Sindumuja - Ukweli kuhusu burundi 2

jMali

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
8,401
4,965
Baada ya Nkurunzinza kuamua kugombea tena, upinzani wa mwanzoni ulikuwa ni wa kisiasa zaidi, na ulijumuisha waburundi wa makabila yote ya wahutu na watutsi, ingawa watutsi walikuwa ndio wengi katika kupinga hatua hii ya Nkurunzinza. Mgogoro huu wa kisiasa ulimalizwa kisheria baada ya mahakama mbili tofauti kuamua kuwa tafsiri ya katiba ya Burundi inamruhusu Nkurunzinza kugombea.

Uchaguzi ukafanyika ingawa wapinzani walisusia uchaguzi kwa sababu wanazozijua wao. Sababu ya wao kutokwenda mahakamani kupinga tafsiri ya katiba haijulikani. Ni wazi kuwa wanajua hawana hoja! Ingawa haipendezi lakini ukweli ni kuwa kwa makubaliano ya Arusha, kisheria Nkurunzinza anaruhusiwa kugombea.

Baada ya kushindwa kesi za mahakamani ndani na nje ya nchi. Wapinzani wakasusia uchaguzi. Hivyo waliopiga kura ni wanachama na wafuasi wa Nkurunzinza tu. Lakini cha ajabu pamoja na kuwa wapinzani walisusia uchaguzi, uchaguzi uliandamwa na mashambulizi mbalimbali. Vituo vya kupigia kura vilichomwa moto, vikapigwa mabomu, watu walipigwa risasi, vifaa vilichomwa n.k. Ni wazi nani alikuwa nyuma ya machafuko haya. Nkurunzinza hawezi kuvamia vituo na kuua wapiga kura wakati yeye peke yake ndio anagombea! Cha ajabu the so called "international community" (read: the western countries and their media) haikulaani vitendo hivyo. Kwa nini wapinzani wafanye vitendo vya kigaidi dhidi ya raia wasiokuwa na hatia waliotaka kushiriki uchaguzi?

Uchaguzi ukampa Nkurunzinza ushindi. Waangalizi wakakubali matokeo na mpaka sasa hakuna nchi HATA MOJA DUNIA NZIMA ambayo haimtambui Nkurunziza kama rais halali wa Burundi kwa sababu yoyote ile.

Baada ya kuona hivyo maandamano sasa yamechukua sura mpya. Sasa wapinzani waandamana kwa slogan ya "sindumuja" movement. They can't be serious. Hiki ndicho kiwango cha upumbavu wao. Wameweka wazi malengo yao hadharani kwa yoyote yule ambae alikuwa na wasiwasi na hayuko biased. Hili neno kwa tafsiri rahisi ni "mimi sitakiwi kuwa mtumwa", au "I am not a slave", "not meant to be a slave" na tafsiri za karibu ya hapo.

Kwa mtu anayefahamu siasa za Burundi/Rwanda huu ni uchochezi. Of course ukiwauliza watakuambia inatafsiriwa vibaya, wao wanamlenga Nkurunzinza tu. Lakini nani hajui kuwa historically, wahutu walikuwa watumwa wa watutsi kwa miaka zaidi ya 400? Nani hajui kuwa mapinduzi yoyote ya wahutu yaliyofanyika yalisababisha wale watutsi wa "matawi ya juu" kuhamia uhamishoni kwa sababu tu ya kutotaka kuwa chini ya uongozi wa wahutu (original sindumuja) ambao wao wanawachukulia kuwa watumwa wao? Sasa wahutu ambao ndio wengi wachukuliaje hii slogan ya sindumuja ambayo inatumiwa na wapinzani ambao "coincidentally" majority ni watutsi, ambapo "coincidentally" wanayemlenga ni raisi mhutu wa chama cha kihutu kilicho madarakani baada ya kufanya vita vya miaka mingi dhidi ya serikali za kijeshi za kitutsi toka uhuru?

Hii imefanya hata wale wahutu wachache waliokuwa hawamtaki Nkurunziza kushitukia kuwa kumbe suala hapa sio kupigania demokrasia bali suala ni kabila la Nkurunziza, hivyo hata wahutu wachache ambao walikuwa wanampinga Nkurunzinza nao wamejitenga na hawa kina "sindumuja". Hii imesababisha kuanza kuonekana waziwazi kuwa wapinzani ni watutsi peke yao exclusively.

