Ronal Reagan
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 5,298
- 3,057
Salaam! Nafurahi kuwaona tena wengi wenu mkiendelea kujadili na kuchambua mambo mengi – hasa siasa. Naendelea kuipongeza JF kwa kuendelea kuwa Jukwaa bora na huru kwa mambo ya kisiasa katika nchi yetu, licha ya changamoto nyingi ambazo imepitia.
UTANGULIZI
Kwanza kabisa nitambue uwepo wa “wakongwe” wote! Pili nitambue uwepo wa vijana wote, hasa wapya – bila kujali itikadi, dini, rangi au jinsia zao. Niwapongeze kushiriki siasa, nataka kuwathibitishia kuwa SIASA NI MUHIMU. Vijana wengi wakishiriki siasa, mapema, na wakapata elimu, taarifa sahihi, na jukwaa la kushiriki kwa uhuru na weledi ngazi mbalimbali hiyo ndiyo afya ya taifa. Ndio maana vyama na taasisi zozote makini huwapa vijana nafasi – karibuni sana!
Nimelazimika kuandika kwa kirefu kidogo ili ninyi vijana mjue mawili-matatu, hasa taarifa hali ya nchi yetu na aina ya sisasa za nchi yetu. Hamtajua bila kuuliza na kujuzwa ukweli wote. Ni budi muwe na utaratibu wa kusoma, kutafuta, kuuliza, kuchambua, kujadili mambo ili kupanua mawazo. Ukweli una gharama, haki pia ina gharama. Uhuru una gharama. Amani ina ghrama. Elimu bora pia ina gharama. Maisha ni ya thamani sana, gharama yake ni kubwa kwani inajumuisha hayo yote. Hakuna kitu cha thamani kilicho cha bure, vyote vina gharama. Ndio maana kuoa/kuoelewa kuna gharama. Baadhi ya mambo humu yatakera na kusumbua hisia zenu. Hilo ni sawa na muhimu. Ili mtafute majibu na kushiriki kuwa sehemu ya majibu ya maswali ambayo yanalisumbua Taifa letu kwa miongo zaidi ya mitano sasa.
ASILI
Nataka kuwapa taarifa, nataka kuwapa kazi “assignments” kwa sababu jamii bora hujengwa na nguzo bora na imara – elimu, desturi, utu, hekima, haki, ukweli, ujasiri, uwazi, ushiriki, nk. Fikra bora hujengwa na elimu bora & endelevu (sio bora elimu) na mijadala huru na endelevu. Kuna njia nyingi za ushiriki, lakini ya msingi zaidi ambayo ina wajibu pia ni kupiga kura ili kuchagua au kuchaguliwa. Kila baada ya miaka 5 nchi yetu huitisha chaguzi kuu mbili – Serikali Kuu (rais, wabunge na madiwani) na Serikali za Mitaa (wenyeviti wa mitaa, vijiji nk), na hupishana kwa takriban mwaka mmoja. Maudhui ya chaguzi hizi ni kuwapa wananchi fursa” ya kuchagua viongozi. Mfumo unaotumika ni wa kura za moja kwa moja. Chaguzi zote hizo zilikuwepo toka miaka ya sitini; na zimeendelea kubaki vile vile ukiondoa badiliko dogo la kuwa na wagombea kutoka nje ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya mwaka 1992 kwa nchi yetu kuingia mfumo wa vyama vingi, na rasmi kuanzia mwaka 1995. Tume ya Uchaguzi (NEC) iliundwa mnamo mwaka 1993, na kuanzia hapo imekuwa ikaratibu na kuandaa chaguzi zote.
Historia na mazingira ya Tanzania kuingia mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 ni ya ajabu na kushangaza, sio kidogo. Serikali ya Awamu ya Pili ya Mh. Ally Hassan Mwinyi iliitikia wito wa kuwa nchi ya “kidemokrasia” kwa kuunda Tume ya kukusanya maoni chini ya Jaji Francis Nyalali mnamo mwaka 1991. Kwa mujibu wa maoni hayo, asilimia zaidi ya 75% ya Watanzania “walikataa” mfumo wa vyama vingi, yaani “walimua”kuwa nchi ibaki chini ya mfumo wa chama kimoja – na sababu kuu iliyotajwa ni kuwa vyama vingi vitaleta vita. Hivyo “wananchi” walichagua Amani badala ya Vita au machafuko! Tume ya Mh. Jaji Nyalali kwa kushauriana na Rais wa kwanza hayati Mwl. Julius Nyerere, ilipendekeza kuwa pamoja na maoni hayo ya “wananchi”, Tanzania ni vema ikaingia kwenye mfumo wa vyama vingi. Na ndipo rasmi mwaka 1992 Tanzania “ikarudisha rasmi” mfumo vyama vingi, kwa KUREKEBISHA (sio kubadilisha) Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 ili iruhusu uwepo wa vyama shindani, yaani vingi. Katiba ya Nchi ya Mwaka 1977 ilitokana na kuundwa kwa CCM kuchukua nafasi ya TANU – kwa Tanganyika na ASP kwa Zanzibar. Ikafutiwa na “chama kushika hatamu”.
Tahadhari: Mtu yeyote, wakati wowote na kwa sababu zozote ambaye hana nia njema na wewe au jamii yako au taifa lako ni yule atakayekunyima kutumia haki na wajibu wako huo wa msingi aidha kwa kukupumbaza, kukudanganya, kukutisha, kukurubuni, kukunu, kukunyima au kutoheshimu ulichochagua – huyo/hao ni wahaini, magaidi na mtu/watu hatari sana kwako na Taifa lako!
Na mtu yeyote anayekupa elimu mbovu ili kupunguza au kuminya uwezo wako wa kufikiri na kuchagua vizuri basi tambua huyo ni mwovu, katili na adui wa Taifa lako, maisha yako na familia yako! Pia mtu yeyote anayejenga mazingira na mfumo duni ili wewe usitekeleze wajibu wako huo huyo ni mtu mnafiki, batili na mharibifu – usimheshimu wala kumpa nafasi au kushiriki kukuharibia maisha yako, jamii yako au nchi yako! – na huo ndio UZALENDO hasa!!! Mtu yeyote, wakati wowote akifanya yote au mojawapo ya hayo – MKATAE! Hastahili heshima yako wala huruma yako.
HALI
Jiulize; hao wananchi na wapiga kura waliopiga kura kwa Tume ya Jaji Nyalali ni wapi?
Tanzania ina tatizo moja kubwa sana na sugu, ambalo ni zaidi ya Mh John Magufuli. Tatizo hilo ni pana, zito na kongwe na linapatikana kwenye mfumo na sheria za nchi yetu. Kwa sababu sheria zetu nyingi hazitoi haki na hata zile chache zenye kutoa haki basi zinahitaji watu wapenda haki, wajasiri, weledi na hodari kutoa hiyo haki. Msomaji anapaswa kujua tofauti kati ya haki na sheria. Sio kila sheria inatoa haki.
Kuwepo kwa mfumo wa sheria usio toa haki ni tatizo kubwa, lilianzishwa na kulelewa na CCM. Kwa hiyo basi CCM ni tatizo kubwa kuliko mtu mmoja - linalobeba maadui wote wa nchi yetu mfano maradhi, ujinga, rushwa/ufisadi, umaskini na mauaji. CCM ndio adui namba moja. Ni Kweli Mh Magufuli ana madhaifu makubwa kama Rais – lakini ametoka Chama gani? Amelelewaje?
CHADEMA sio perfect kama vile CCM isivyo perfect. Vyama na wanasiasa WOTE sio perfect - perfection is merely an illusion under the sun. Na ndio maana nimejikita kuonyesha udhaifu, uozo na ubaya wa CCM maana ndicho chama kimekuwepo madarakani. Kikija chama kiingine nitafanya hivi hivi – huo ndio wajibu na haki yangu kama raia na mzalendo (patriot). Na ndio maana nataka chama kingine kishike dola.
Hivyo basi kwa vile CCM sio perfect, hakijawahi kuwa perfect na hakitokuja kuwa perfect; na tena kwa vile hakuna chama chochote cha siasa au mwanasiasa mwenye kuhodhi ukweli au mustakabali wa nchi yetu kama apendavyo yeye, ni budi basi bila woga wala kusita kuitoa CCM madarakani ili nchi yetu ianze upya – RESET. Achana na dhana na hoja dhaifu za hatari, vita, fujo nk nk kwanza itolewe maana Tanganyika ilikuwepo kabla ya CCM na bado itakuwepo baada ya CCM. Wao ndio wenye hofu sio wananchi wa kawaida - ukitazama kwa undani. Hivyo basi ifanyeni hofu yao kuwa halisi tarehe 28 Oktoba 2020!
Kila kitu kilichotengenezwa na mwanadamu huchanua, hustawi kasha hufa – kwa sababu muda huvifanya viwe havifai, viwe takataka (irrelevant and useless). Na CCM hakiwezi, hata wakisemaje au kufanya nini, kuepuka utaratibu huo wa kuwa kila kitu kina wakati wake na majira yake. Watanzania tupige kura kuitoa CCM madarakani, kisha tuibane serikali mpya ili nguvu na madaraka yarudi kwetu sisi wananchi na sio kukaa kwenye mikono ya wachache kwa maslahi yao. Hao wenye maslahi wameunda “magenge” mengi tu na mengine wanayaita “taasisi” au “mamlaka”. Tunahitaji sasa madaraka halisi na sio kivuli & usanii uliopo sasa; na vitawafanya wanasiasa kuwajibika zaidi, nchi yetu kuwa na taasisi imara zaidi za kiutendaji na hivyo kupelekea kuwa na mfumo bora na imara wa kuleta maendeleo. Kama tukitumia vizuri miaka 2-3 ya mwanzo ya Serikali Mpya kujipanga kwa kujadili kwa uwazi na kina mambo yetu kasha tukafanya uchaguzi katika mfumo mpya na bora tutafanikiwa kweli kweli. Maana watawala wetu wamekuwa wakicheza na maisha yetu kwa kejeli na ahadi nyepesi ambazo zimekuwepo kwa zaidi ya miaka 40 sasa. Hakuna uwajibikaji na hakuna uhuru wala tumaini isipokuwa sisi wananchi tuamue kweli na kwa dhati kuwa tunataka mabadiliko ya kimfumo na kimaisha. BOFYA kitufe cha RESET kwa kura yako 28 Oktoba 2020.
Mvinyo mpya kwa kiriba kipya, tunahitaji vyote viwili ili tufanikiwe.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki Watanzania!

- Ni wale wale waliokuzwa na kulelewa toka TANU, na miaka yote waliipigia kura CCM.
- Walifundishwa na kukariri kuwa Ujamaa ni imani. Yaani kwao maisha na taifa vimefungwa na kutafsiriwa na Ujamaa = CCM.
- Waliojua kusoma na kuandika tu – wasiokuwa na uwezo wa kufikiri au kuchambua mambo
- Hawakuwa na elimu wala upana wa fikra au uzoefu wowote zaidi ya huo walioukuta na kuuzoea (maana yake hawakujua au kuwa na uwezo wa kuchagua in any real sense)
- Walikuwa na ufinyu wa taarifa - redio (moja) ya Taifa kama chombo kikuu cha kuwapasha habari za ndani na nje. Magazeti (ya Chama [CCM]) na ya Serikali (ya Chama hicho hicho) hayakuwa na tofuati wala huru. Hata magazeti kama vile Mfanyakazi, yalikuwa ya kipropaganda zaidi, sio huru wala kiuwezo tofauti na yaliyotangulia.
- Hakukuwa na internet, TVs wala JF, kama ilivyo sasa – ambapo unaweza pata habari na taarifa kwa njia zaidi ya hizo zinazoratibiwa na dola.
- Jiulize; kwa nini Jaji Nyalali & Mwl. Nyerere (Mwasisi wa TANU, CCM, Ujamaa na Mfumo; Rais wa kwanza wa Tanzania) walipendekeza nchi iingie kwneye vyama Vingi – kinyume na maoni ya “wananchi”?
- Ilikuwa ni njia ya kujibu mbinyo (pressure) wa Kimataifa.
- Kuvunjika kwa Soviet Union (Ujamaa) kuliashiria kushindwa kwa ujamaa katika Vita Baridi kati ya Urusi na Marekani, Ujamaa vs Capitalism, Mfumo Kandamizi vs Demokrasia nk
- Ni rahisi kumpeleka punda mtoni lakini huwezi kumlazimisha punda kunywa. Na hadi leo tunashuhudia kuwa punda (Tanzania) hakuwahi kutaka kunywa maji (mfumo wa vyama vingi).
- Ilikuwa ni njia rahisi ya kuepusha misuguano ya moja kwa moja na nchi za Magharibi (Capitalist States) na hasa kwa vile Urusi & Ujamaa vilikuwa dhaifu.
- Ilikuwa ni njia rahisi ili KUHODHI mfumo mzima bila kuingiliwa toka nje.
- Ni wazi basi, “nia njema ya Mwl. Nyerere” haikumaanisha kumpa uhuru au uchaguzi Mtanzania wa kawaida bali kulinda Mfumo na Chama chao (wao huita Nchi).
- Msomaji, chunguza sana kauli za, mfano, “sisi” au “nchi” kila….na utagundua kuwa mara nyingi ni za kupumbaza tu, wewe haumo! Kama umo kwa nini hali yako iko hivyo?
- Hali ya Nchi yetu kiuchumi ilikuwa mbaya kwa hiyo ilikuwa ni kukaa kinafiki ili ule vya “kafiri”.
- Jiulize; kama wachache waliweza kubadilisha na kupindua maoni ya wengi, je! kwa nini wasiendeleze utamaduni huo leo?
- Ilikuwaje watu wachache kuamua kwa niaba ya wengi? Maana kama ni hofu ya vita na machufuko basi wengi ndio ingewahusu. Walisema “Njia ya Mwongo ni fupi”. Kwa kitendo kile ina maana walizoa matapitishi yao na kuyala. Ndio! Ina maana kwa miaka yote walikuwa wakiwadanganya wananchi kwa na propaganda zao (nao ni mahiri kwa propaganda) mbaya dhidi ya kitu ambacho aidha haikukuwepo au kilichopotoshwa au kilichotungwa kwa malengo na faida za wachache tu.
- Kama wachache wale walikuwa na hiyo nguvu na uwezo ule kupindua na kubadili, kwanini walisumbua wengi? Ina maana yale yalikuwa maigizo. Na kama walifanya maigizo ili kulinda maslahi yale yale, je kwa nini leo wasiendelee?
- Kwa nini wasingewauliza wachache tu ili kunusuru fedha na muda kutupotea kwa maigizo? – kwa sababu ni wanafiki na wabinafsi. Je kama walikuwa wanafiki zamani je leo wameacha au wamezidi kuwa wanafiki na wabinafsi? Mnafiki huwa habadili tabia ila ngozi ya nje tu.
- Tume ya Nyalali iliundwa kama kivuli tu, lakini mrejesho (maoni) yake ili KUHALALISHA mambo tunayoyaona na kuyashuhudia leo. Mfano hakikuweka nguvu na msisitizo wa KUBADILISHA Katiba ambayo ndio Sheria Mama (iligusia tu). Haikuona mbali zaidi ya miaka 3!
- Yaliyotokea kwenye Tume Ya Nyalali yaliakisiwa katika Uchaguzi wa mwaka 1995 na yameendelea kutokea katika chaguzi zilizofuata.
- Maoni (kura) za wananchi kupuunzwa
- Matokeo huratibiwa na watu wachache kwa maslahi ya wachache. Ndio wenye maamuzi.
- CCM kuhodhi chaguzi kupitia teuzi – ni kiongozi gani wa taasisi yoyote nyeti ambaye si mwana-CCM iwe kwa matendo au itikadi?
- Uwepo wa vyama na wagombea pandikizi (mamluki) – Anzia kwa Mh Agostino Lyatonga Mrema, nenda kwa Mh Edward Lowassa, Mh Benard Membe na wengineo katika kila ngazi hasa ubunge.
- Kwa CCM uchaguzi ni vita. Wananchi hawajui, kondoo wa kuhalalisha maamuzi ya wachache. Wapinzani wamelala au ni wazembe.
- Tasisi zote nyeti ni butu, bubu na dhaifu katika kusimamia chaguzi ziwe huru na haki. Hakuna taasisi yoyote ambayo haijielekezi au kutumika kwa maslahi ya CCM na kuhakikisha CCM na wagombea wanapata upendeleo na sapoti kushinda chaguzi hasa wa Rais na Wabunge.
- CCM imeendelea kutumia silaha na mbinu zile zile. Hawana haja ya kubadilisha kwa sababu kwanza zinawapa kile wanachokitaka. Pili mfumo unahitaji hizo silaha.
- UJINGA
- Miaka ya 60-70 Mwl. Aliwahi kueleza katika hotuba zake kuwa lengo la mfumo wa elimu wan chi yetu ni kuzalisha “watiifu wasio na uwezo wa kuhoji” na watumishi wachache. Matokeo yake yanapimika na kuonekana. Kwani mfumo wetu wa elimu umebadilika?
- Je iwapo mjinga atabaki katika hali ya ujinga, hali yake kiakili haiwi mbaya zaidi?
- Kwa waovu na wakatili, ujinga ni silaha na ambayo huitengeneza na kuitumia bila huruma.
- RUSHWA
- Umewahi kusikia au kuona watu wakilishwa nyama, pilau, soda nk katika kampeni za chaguzi?
- Uliwahi kusikia takrima ni ruksa?
- Umewahi kusikia bila kuwa na hela huwezi pata uongozi
- Uliwahi kumsikia Mwl. Nyerere akilalamika kuwa rushwa ilikuwa donda ndugu na alipoondoka likawa baya zaidi hasa ndani ya CCM?
- Umewahi kusikia au kuona wagombea wa nafasi za uongozi CCM wakilalamika kuwa rushwa ilitumika kumpitisha flan na sio wao – na wengine wakatoa ushahidi. Lakini mwisho wake umewahi kusikia mjumbe au mgombea wa CCM (kwa uwiano) ameadhibiwa kwa kosa hilo mbele ya Mahakama ya Sheria? Kwa nini?
- VITISHO
- Umewahi kusikia vitisho vya fujo, uvunjifu wa amani kutoka CCM kwenda kwa wananchi?
- Umewahi kushuhudia vitisho nyakati za kampeni?
- Umewahi kusikia mauaji, mateso na ukatili nyakati za kampeni?
- Umewahi kusikia au kuona ukatili wa Polisi kwenye mikutano ya CCM?
- Umewahi kusikia vitisho wanavyopewa kwa watumishi wa umma au wasimamizi wa chaguzi?
- PROPAGANDA
- Umewahi kusikia wakijinasibu kuwa kuku ni wao lakini wanatumia manati na nguvu kubwa kumkamata?
- Umewahi kusikia ahadi za uchaguzi na kulinganisha na kilichofanyika?
- Umewahi kujiuliza kwanini Tanzania na Watanzania bado ni maskini kwa wingi wao ingawa kila mara mnatajiwa “mafanikio, utekelezaji wa ilani na
- Umewahi kujiuliza kwanini huduma za msingi kama maji safi, afya na elimu bado ni duni na za kiwango cha chini mpaka sasa?
- Umewahi kujiuliza na kuchunguza maisha ya wapiga kura wengi CCM hali zao ki-elimu na kiuchumi?
- Umewahi kusikia wakijisifia “Mbinu za ushindi”? Je umewahi kuzichunguza kidogo ni zipi?
- Ukweli ni kwamba hakuna Uchaguzi Huru wala wa HAKI katika mfumo na mazingira tuliyonayo. Ni rahisi kubaini na kulithibitisha hilo.
