Singida Big Stars Football Club | Special Thread

Aug 31, 2022
14
27

Logo sbs.JPG

Ndugu WanaJF,​

Karibuni kwenye uzi maalum wa klabu yetu ya Singida Big Stars. Kupitia uzi huu mtafahamu masuala mengi kuhusu klabu yetu ambayo ni mgeni wa Ligi Kuu Tanzania Bara na msimu huu ukiwa ni msimu wetu wa kwanza kushiriki Ligi Kuu ya NBC (2022/2022).

HISTORIA

Klabu ya Singida Big Stars imeanzishwa na kupata usajili wake kamili chini ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) tarehe 20 Desemba 2021.
Singida Big Stars ni klabu ya soka ya Tanzania yenye maskani yake mjini Singida. Klabu yeu ilibadili jina kutoka DTB Football Club na kuwa Singida Big Stars Football Club baada ya kufuzu kuingia ligi kuu kutokra ligi daraja la kwanza.

Singida Big Stars inashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) na ni miongoni mwa klabu mpya kabisa kwenye ligi.

Tangu ilipopanda ligi kuu, Singida Big Stars imevutia watu wengi kitaifa na kimataifa na kutajwa miongoni mwa klabu zenye kuleta matumaini makubwa nchini Tanzania.

Klabu yetu imesajili wachezaji wazoefu, wanaojulikana na wenye vipaji vya hali ya juu kutoka Tanzania na sehemu nyingine duniani kama vile Brazil, Argentina, Angola, Ghana, Rwanda, Burundi na kwingineko - ili kuisaidia klabu kufikia dhamira yake kuu ya kutwaa mataji na kuzipa chalenji klabu mbili kubwa ambazo zina mashabiki wengi nchi nzima, Simba SC na Yanga SC, katika hali ya ushindani.

Klabu yoyote inaweza kufanikiwa kupitia juhudi za pamoja za mashabiki na wapenzi wake na Klabu yetu inatambua umuhimu huo katika maendeleo ya Klabu. Uwekezaji wa siku zijazo utaendelea kuelekezwa katika suala la kuboresha kikosi, kuboresha uwanja na maeneo ya mazoezi, vifaa na kushirikiana na jamii.

KIKOSI

Singida Big Stars ina jumla ya wachezaji 27 ambapo 12 kati yao ni wachezaji wa kigeni na 15 ni wachezaji wa ndani.

MAKAO MAKUU

Makao Makuu ya Timu Singida Big Stars ni mkoani Singida, Tanzania.

UWANJA

Uwanja wetu wa mechi za nyumbani ni Uwanja wa CCM Liti (zamani CCM Namfua).

MFUMO WA TIMU

Timu yetu inaendeshwa kwa mfumo kampuni ambapo ina bodi ya wakurugenzi inayoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi pamoja na sekretarieti/menejimenti.

Pia, timu yetu inajiendesha kibiashara ambapo masuala yote ya kiungozi na kiutawala yanafanyika kupitia Bodi ya Wakurugenzi na Sekretarieti husika.

BENCHI LA UFUNDI

Kocha Mkuu wa Singida Big Stars ni Hans van der Pluijm. Kocha Msaidizi ni Mathias Lule. Kocha wa Makipa ni Stephane Bire na Meneja wa Timu ni Nizar Khalfan.

Wengine ni Daktari wa Timu, Msaidizi wa Daktari, Mtunza Vifaa na Dereva wa Timu.

WADHAMINI

Kwa sasa, klabu ya Singida Big Stars imesaini mkataba na SportPesa kuwa Mdhamini Mkuu wa Klabu. Wadhamini wengine wa klabu ni Azam TV, GSM, Maji ya Uhai (Bakhresa), Benki ya NBC, Meru Sunola, TBL, Vunjabei na Airtel.

Mazungumzo yanaendelea na makampuni mengine ili kuweza kupata nguvu zaidi ya kifedha na huduma ili kuiwezesha klabu kujiendesha kibiashara na kuzisaidia kampuni hizo eneo la matangazo na mengineyo ya kibiashara.

SAFU YA UONGOZI

1. Ibrahim Mirambo - Mwenyekiti
2. Dismas Ten - Afisa Mtendaji Mkuu
3. Tabitha - Mkurugenzi Fedha na Masoko
4. Anatoly Nyaki - Mwanasheria
5. David Migongo - Muhasibu Mkuu
6. Hussein Massanza - Meneja Habari na Mawasiliano (Msemaji)
7. John Kadutu - Mkurugenzi Utawala​
 
Je, siku Mwigulu Nchemba akitoka kwenye nafasi ya Uwaziri wa Fedha, kuna uhakika gani wa hii timu ya Singida kuwepo?

Asante kwa maoni mdau.

Tungependa tufafanue kama ifuatavyo:

1. Timu yetu haiendeshwi na Mwigulu Nchemba wala kiongozi yoyote wa serikali. Upotoshaji kama huu ndio umefanya tuje na uzi maalum kuweka rekodi sawa.

2. Tuna wadhamini wa kutosha na tumeingia mikataba na makampuni yote kwa umakini ambayo inaenda kulinda maslahi ya klabu na sustainability yake.

3. Focus yetu ni kuleta ushindani kwenye ligi na kufikia malengo tuliyojiwekea.

Karibu Singida Big Stars. Tunahitaji sapoti yako kama mdau wa michezo.
 
Kwa kufanya scouting mpo vizuri sana. Kwa hilo hongereni timu changa lakini mmewaleta key players kutoka sehemu mbalimbali.

Kwa hili naomba mkawape semina hata wale makolo (Simba)......kwenye mambo ya kufanya scouting kwa wachezaji
 
Asante kwa maoni mdau.

Tungependa tufafanue kama ifuatavyo:

1. Timu yetu haiendeshwi na Mwigulu Nchemba wala kiongozi yoyote wa serikali. Upotoshaji kama huu ndio umefanya tuje na uzi maalum kuweka rekodi sawa.

2. Tuna wadhamini wa kutosha na tumeingia mikataba na makampuni yote kwa umakini ambayo inaenda kulinda maslahi ya klabu na sustainability yake.

3. Focus yetu ni kuleta ushindani kwenye ligi na kufikia malengo tuliyojiwekea.

Karibu Singida Big Stars. Tunahitaji sapoti yako kama mdau wa michezo.
Kwa udogo/uchanga wa timu yenu mliwezaje kupata wadhamini wengi kiasi hicho bila influence yeyote ya Mwigulu au kiongozi wa kisiasa?

Ni mbinu gani mliitumia ili timu nyingine changa zijifunze kutoka kwenu kwani mlichokifanya hakina tofauti na miujiza.
 
Siri ya yote haya ni taaluma. Tunafanya kila kitu kwa kuzingatia weledi na kufanya utafiti wa kutosha. Wadhamini wengi tuliowafuata na tunaoendelea kuwafuata wanashawishika na namna tunavyojieleza kwao, wakiangalia dhamira na mipango yetu wanaamua kutake risk na kuwekeza. Ni jukumu letu kuhakikisha tunafanya yale tuliyokubaliana nao. Hili la taaluma likawe somo kwa wenzetu.
 
Mwigulu Nchemba ni Silent Investor kwenye timu ? Na ana asilimia ngapi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom