Sitafanya utetezi wa mkataba mbovu kwa nchi yangu kisa mimi ni Muislam

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
1,049
3,084
TUENDELEE KUJADILI MAPUNGUFU YA MKATABA.

Baina ya Tanzania na Dubai wa uwekezaji wa Kampuni ya DPW katika bandari zetu zote.

Tusitolewe kwenye mstari na kukubali Kujadili Udini.

Naomba nitumie muda huu kuwakumbusha Watanzania na watu wengine Duniani kuwa ni jukumu la Muislam kujenga, kuimarisha na kutetea Uislam wake.

Akuna asiye Muislam anaweza kujitoa kwa wajibu wote huo.

Turudi katika mapungufu ya Mkataba na sio Ujenzi wa Uislam kufanywa na Muislam.

Na katika hili sitafanya utetezi wa Mkataba huo Mbovu kwa Nchi yangu kisa mimi ni Muislam.

lakini Sioni tabu Waislam wa DP Wprld kusaidia Uislam na Waislam kwa sababu wao ni Waislam pia.
Watakua wanatimiza wajibu kwa Dini yao.

Waislam wa Tanzania ni Watanzania hivyo kuimarika kwao kwa imani na uchumi wao ni faida kwa Tanzania.

Najua kwa majibu wa mafunzo ya Uislam kuimalika kwa Muislam kwa Elimu yake iliyo bora kuna weza wafanya wasio waislam kujiunga na Dini hiyo kwa kupenda Mira na Desturi za Uislam.

Lakini Wasio waislam hili jambo haliwezi kufikiwa kwa msaada wa DPW bali kwa wito wa Waislam wenyewe walipo Nchini na tupo wote kwenye jamii na mnatuona Waislam wenyewe kama kina SHERKH MWAIPOPO kweli kuna la kukuvutia mpaka uache Dini yako kweli.

Pengine kutolewa kwa Video hii inayo onyesha makubaliano au mkataba wa Ujenzi wa Msikiti wa Ijumaa katika jiji Mbeya dhidi ya DPW na Viongozi wa Uislam huko Mbeya muda huu ni kwa lengo la kuwatoa wasio Waislamu katika msingi wa toka mwanzo kupinga Mkataba mbovu uliopo na sio kwa mtazamo wa Udini.

Hivyo ni waombe msio Waislamu msitoke katika hoja ya msingi ya kupinga Mkataba mbovu na sio kwa sababu uwekezaji huo utawanufaisha Waislamu.

kwa sababu mkataba huo usingekua mbovu sifikiri kusaidiwa Waislamu kungetufanya tupinge kwa chuki ya Udini Mkataba Mzuri.

Hivyo tukifanikiwa vita kupinga huu Mkataba mbovu nafikiri atutapinga Waislamu wa DPW kusaidia Waislamu wenzao waliopo katika Nchi hii na kwengine kokote Duniani.

Kumbukumbu zangu zinasema Waislamu na Uislam wa Nchi hii umepokea misaada mingi kutoka kwa matajiri wa kiislam toka huko Uarabuni na kwengineko lakini akuna cha maana walicho fanya.

Na sote ni mashahidi tumeona Msikiti na MAJENGO ya ofisi yalipo Makao Makuu ya Bakwata ya kijengwa kwa kupigiwa Debe na Rais Magufuli.

Hivyo tatizo sio Waislam kupata misaada tatizo wanaifanyaje hiyo misaada

Hilo mtuachie.

Mwisho tuendelee na jitihada za kukomboa Bandari zetu kutoka katika Mkataba mbovu.

Tuache wajinga wajadili kwa Udini na video hiyo inalengo kututoa katika hoja.

Na usikubali kuingizwa Kujadili Mkataba huo kwa Udini hili wewe ugombane na Ndugu yako.

KATAA MKATABA MBOVU.

King Mwingi Ndugumbi Kitenge.

Fikra Huru.

@⁨~A-Kalikawe⁩
 
Ukiona mtu anajificha kwenye kivuli cha dini au kabila kuunga mkono suala au kupinga huyo ni mtu dhaifu na ameishiwa hoja. Mwl julius kambarage Nyerere
 
SA Kalokola: .....Baada ya kusema hayo, hoja yangu ni kwamba IGA ni Mkataba wa kimataifa uliopitia mchakato wa 63[3]e ya KATIBA

Jaji: kwani issue ilikuaje?

SA Kalokola: issue ilikuwa whether IGA is contract

Jaji: wewe umejibu vipi?

SA Kalokola: IGA is international agreement

Wadau: Miguno kidogo.
 
Kuna majini na mashetani
 
Sheikh mwaipopo ashakutahadharisheni, shaur yako ujue!!
 
Koran 5;51. Enyi mlio amini! (Waislamu) Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki.

Unapingana na Quran?????
 
Kila mtu anayejielewa hawezi kuleta hoja za udini na u-zanzibari/tanganyika kwenye hoja mama ya bandari. Ni distractions za hovyo sana zinafanywa na hawa wanasiasa wapumbavu.
 
NAITWA TWAHIR NI MUISLAM,ILI NIUNGE MKONO MKATABA HUU WA BANDARI, YAFUATAYO YAFANYIKE KWENYE MKATABA MAMA WA IGA

1. Mosi, Indhari zote za TLS zifanyiwe kazi. TLS wamependekeza vifungu viandikwe upya ili kuepuka uwezekano wa "kupigwa" siku zijazo mahakamani.

2. Profesa Shivji kasema mkataba unatoa haki zaidi kwa mwekezaji halafu sisi unatupa wajibu zaidi. Napenda mkataba uwe bayana haki za kila upande na wajibu wake. Siyo kila statement inaanza na The governament of Tanzania will/shaa do this, shall do that.

3. Ukomo wa Muda uwe specific ndani ya Mkataba mama bila kumung'unya maneno, au kuacha utata wa Tafsri. Kiufupi HGA ziwe drafted kutii Time frame itakayowekwa ndani ya mkataba mama na si anything.

4. Mkataba uzungumze bandari moja tu ya Dar es salaam, Usiweke reference ya bandari nyingine yoyote ya kwenye maziwa au baharini au nchi kavu. Yaani hata kwa bahati mbaya usitamke bandari zisizohusu.

5. Ninataka loophole ya Tax exemptions iondoke katika mkataba. Tumeshainvest resources nyingi sana kwenye kujenga hii bandari toka mwaka 1961, Hatuwezi kuafford kumpa exemptions ya kodi bandarini wakati pesa tuliyoinvest haijarudi.

6. Tunataka Ubia kwenye kuendesha hiyo investment hapo bandarini. Share zetu ziwe stipulated very clearly, Tugawane faida. Siyo habari za kodi tu na viushuruushuru vya forodha.

7. Tunataka Nafasi katika management, yaani na sisi tuwemo ndani ya uongozi

8. Kipengele kinachosema kuwa mkataba hauwezi kusitishwa under any circumstances kiondoke. Sisi ni nchi huru tukiona Mkataba unatishia national security au mwekezaji kashindwa kuwa na Tija tumtimue.

9. Tunataka kipengele kinachohusu haki za binadamu, haki za wafanyakazi, na commitment ya kuzuia mambo ya rushwa na magendo, na upitishaji wa nyara za nchi ikiwemo wanyama pori na madini kinyume cha sheria kiwemo ndani ya mkataba.

10. Na kiwemo kipengele cha namna ya kuterminate mkataba, Namna Transfer itakavyofanyika n.k

11. Kiwemo kipengele cha Sehemu ya faida kutunzwa katika mabenki yetu, siyo pesa yote inarudishwa Dubai.

12. Mkataba ueleze kwamba kuhusu pesa zote tulizokopa huko nje kwa ajili ya kuendeleza bandari, Mwekezaji naye achangie kwenye kulipa hilo deni maana ananufaika na miundo mbinu ya hapo na bado tunaendelea kulipa hilo deni.

13. Mkataba ueleze kuwa kwa ajili ya ulinzi na usalama tuwe na haki ya kujua kinachoingia na kupita hapo bandarini, kwa kuwa na haki ya kuinspect chochote.

14. Kuhusu fidia za wananchi walio katika mradi watakaohamishwa kupisha mradi , Itamkwe bayana nani mlipaji , ni serikali au Dubai au DP World?, na fidia iwe Stahiki na ya haraka

15. Mkataba uwe formulated in such a way kwamba Sovereignity ya nchi iko juu, na mkataba uendane na sheria zetu siyo kubadili sheria zetu ziendane na mkataba.

16. Mkataba ueleze kuwa mwekezaji hatofanya matendo ya hila au makusudi au kwa hila kuinyima bandari yetu mzigo na kuupeleka kwa washindani wetu kule ambako kuna bandari anazoziendesha pia.

17. Mkataba ueleze kuwa mwekezaji atatii sheria za nchi yetu, kuheshimu sovereignity yetu awapo nchini na hatotumia ushawishi wake kuingilia shughuli za kisiasa na utawala katika nchi yetu

Mimi hayo yakifanyika, Sina neno na mkataba.

Maoni ya Twahir Kiobya (a.k.a Gamba la Nyoka )
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…