Sista Ulichonifanyia Sikusamehe Mpaka Kiama

STUNTER

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
13,075
17,237
Kuna mademu juzi wamehamia hapa karibu na
nyumbani wazuri vibaya mno nilivyowaona tu
nikasema lazima nimtongoze mmoja
Leo nimetoka zangu kanisani sijaamini macho
yangu nimewakuta wale mademu nyumbani
wamekaa sebuleni wanapiga stori na sister nimefurahi sana nikasema wamejileta wenyewe
lazima nikomae na mmoja hadi kieleweke
Nimeingia fasta gheto nikatupia Sweta langu la
Dume condom nikatupia Pensi yangu ya Turubai
ndani nikavaa boxer yangu ya Chadema chini
nikatupia supra yangu ya ngozi juu kofia yangu ya mkeka kama kawaida na miwani yangu myeusi
mikubwa kama ya wachomelea vyuma
Nikajipulizia na Rungu yangu ili ninunukie
nilivyoona niko fiti nimetokelezea nikajipitisha pale
sebuleni kwa wale mademu na mwendo wangu
wa kunesanesa kama nataka kuanguka Wale mademu walivyoniona wakaanza kucheka
nikajua tayari wameshanishobokea mmoja
akamuuliza sister "huyo ndo mdogo wako?? Sister
akawajibu "ndiyo anaitwa chogo ndizi" mmoja
akamuuliza sister "mbona anaonekana ana vituko
sana ni muigizaji?? Sister akamjibu "hapana sio muigizaji mtundu balaa
anajifanyaga sana sharobaro hapo shule kaacha
hata hatumuelewi kila siku kesi za uwizi hapa
nyumbani mara amebaka yani kesi kibao
usimuone hivyo hapo mikikaa tu vibaya anaweza
akaiba simu zenu na pochi" Sister kaniharibia sana kwa wale mademu
wakabaki tu wananisikitikia huku wananicheka
nimeona sana aibu nikawaambia "nyie warembo
dada anawadanganya anataka tu kuniharibia mimi
hapa mtaani wananiita Criss brown ni msanii wa
Bongo fleva na movie dada anaona akiwaambia ukweli mtaanza kunipenda ndio maana
ananiharibia"
Wale mademu kusikia vile ndo wakazidisha
kicheko hadi wengine wameanguka chini
Sister akanirukia amenikunja ameanza kunipiga
makofi mbele ya wale mademu akaniambia "wewe litoto lipumbavu sana yani ukiniona tu nimekuja na
rafiki zangu hapa nyumbani unaanza misifa hebu
toka hapa wewe utawawezea wapi wanawake
kama hawa wasomi wewe shule hutaki kazi hutaki
umekalia uwizi tu"
Daah sister amenipiga makofi alivyoniachia tu nimetoka nduki balaa peku supra zangu za ngozi
nimeziacha pale pale nimeenda kujificha nimelia
sana sister alivyoamua kuniumbua mbele ya wale
mademu wakati mimi nilikuwa na mpango wa
kumtongoza mmojawao Yani kashaharibu kila kitu
siwezi tena kupita hata pale kwao naogopa wakiniona wataanza kunicheka
 
Sijakusoma siku nyingi, leo nimekusoma naona kweli unaendana na aliyoyasema dada yako na hakutunga.

kumbe upo hivyo, haya kasome ufaulu si unajua bado upo shuleni.
 
Wee hujui,sister ndo kakupaisha
ile mbaya,mwanaume unapigwa vibao
wala hukujibu mapigo?
Nyie ndo mnatafutwa siku hizi.
Jipe moyo,ila hilo la kuiba mikoba ya watu nalo neno.
Linaweza kukusababishia mafuta ya taa na kiberiti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…