- Nitoe rai kwa wale wana CCM na mashibiki wao, waje hapa au popote kwenye majukwaa halisi (sio kwa watoto wa shule au kwa wasiojiweza kiakili (wajinga) au wenye njaa - na waseme ni kwa namna gani hilo litawezekana. Watueleze kwa nini limeshindikana katika chaguzi zote na mpaka huu wa 2020. Sio kusema TUME (NEC) au Rais kasema uchaguzi utakuwa huru iishie hapo. Hapana tafadhali! Jionee huruma na thamini utu wako.
- Huwezi kukusanya watu wasio na uwezo wa kusikia na kuelewa jambo (kwa vile mfumo wa elimu uliwajenga hivyo kwa makusudi ya watawala) uwaeleze mambo ambayo hawajui na hata baada ya kuyasema giza na upofu wa fikra umebaki jinsi ulivyokuwa. Ila wamekariri(shwa) viitikio.
- Kama ilivyo kwenye kila Nyanja muhimu mfano uchumi au elimu kuna madaraja. Kuna nchi zilizoendelea za ulimwengu wa kwanza, pili, kati na kuna nchi maskini. Kwenye Demokrasia ni hivyo hivyo. Kuna demokrasia ya kiwango cha juu mfano Marekani, UK, Israel, Uholanzi, Australia. Kuna demokrasia za kati mfano India, Korea Kusini na Brazil
- Na zenye demokrasia la chini mfano Tanzania na nchi nyingi za Africa na America Kusini. Na mbovu mfano Korea Kaskazini, China na Sudan.
- HISTORIA & UTAMADUNI
- Hakuna RAIA wa Marekani au mkazi wa Florida aliyewahi kuzamia au kutoroka kwenda Cuba kutafuta maisha bora.
- Hakuna raia wa Korea Kusini anayetorokea Korea Kaskazini, bali kuna maelfu wanaotoka Korea Kaskazini kukimbilia Kusini kila mwaka – na wengi hukamatwa - kisha kuteswa na/au kuuwawa au kupotezwa.
- Hakuna nchi za Kijamaa zilizowahi kusaidia nchi za Kibepari! Lakini leo nenda Russia na kwenye zilizokuwa nchi za Soviet uone uhalisia.
- Maana yake ni nini? Ujamaa ni ushetani (ndio walivyosema wenyewe, ndivyo walivyotenda na ndivyo historia inasema). Ujamaa ni uovu (unajua mauaji na ukatili wa Joep Stalin? Unamjua Pol Pot wa Cambodia? Unamjua Adolf Hitler alikuwa Socialist? Unamjua Fidel Castro wa Cuba? Someni, tafuteni ukweli zaidi ya hayo yaliyoratibiwa na kutungwa kwa ustadi ambayo mnayaita elimu. Ujamaa ni mfumo katili, wa hila na ulioshindwa kumsaidia mwanadamu katika wakati wowote kuanzia kuumbwa kwa ulimwengu. Ndio!
- Achana na nadharia za kwenye vitabu na maneno ya kuvutia ya Maprofesa na Wanasiasa, nenda mbali zaidi kachunguze maisha halisi ya watu halisi katika dunia halisi. Tembeeni duniani muone. Panua wigo wako wa taarifa na elimu. Jikomboe sasa kutoka kwenye kifungo, tambua KWELI nayo itakuweka huru. Ni KWELI tu ndiyo yenye nguvu ya kukukomboa na kukuweka huru toka kwenye utumwa na nira za ujinga na ujamaa, mengine ni udanganyifu na kujilisha upepo!
- Wasivyo na hekima na ambao ni maskini wa hoja na wenye upungufu wa KWELI watashambulia na kudhihaki yaliyomo hapa bila kujibu au kupangua hizo hoja! Watapiga kelele zile zile tulizokuwa nazo wakati wa vita baridi……hawana jipya.
- Hoja hupingwa kwa hoja. Narudia tena, Ujamaa (ambayo ni imani) ni ushetani. Na Shetani hana zawadi ya bure. AMKENI!
- Komesheni na vunjilieni mbali utamaduni haramu wa hila na uonevu wa CCM. Kila kizazi cha wanadamu kina changamoto na fursa zake. Kizazi hiki kina wajibu wa kukomesha na kung’oa mambo ya kishenzi yaliyopakwa rangi za kuvutia lakini ni mafu na ya hovyo kabisa. Maisha ni halisi, sio kuendelea kucheza na akili za watu na vijizawadi vya kupumbaza akili kwa muda mfupi wakati wa kampeni.
- SANAA & USHIRIKINA
- Vipi uliwahi kusikia Mwl. Nyerere akisema redioni jinsi alivyofanyiwa zindiko Bagamoyo ili atawale nchi hii? Sidhani kama kuna maandiko ya hotuba ile. Tafuteni.
- Umewahi kusikia vikundi vya ngoma, sanaa na muziki vikitumbuiza ili kuita nakutafuta kibali CCM nyakati za Kampeni. Zile “burudani” ni kuwapa faraja la uongo katika maumivu yenu.
- Zile burudani wala sio hata pain killer ni kilevi tu. Baada ya hapo maumivu yanabaki pale pale.
- Wasanii wanamuziki – hawa wamekuwa wakitumika kwa lengo na sharti maalum ili kuleta watu, kutafuta uhalali na kibali cha wananchi na kupumbaza wengi ili kugeuza akili ziwe hisia. (Search out what happens when emotions replace thinking)
- Je umewahi kusikia au kuona kuwa nyakati za chaguzi kuwa waganga & wachawi hupata biashara kubwa zaidi? Yaani hukiita kipindi hiki kuwa cha mavuno!
- Ukiwa na viongozi wanaoenda kwa waganga na masangoma maana yake wanadhirisha kuwa hawana uwezo wala kibali cha uongozi - na wewe ukimpa kura yako basi umekubaliana na mambo ya kishenzi aliyofanya huko gizani. Kuna wakati Bunge la JMT lilikuwa na wabunge wanaosema hayo Bungeni na wengine walikuwemo mle na mnajua walitoka chama gani.
- Tawala zote dhalimu katika historia, hasa kuanzia kwa Wagiriki (Wayunani), Warumi na Wajamaa wote zinajua udhaifu wa mwanadamu kuhusu muziki na burudani za sanaa. Na kwa kulitambua hilo zimekuwa zikitumia muziki ili kuendelea kutawala na/au kupotosha fikra za wananchi wao kila wanapohitaji kufanya hivyo. Hizo burudani zao zinalenga lilo hilo.
Tanzania ina tatizo moja kubwa sana na sugu, ambalo ni zaidi ya Mh John Magufuli. Tatizo hilo ni pana, zito na kongwe na linapatikana kwenye mfumo na sheria za nchi yetu. Kwa sababu sheria zetu nyingi hazitoi haki na hata zile chache zenye kutoa haki basi zinahitaji watu wapenda haki, wajasiri, weledi na hodari kutoa hiyo haki. Msomaji anapaswa kujua tofauti kati ya haki na sheria. Sio kila sheria inatoa haki.
Kuwepo kwa mfumo wa sheria usio toa haki ni tatizo kubwa, lilianzishwa na kulelewa na CCM. Kwa hiyo basi CCM ni tatizo kubwa kuliko mtu mmoja - linalobeba maadui wote wa nchi yetu mfano maradhi, ujinga, rushwa/ufisadi, umaskini na mauaji. CCM ndio adui namba moja. Ni Kweli Mh Magufuli ana madhaifu makubwa kama Rais – lakini ametoka Chama gani? Amelelewaje?
- Kwanza sio kiongozi ni mtawala.
- Ana jazba na hana staha inayokipasa cheo na kiti husika.
- Hana hekima – Urais au Uongozi bila hekima ni sawa na mti bila mzizi, hakuna matunda.
- Hana upendo – jazia hapo mwenyewe
- Hapendi haki wala ukweli – ni mbaguzi, jeuri na mwenye kulipiza visasi. Pia ni mwongo.