Mashambulizi na Mauaji:


Upande wa wapinzani ulishatangaza kuingia msituni na kufanya vita dhidi ya Nkurunzinza, cha ajabu wanaua raia wasio na hatia kwa kurusha mabomu hovyo, kuvamia mitaani na kumwaga risasi pasipo sababu. Kwa mtu asiyejua unaweza kuona hawa ni wendawazimu lakini angalia, kitakwimu wahutu ni asilimia zaidi ya 80 ya warundi wote, watutsi ni chini ya 20. Kimakazi watutsi wengi wako mjini Bujumbura tena wamejaa kwenye baadhi ya maeneo tu. Maeneo hayo hayashambuliwi na "waasi" ila ndio yanayoongoza kwa maandamano na vurugu dhidi ya Nkurunzinza. Mashambulizi haya ya "watu wasiojulikana" yanayoonekana ni ya hovyo hovyo, ya kupiga risasi masokoni yanamlenga nani? Niliwahi kusema, huwezi kuwa na vita kati ya wadosi na wabongo halafu useme hujui upande wa nani unarusha mabomu hovyo hovyo Tandale, na upi unarusha mabomu hovyo hovyo kisutu.

Mipango ya genocide:


Kwa anayejua siasa za watutsi na wahutu, kinachofanyika ni utengenezaji wa genocide kwa makusudi. Hatua zote zinazoendelea sasa zimeshawahi kufanya kazi Rwanda.

Sababu za vita:
Rwanda: Kagame alikataa mazungumzo na kufanya vita na serikali halali ya Rwanda chini ya raisi Habyarimana kwa miaka minne. Muda wote huo, Habyarimana alikuwa ni rais halali na anayetambulika dunia nzima na jumuiya zote za kimataifa except kwa watutsi wa RPA peke yao! Habyarimana akaamua kugawana nao madaraka kupitia mazungumzo, walipoona bado watakuwa chini ya wahutu ili hali wao ni "sindumuja", ndege itatunguliwa na wahutu wakalipa kisasi (genocide) na sasa hoja ikabadilika kuwa inabidi waingie kijeshi ili kuzuia genocide.

Burundi:
Hawa nao hawataki mazungumzo ya aina yoyote bila sababu za msingi ila wanataka vita bila sababu. Nkurunzinza hajawapiga, wala hapambani (ila anajilinda) ni rais halali na anayetambulika na nchi zote duniani. There is no legal basis ya kumpinga Nkurunzinza kwa kutumia vita. Mauaji yanayofanywa sasa na hawa ?sindumuja? hayana sababu yoyote ile. Lengo ni kughadhabisha wahutu ambao ndio majority (8/10) ya waburundi kufikia hasira za kuanza kulipa kisasi kwa kuua raia wenzao wa kitutsi, ili isemekane kuwa kuna genocide, na hivyo jumuiya ya kimataifa ipokonye utawala Nkurunzinza. Fikiria leo kutokee bomu sokoni likaua mkeo, kesho risasi shuleni, wafe wanao, hivi unadhani utaendelea kuwa mzima kichwani? Hawa wachochezi wanacholenga kuchochea ndio hicho. Kuwa ifikie wahutu wawehuke kama walivyowehuka Rwanda ili kutokee genocide.

Maandalizi ya keywords kwa matumizi ya baadae:
Rwanda: Wakati wanavamia Rwanda, waasi wa kitutsi RPA chini ya kina kagame walikuwa wanajiita "inyenzi", au "Mende", wakijisifia kuwa wanashambulia usiku na mchana hawaonekani. Neno hili halikuanzia hapo bali lilianzia kwenye miaka ya 60 kwa waasi wa kitutsi wakiongozwa na Aloyce Ngurumbe. Hivyo kina Kagame kutumia neno hili lenye historia hii ililenga tu kukasirisha wahutu kwa kuwafahamisha nini hasa wanamaanisha. Baada ya genocide, zikatengenezwa sinema nyingi na vitabu lukuki na wengi wasiojua wanaamini mpaka leo kuwa "inyenzi" ni tusi liliotungwa na wahutu dhidi ya watutsi. Kumbe it was not that simple. Ukisoma tu historia unajionea mwenyewe.
Pia karne za zamani kulikuwa na mtemi wa kitutsi (Rwabugiri) aliyekuwa na jeshi lake maalum lililoitwa "inkotanyi", hili jeshi lilitumika toka zama hizo kuzima majaribio ya mapinduzi ya wahutu. Wakati anavamia Rwanda, kagame alianza tena kulitumia kwa jeshi lake akijiita RPA inkotanyi. Deliberately provoking the hutus.

Burundi:
Sasa hivi hawa waasi watutsi wanaofanya mashambulizi dhidi ya wahutu wanajiita "sindumuja". Kila mtu anaona kuwa hawa ni watutsi. Lakini ikitokea wahutu wakaanza kulipa kisasi dhidi ya hawa sindumuja, kesi za genocide zitakazotokea zitadai sindumuja ni tusi dhidi ya WATUTSI WOTE na sio hawa waasi wanaofanya mashambulizi dhidi ya raia wasio na silaha. Hivi kama suala ni Nkurunzinza kugombea tena, imekosekana slogan nyingine yoyote isipokuwa "sindumuja" yenye kugawa watu kimakabila?

Foreign media biaseness:

Rwanda:
Mauaji ya waasi wa RPA mpaka leo hayaongelewi, hata baadhi ya watoto humu JF hawajui wala hawaoni uzito wa mauaji yaliyofanywa na wanajeshi wa kitutsi, RPA, kwa MIAKA MINNE dhidi ya wananchi wa Rwanda (majority wahutu), kwa bunduki na mabomu kwa sababu media zote zinatoa uzito kwa mauaji ya siku 100 tu yaliyofanywa na wananchi wa kawaida kabisa wa kihutu dhidi ya wananchi wenzao kwa kutumia mapanga na visu. Media za kimataifa hazitoi uzito wowote ule kwa mauaji aliyofanya kagame dhidi ya mamilioni ya wahutu ndani ya Rwanda (kibeho massacre), na nje ya Rwanda (DRC). Matokeo yake Kagame anaheshimiwa kama "mkombozi" wa Rwanda wakati wapinzani wake anaowaua kila siku ndio wanaitwa magaidi.

Burundi:
The same trend inaonekana sasa Burundi. Yakitokea mauaji ambayo jeshi la Burundi limepambana na watu wenye silaha, media za nje zinaonyesha mauaji. Wakiuawa wanaharakati wa sindumuja na watu WASIOJULIKANA, media za nje zinaonyesha. Lakini kila siku wanakufa makumi ya waburundi katika yale maeneo yasiyo ya kitutsi, media hazionyeshi, wanakufa wanachama vigogo wa CNDD-FDD kwa kuchinjwa lakini media za nje hazionyeshi, wala "international community" hailaani. Hii inalenga kumfanya Nkurunzinza aonekane ndie gaidi. Hata hapa kwetu majuzi tuliona b.we.ge mmoja anaitwa JoeTrippi akianza kututengeneza ila tukambwekea twitter kule akasepa?.Kinachoendelea kule Burundi sasa hivi kwa upande wa media ni exactly what people like JoeTrippi are paid to do.

Wengi wanaotumia mitandao kumuongelea Nkurunzinza vibaya ni jamii ya sindumuja ambao hata hawako Burundi, waburundi wa kweli wanapatikana kupitia hashtag hizi:

https://twitter.com/hashtag/TheSilentMajority?src=hash
 
Kazi kweli kweli, ila mwisho wa siku watakao kufa na kuumia ni Warundi wenyewe, ngoja wazoefu ni hii tifu waje
 
Mkuu umefanya uchambuzi mzuri sana nimependa na nimeelewa vizuri lakin swali langu linakuja hivi

Hivi kwanini viongozi wengi waafrika wana hii kadhia ya kung'ang'ania madaraka?

Nakwazwa sana na hili jambo japo nkurunzinza alikuwa anahaki ki katiba ila hana busara hata kidogo
 
Mkuu kiasi fulani umechambua vizuri ila nachelea kuna jambo either unaficha au unatafuta mtu wa kulink kisicho sahihi.

1. I can smell unataka kutuambia kuwa kuna force behind inasponsor hao sindumuja ambaye ni Kagame???

2. Pili kusema RPF ndio waliotungua ile Ndege kule Rwanda nadhani si kweli na undermine influence ya Hutu extrimists ambao hawakutaka kushare power na mtu.

