Sirocco: Nokia yaunda simu imara zaidi duniani ya Android

eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,235
16,205
Kampuni ya Nokia imetangaza kuwa imeunda simu ya Android ambayo ndiyo imara zaidi kiasi kwamba haiwezi kuvunjwa kwa mkono.

Kampuni hiyo pia imeanza kuuza simu nyingine yenye sehemu ya kuteleza, ambayo inafanana na simu zilizokuwa maarufu mwishoni mwa miaka ya 1990 na mwanzoni mwa miaka ya 2000.

Simu hiyo ya Nokia 8 Sirocco imeundwa kwa sehemu ya juu ya chuma cha pua na inadaiwa kuwa imara zaidi kwa sasa.

Simu ya Nokia 8110 inakumbatia muundo wa zamani wa simu, ambao ulitumiwa kwenye filamu za Matrix.

Wachanganuzi wanasema simu hizo mbili zitaendeleza ufanisi wa simu za Nokia sokoni uliopatikana mwaka jana kutokana na uuzaji wa simu maarufu za zamani za Nokia 3310.

Ingawa simu hizo zinauzwa kwa jina la Nokia, zinaundwa na kampuni ya Finland kwa jina HMD Global ambayo ilipata haki na idhini ya kuunda na kuuza simu za Nokia.

Simu ya Nokia 3310 yazinduliwa upya
Kampuni hiyo ilijipatia umaarusu sana katika Maonesho ya Dunia ya Simu za Rununu mwaka 2017 ilipozindua simu za 3310 pamoja na simu nyingine za kisasa zenye nguzu zaidi.

Yamkini kampuni hiyo ililenga kurudia ufanisi wa mwaka jana katika maonesho ya mwaka huu wikendi mjini Barcelona.

Haki miliki ya pichaNOKIA

Pamoja na kuundwa kwa chuma, Nokia 8 Sirocco pia haiwezi kuingia maji na haiwezi kusumbuliwa na vumbi

"Mwaka uliopita ulikuwa kuhusu kuzindua upya biashara ya simu za kisasa za Nokia," alisema Ian Fogg kutoka shirika la ushauri la IHS Technology.

"HMD walianza kuuza simu hizo nchi za nje miezi saba ya mwisho mwaka 2017, na katika kipindi hicho walifanikiwa kuuza zaidi ya simu 8 milioni.

48ef3e13a6ed5d7ebabd07f52c54f83f.jpg
a97dc430769d42a8ffadcd316950ef76.jpg
 
kwa simu za jana walizotoa Nokia my favourite ni Nokia 7 plus.
-Flagship camera
-perfomance kubwa karibia na flagship
-bei isiyoumiza kichwa.

wakiitangaza vizuri itauza sana.
vipi kuhusu ukubwa wa RAM, internal memory, camera na bei yake sh ngap?
 
Back
Top Bottom