ya kukimbilia kula ARVs ambazo ndizo zitakazokuua,pharmaceutical tycoons have made a very simple trick to grab our minds.

3.Kitu kingine ambacho ni kibaya sana ni kwamba,watu wengi wakishapima na kuambiwa ni HIV+,baaaasi,ndio wamemaliza,hawapimi tena katika maisha yao kwa kuwa tayari kwenye bongo zao kuna kale ka mindset kwamba ukishakuwa na HIV ndio baasi,eti HIV hatoki mwilini mpaka kifo kitakapokukuta.Lakini hawajui kwamba kinachopimwa na kipimo SI HIV,bali vipimo hupima vitu 'VINGINE' kabisa tofauti na HIV,and infact vipimo havipimi kijidudu chochote kile kwa muonekano.Hivi vitu ambavyo naviita 'VINGINE' huweza kuwepo kwenye damu ya mtu yeyote yule(hata Obama au Bush) bila kujali kama kwenye damu kuna vijidudu vyovyote au la.Na ndio maana leo hii ukimuuliza daktari yeyote yule unayemjua kama ameshawahi kuona HIV hata kwa kutumia chombo chochote cha maabara,atakwambia "sijawahi",sasa kama hajawahi kuona HIV kwa macho yake anaamini nini?anapima nini?wamejuaje kama HIV ndio husababisha UKIMWI?Hivyo kama utakuwa tayari nitakushauri jambo la kufanya halafu uende kupima tena mara kwa mara mpaka upata majibu HIV- then uje tena hapa uwe shuhuda kwa wengine,sitahitaji chochote kutoka kwako,hii ni kwasababu ninajua hiki ninachokisema ni ukweli mtupu,sibahatishi.

4.Fahamu pia kwamba MINDSET ndio inayofanya watu washindwe kutofautisha kati ya HIV(ambaye ni feki pia) na UKIMWI(ambao upo lakini hauui).HIV hayupo kiuhalisia,UKIMWI upo lakini SI ugonjwa na hauui.Ukimwi si kitu cha kuogopa kwa kuwa hauui na UKIMWI hausababishwi na HIV(Feki),kila mtu anaweza kupata ukimwi na ukimwi huondoka wenyewe mwilini kama mtu utabadili style ya maisha iliyokufanya uwe na upungufu wa kinga.Akili ni kitu cha ajabu sana,yaani ukisema IKIMWI watu wanaogopa sana,lakini ukisema upungufu wa kinga watu hawashtuki wala kuogopa,watu hawana hisia kwamba UKIMWI ndio upungufu wa kinga,hii inatokana na MINDSET mbovu zilizojengeka kwa zaidi ya miaka 30 baada ya kampeni nzitonzito zilizoambatana na movie zenye vitisho za 'eti ukimwi' na matangazo redioni na kwenye TV,kampeni hizi zimefanikiwa kupenyeza IMANI(na si FACT) kwenye vichwa vya watu ambazo zimedumu hadi leo hii.

NB:
Sitakushauri chochote mpaka pale utakapoonesha utayari,nisingependa kupoteza muda wangu bure kwa mtu aliyegubikwa na MINDSET mbaya.Mtu anayeongozwa na MINDSET mbaya kama hizi za HIV/AIDS huwa ni vigumu sana kuuona ukweli,nina mifano.Hata kama unaeleza FACT, mtu hawezi kuiona hiyo FACT iko wapi,hili ni tatizo kubwa sana.

Habari kama hizi zinapaswa watu wazifurahie kwa kuwa ni habari njema zinazookoa maisha yako na wengine kama utazitujua,lakini kinyume chake watu huishia kudharau na kukebehi tu.Ndio maana nasema hii IMANI tuliyojengewa kwenye HIV/AIDS imetumia akili nyingi sana kiasi cha mtu asiyependa kufikiri kushindwa kung'amua ukweli ulivyo.

Utayari wako wa kusikiliza ndio ukombozi wako kiafya na kifikra hasa kuhusu suala hili.Ninaamini kama ulichoeleza ni kweli na wewe ulikuwa na sifa ya kusoma masters,basi utaelewa hiki ninachosema ingawa hutakuwa na full confidence,full confidence utaipata pale utakapoanza kuruhusu ubongo wako kupokea zaidi ya haya.

HAMNA CHA ADIOS HAPA....
 
Back
Top Bottom