3. Mtu kama Niyombare (mhutu) aliyeongoza mapinduzi dhidi ya Nkurunzinzah unamuweka wapi?? Mi nadhani its not about maandalizi ya genocide ni tatizo la kimfumo wa utawala na kikatiba la Burundi.

Mwisho I thought mechanism za kujua huyu ni mtutsi au muhutu zilishaisha. Au mpaka leo bado kuna ID za mtutsi na mhutu?? Na pia nilidhani muungano wa taifa umesababisha intermingle baina ya hawa watu wawili. How comes serikali imeshindwa na kuruhusu makazi ya wahutu au watutsi??
 

Mkuu kama ulikuwepo... huyu FDLR jMali ni majanga kwenye jamii yoyote ile! tatizo lake kila siku anarudia yaleyale... ukitaka kujuwa jinsi matatizo ya Burundi walivyo yavalia njuga basi we tazama jinsi wanavyoyaunganisha na ukabila... ndugu yangu ugomvi unao endelea Burundi haufanani na ulio wahi tokea hata siku moja... Rwanda, watutsi walioukimbizini waliambiwa eti nchi imejaa... na waliokuwa ndani ya Rwanda walijuta kuzaliwa... huyu mwehu Interahamwe atakupotezea wakati, kwani ukimbananisha sana na kumuuliza maswali mazito atakuambia eti basi tuache, tufanye umeshinda, you see? tatizo la Burundi sio ukabila hata kidogo! tatizo la Burundi ni la madaraka, kama hauamini basi waulize kina Nyangoma, Radjabu, Rwasa, Mbonimpa, Ngendakumana, ntavyohanyuma na wengine na wengine... kina jMali ndio wamemtia kimavi Nkurunziza na hivi kaamuwa kuanzisha ukabila kusudi azuge... hawa Interahamwe sio watu, kitu ambacho hakimuingii jMali kichwani ni kwamba hata iwe vipi haiwezekani kuuwa raia wasio na hatia... hata ndege ikitunguliwa au ufanyiwe coup d?tat! mbona Raisi wa Burkinafaso karudishiwa ofisi yake na hivi anaendelea kupeta bila mauwaji? huyu jamaa jMali atakupotezea wakati bure, hana la maana zaidi ya Hutu power ideology...
 
haya jMali bishana na hawa basi...
[h=1]Statement on Violence and Disturbing Rhetoric in Burundi[/h]More Sharing ServicesShare




Ambassador Samantha Power
U.S. Permanent Representative to the United Nations
U.S. Mission to the United Nations



November 5, 2015

FOR IMMEDIATE RELEASE
The United States is alarmed by the escalating violence in Burundi and dangerous, irresponsible rhetoric on the part of the government, loyalist militias, violent anti-government forces and criminal elements. The United States will support the region and our partners in the international community so that those who commit or incite violence are held accountable.
We are deeply concerned by President Nkurunziza?s speech of November 2nd, in which he pledged to use violent methods to have security forces search homes for weapons and opposition figures within five days. The continued sowing of a climate of fear and tension through such language and the use of such measures only prolongs and deepens Burundi?s political and security crisis. The United States expresses its extreme concern that the five-day ultimatum issued by the President will trigger widespread violence beginning this coming weekend.
We are also deeply disturbed by reports that incendiary and divisive speech is being used by other government officials. The President of the Burundian Senate, R?v?rien Ndikuriyo, has reportedly invoked the language of horrors the region hasn?t witnessed in 20 years. Whether in Kirundi or English, this language is terrifying: ?You tell those who want to execute the mission: on this issue, you have to pulverize, you have to exterminate ? these people are only good for dying. I give you this order, go!?
Such dangerous speech and the President?s call for a widespread, indiscriminate security crackdown exacerbate an already volatile situation and risk inciting even greater violence. We call on the Government of Burundi to allow immediate, unfettered access for African Union human rights and security monitors, and to act immediately on its stated commitment to participate in an internationally-mediated dialogue outside of Burundi in pursuit of a consensual path toward restoring stability and ending the climate of fear in the country.
###​

 

Uko sahihi mkuu, huyo Nkurunzinza kwani ni lazima agombee tena hata kama mahakama imempendelea? Hivi baada ya kuona watu wanakufa si bado angesema basi sigombei tena na akabaki na heshima yake? Lazima awe king'ang'anizi kama yule rais wa Syria? ?
 

Asante for your comment.

1. Ni kweli kabisa, you smelled well. Ingawa sikutaka kubase sana huko kwa sababu tayari nilishapost thread kuelezea hilo. Rwanda's involvement in Burundi ni ile kitu wazungu wanaita 'open-secret', yani siri ya wazi. Kama ambavyo kila mtu alikuwa anajua Rwanda ndio M23 kabla hata ripoti ya UN haijathibitisha hilo. Kwa sasa kuna sababu zifuatazo za hiyo 'smell'.


  1. Baadhi ya viongozi wakuu wa mapinduzi yaliyofeli wamejificha Rwanda. Na Burundi imeshaomba wawe extradited kurudishwa Burundi kujibu mashtaka, Rwanda haitaki. Na hii sio ajabu, Rwanda huwa inalinda sana vibaraka wake. Hata M23 ambao Rwanda inakataa kuwa sio wanyarwanda, haitaki kuwarudisha DRC, Laurent Nkunda mahakama ya ICC lakini Rwanda inamhifadhi haitaki kumtoa, je kuna sababu gani za Rwanda kulinda watu waliojaribu kufanya mapinduzi nchi za wengine?
  2. Mwanzo kabisa wa maandamano, Burundi ilikamata na kuwa deport raia wa Rwanda waliobainika kufanya kazi ya ushushushu katika makampuni ya telecom pamoja na media, vile vile baada ya kugundua kuwa wao ndio coordinators wa maandamano. Swali ni kwa nini wanyarwanda wawe involved kwenye maandamano katika nchi isiyowahusu?
  3. Viongozi wote wakubwa 'wanaharakati', 'journalists' wanao cordinate media/publicity ya hawa 'sindumuja' wa Burundi, wako Rwanda.
  4. Kagame na serikali yake ndio pekee hapa EAC wanao support wapinzani wa Nkurunzinza. Quote: " "If your own citizens tell you we don't want you to lead us, how do you say I am staying whether you want me or not," Kagame said May 8, 2015, at the 45th St Gallen Symposium in Switzerland."
    Lakini cha ajabu Kagame hazungumzii mkataba wa makubaliano ya Arusha wala katiba ya Burundi, labda kwa sababu yeye mwenyewe ALIVUNJA makubaliano ya Arusha kuhusu Rwanda alipoipindua serikali ya Habyarimana! Mahakama zote zilizopelekewa mkataba zimethibitisha kuwa Nkurunziza ana haki, sasa hao wanaompinga wana uhalali gani? Yeye anasema warundi hawamtaki Nkurunziza, je haoni kuwa warundi hao ni wachache sana? Maandamano yangefanyika nchi nzima hapo sawa, inakuwaje maandamano yafanyike kisutu na upanga, halafu atokee rais wa kabila la kihindi wa nchi jirani, adai watanzania wooote mpaka wale wa mpanda hawamtaki Magufuli kwa sababu ya maandamano hayo? Huyo rais mhindi wewe utamuonaje?

