Nasema Uongo Ndugu Zangu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 279
- 779
Ajali mbaya iliyo husisha gari dogo aina ya Raum imetokea wilayani Mkalama katika mkoa wa Singida.
Chanzo cha ajali ni mwendo kasi.
Mzee Kinana nilikwambia kupitia uzi fulani hapa, kazi iendelee.
========
Watu sita wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Raum, kuacha njia na kupinduka katika eneo la Iguguno Ushamba Wilayani Mkalama Mkoani Singida, huku chanzo kikitajwa kuwa ni mwendokasi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Stella Mutabihirwa, amesema tukio hilo limetokea jana na kusema Dereva wa gari hilo alikuwa anaendesha bila kuchukua tahadhari na ndipo gari hilo lilipohamia upande wa pili wa Barabara na kupinduka mara tatu.
Ajali hiyo imetokea kwenye Barabara Kuu ya Dar es Salaam - Mwanza wakati abiria wa gari hilo wakitokea Arusha kuelekea Mwanza ambapo Watu watano kati yao walipoteza maisha papohapo huku Dereva wa gari hilo akipoteza maisha wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Singida.