Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,535
Juzi alfajiri ya Aprili 19, mwaka huu, Kiba alifunga ndoa na mrembo Amina Khaleef katika Msikiti wa Ummul Kulthum uliopo mjini Mombasa, Kenya. Ndoa hiyo ilifungishwa na Sheikh Mohamed Kagera.
Hakika ilikuwa ni furaha, shangwe, nderemo na vifijo kwa maharusi hao, wanafamilia na mashabiki wa Kiba mjini Mombasa mara baada ya ndoa hiyo kufungwa.
Mara baada ya kufungwa kwa ndoa hiyo, mitandaoni kulichafuka ambapo baadhi ya mashabiki wa Kiba walikuwa wakihoji ni kwa nini mkali huyo wa Wimbo wa Seduce Me ameacha warembo kibao Bongo na kwenda kwa Amina wa Mombasa? Kufuatia wengi kutaka kujua Amina ni nani au ana nini cha tofauti kilichomteka Kiba, Risasi Jumamosi lilifanya uchunguzi wake wa kushiba na kuibuka na siri sita zilizomvutia Kiba kwa mrembo huyo na kuwasahau kabisa warembo wa Bongo;
Uchunguzi huo ulibaini kwamba, Amina ambaye aliingia kwenye uhusiano wa uchumba na Kiba mwaka 2016, ana sifa za kuwa mke (wife material) na pia anafaa kuwa mama bora kutokana na utulivu wake na kujua malezi kwa jumla. Ilibainika kwamba, Amina ni binti mwenye maadili na aliyekulia kwenye familia iliyoshika mno Dini ya Kiislam hivyo ‘amekwiva’ kwenye eneo hilo la kuwa mama bora wa familia ukilinganisha na warembo wengi wa Kibongo ambao ilisemekana, wengi hawajatulia na hawajashika dini kwa dhati zaidi ya kuigiza tu.
2: SIYO TEGEMEZI, NI MCHAPAKAZI
Uchunguzi huo uliotumia watu wa nyumbani kwa akina Amina ulibaini kwamba, mrembo huyo mwenye umri wa miaka 23, siyo mtu wa kukaa tu nyumbani na kusubiri kuletewa pizza au chipsi kuku na mwanaume, bali ni mchapakazi asiyependa kuwa tegemezi, tofauti na mabinti wengi wa Kibongo ambao hubweteka na kutegemea kila kitu kutoka kwa wanaume.
3: SHULE IPO KICHWANI
Ilifahamika kwamba, Amina hakukimbia umande kwani ni msomi mwenye shule yake kichwani, akiwa amehitimu masomo ya uhasibu kwa levo ya chuo kikuu na kuwa mfanyakazi wa serikalini katika Kaunti ya Mombasa. Hii ni tofauti na baadhi ya mabinti wa Kibongo ambao wengi walikimbia umande.
4: UZURI WAKE SIYO FEKI
Ukimtazama Amina hata kwenye picha zilizosambaa mitandaoni, utagundua kuwa uzuri wake ni wa asili na siyo wa kutengeneza yaani feki kama walivyo warembo wengi wa Kibongo. Ilielezwa kuwa, kutokana na mvuto wa kipekee alionao, basi Amina amebeba maana halisi ya uzuri wa mwanamke. Hana makalio feki ya kutengeneza wala nido zake kifuani siyo za kubusti na hategemei make-up ili aonekane mzuri bali kila kitu kwake ni cha asili.
5: HASHINDI NA KUKESHA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII
Uchunguzi wetu huo ulibaini pia kwamba, Amina siyo mtu wa kushinda na kukesha kwenye mitandao ya kijamii kama walivyo warembo wengi ambao kazi yao huwa ni kuposti picha na video za kuwatamanisha wanaume. Katika kuthibitisha hilo, tangu aingie kwenye uhusiano na staa huyo mkubwa ambaye kwa mrembo mwingine angefanya matangazo kwenye mitandao ya kijamii hadi dunia nzima ijue, lakini Amina yeye hakuwahi kufanya hivyo.
6: ANAJUA ATAKAVYODILI NA WALIOMZALIA KIBA
Ilifahamika kwamba, Kiba ana watoto watatu ambao kila mmoja ana mama yake, lakini ilisemekana Amina alimhakikishia atakavyodili na mama wa watoto hayo na yupo tayari kuwalea bila kusababisha drama au tafrani. Sifa nyingine aliyoelezwa kuwa nayo Amina ni pamoja na kujua kutunza siri za familia kama alivyofanya kwenye uhusiano wake na Kiba tangu mwaka 2016 bila kujali skendo zilizokuwa zikimuandana staa huyo.
MASKINI MASTAA HAWA, BAHATI HAIKUWA YAO
Kabla ya kumuoa Amina, Kiba aliwahi kutajwa kutoka na warembo mbalimbali wakiwemo wanawake watatu aliozaa nao, mastaa wa Kibongo, Jokate Mwegelo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Jacqueline Wolper na wengineo ambao mashabiki wao wengi waliwahurumia kwa kukosa bahati ya kuolewa na staa huyo anayejiita Pasua Kichwa