  5. Wakimbizi wanaokimbilia Rwanda mainly ni wa kabila moja na wale wanaokuja TZ ni wa kabila lingine. Tayari serikali ya Burundi imeshatoa malalamiko kwenye jumuiya za kimataifa kuwa kwenye makambi ya wakimbizi kule Rwanda, inafanyika recruitment, training na arming. Na hao ndio wanaorudi na kufanya mashambulizi Burundi. Kuna incidents nyingi tu ambazo jeshi la Burundi limepambana na the so called 'waasi' mpakani mwa Burundi na Rwanda. Hapa unaweza kuangalia mwenyewe ripoti ya Aljazeera inayothibitisha hilo. Burundi refugees lured to join rebel group - Al Jazeera English
  6. Uzushi wa serikali ya Rwanda nayo ni sababu kubwa. Vurugu zilipoanza, Rwanda haraka ikaanza kueneza uongo kuwa kundi la FDLR limehamia Burundi, and that Rwanda is 'ready to defend itself against FDLR in Burundi'. Huo ni uongo ambao uko designed kujustify askari wa Rwanda kuingia Burundi and nothing else. Wamefanya hivyo DRC kwa miaka mingi. Rwanda toka 1994 inaingia na kutoka huko DRC kwa kisingizio cha kupambana na FDLR, mpaka ikafikia DRC wakapigana vita na Rwanda! Hao FDLR hawaishi? Cha kushangaza FDLR walishasambaratishwa zamani sana na majeshi ya FARDC hapa majuzi, na kila siku Rwanda kupitia watu kama Mushikiwabo huwa wanasema kuwa FDLR "is not a threat militarily". Sasa hii concern ya FDLR leo hii imetokea wapi? Na how come ni Rwanda tu peke yake ndio wanaowaona hao FDLR huko Burundi? Not EAC community, not UN, not DRC, nobody else!
  7. Tukimalizia kimataifa, Burundi kumegundulika madini, na kampuni za kirusi na kichina tayari ziko huko. Wanaofahamu wanajua kuwa Kagame ni kibaraka wa marekani linapokuja suala la kuvuruga nchi za hapa kati ili makampuni ya marekani yapate access. Hivyo ukichanganya na hizo sababu zilizopita pamoja na role ya 'international media' ya kunyamazia mashambulizi dhidi ya raia ambayo yako coordinated, na badala yake ku amplify mauaji ya wapinzani ya kulipiza kisasi, unaona wazi kuwa yanatengenezwa mazingira hapa. Utawala unaotakiwa hapa ni ule ambao utaipa marekani foothold kwenye rasilimali za Burundi na kuwatoa wachina na warusi. Kama ambavyo makampuni ya ufaransa yaliyoondoka na utawala wa Mobutu na makampuni ya kimarekani kuja na Kabila....
2. Kuhusu RPF kutungua ndege, naomba tusidhani, mahakama TATU zina mashitaka ya kagame na RPF kutungua ndege. Mahakama ya ufaransa, mahakama ya spain pamoja na iliyokuwa ya ICTR. Sababu pekee kagame na RPF hawajashitakiwa ni kutokana na geo politics. Ufaransa na spain bado zina arrest warrant dhidi ya kagame na maofisa wake. Kagame hawezi kukamatwa kwa sababu ya presidential immunity. Ndio maana anajiongezea miaka afie madarakani. Kwa upande wa arrest warrant ya ICTR, imekaliwa mpaka mahakama imeisha kutokana na influence ya marekani. Tafuta taarifa kuhusu mwendesha mashtaka Carl del ponte wa ICTR alivyoshurutishwa kukalia file la Kagame kwa sababu Kagame alikuwa 'ally' wa marekani kwenye region hii.
Hio theory unayosema (kuwa Hutu extremists ndio wahusika) ni standard propaganda ambayo serikali ya kagame huitumia kila siku. Nisamehe lakini ni theory ya kipuuzi sana kwa sababu zifuatazo:


  1. Habyarimana alishatia saini ule mkataba wa kugawana madaraka. Sasa hao Hutu extremists wamtungue ili iweje? Kama walikuwa hawataki kugawana madaraka basi ndege wangetungua wakati anakwenda sio wakati anarudi! Kwani mkataba ule ulikuwa suprise? Actually Habyarimana alikuwa tayari kusaini muda mrefu sana, ni upande wa RPA ndio uliokuwa unajivuta vuta kwa sababu hii na ile, sio Habyarimana. Hii theory sio valid.
  2. Pili, tunaweza kubishana upande gani umetungua ndege, lakini hatuwezi kubishana kuwa ni wanajeshi ndio waliofanya hivyo. Kuitungua ndege kunahitaji utaalamu wa juu, na silaha maalum, hivyo tunakubaliana at least kuwa, kama waliotungua walikuwa ni upande wa serikali, basi waliotungua walikuwa ni jeshi la Rwanda chini ya Habyarimana. Lakini ukiangalia kilichotokea baada ya kutunguliwa ndege, wanajeshi wa RPA walimove haraka sana kuanza mashambulizi, wakati jeshi la Rwanda likiwa limezubaa. Hii inashangaza, kwa sababu kama jeshi ndilo lililopanga kutungua ndege, basi ni lazima wawe wamepanga the next step. Hakuna jeshi la kipuuzi linalopanga tukio zito la kutungua ndege, halafu lisijue what do to next. Jeshi la Rwanda lilipigwa kama limesimama, kwa sababu the truth ni kuwa hawakuwa hata na habari ya kutunguliwa ndege, wao na nchi nzima walikuwa wame relax wakijua vita imeisha na amani imekuwa secured kupitia mkataba. Ndege ilipotunguliwa jeshi la Habyarimana lilikuwa limepigwa butwaa, lilikuwa suprised, haikujulikana kamanda ni nani, na nani yuko in control. Upande pekee ambao reaction yao ilikuwa swift as if walikuwa wanajua ndege itatunguliwa ni RPA!
  3. Waliokuwa washirika wa kagame wa karibu kama Gen Nyamwasa na Dr Theogene Rudasingwa na wengineo tayari wameshakiri kuwa Kagame ndio aliyehusika. Kila siku wanatoa ushahidi kwenye tume mbalimbali kuhusu hilo. Ingawa kwa sasa hawa ni wapinzani lakini ushahidi wao ni muhimu kwa sababu umejaa details. By the way Gen Nyamwasa ameshasema yuko tayari kushirikiana na mahakama yoyote ile ku provide details of what happened as long as kuna deal in place for him (immunity maybe), kwa sababu shida ni kuwa akishashusha mambo na yeye mwenyewe atakuwa ameji -implicate. Ndio maana kagame watu kama hawa anawawinda popote pale.
  4. Kagame and co wakiwa wanaelezea hii theory huwa wanawatuhumu watu wanaowaita Akazu. Hawa Akazu ni watu wa karibu na Habyarimana ambao wao wanasema ndio waliokasirika na kutungua ndege. Cha ajabu ni kuwa miongoni mwao ni mke na watoto wa Habyarimana mwenyewe. Idea ya kuwa eti mke wa Habyarimana , wanae, wajomba zake, mashangazi, washikaji zake n.k wameshiriki kwenye njama za kutungua ndege ya ndugu yao kwa sababu tu hawataki kugawana madaraka na watutsi, mimi hainiingii akilini kabisa. Mkataba uliweka wazi kuwa baada ya kipindi cha mpito ungefanyika uchaguzi huru na haki. there is no way kagame na kundi lake waliokuwa wanaua watu kwa miaka minne wangechaguliwa. The hutus did not down that plane. they had nothing to gain from it.
3. Niyombere na wengine: Nilishasema mwanzo kuwa ishu ilianza kama siasa. Lakini siasa zimemalizwa kisiasa mahakamani. Niyombere mwenyewe ameshasema hataki vita na amesurrender. Jeshi zima la Burundi liko intact, hakuna wanajeshi wowote walioasi isipokuwa viongozi wachache sasa haya majeshi ya waasi yenye silaha ambayo yanadai yanapigania sababu zile zile za Niyombere wanapokea amri toka kwa nani? Obviously kuna mtu amechukua advantage hapa na kugeuza mgogoro uwe kitu kingine.

Mwisho, kuhusu mechanism ya kujuana makabila. Ni kweli kuna mchanganyiko mkubwa na kwa sisi nje ya mataifa haya hatuwezi kuwajua, lakini wenyewe kwa wenyewe wanajuana. Hakuna IDs hiyo mambo ilishafutwa. Lakini socially watu wanajuana. Ndio maana ukitembelea #sindumuja kwenye twitter utaona kuwa hawa 'sindumujas' wanatangazia dunia kuhusu genocide ambayo Nkurunzinza anataka kuwafanyia, sasa wewe jiulize kama haijulikani nani mhutu na nani mtutsi hiyo genocide wanayozungumzia itatokeaje? How will those killers know which one is Tutsi and which one is Hutu? ili hali hakuna IDs?
Kuhusu makazi sio kweli kwamba serikali imeruhusu makazi ya watu fulani na fulani. Hii imetokea naturally. Historically watutsi walikuwa ni priviledged class hivyo mpaka sasa vizazi vyao viko concentrated sana kimakazi maeneo ya mijini. Sio kitu cha makusudi. Ni kama vile hapa bongo, wazungu, wahindi na waarabu kuwa concentrated kwenye baadhi ya makazi sio jambo la makusudi ni jambo la kihistoria.

Thank you.
 
Uko sahihi mkuu, huyo Nkurunzinza kwani ni lazima agombee tena hata kama mahakama imempendelea? Hivi baada ya kuona watu wanakufa si bado angesema basi sigombei tena na akabaki na heshima yake? Lazima awe king'ang'anizi kama yule rais wa Syria? ?

Watu wanakufa kwa sababu gani? Yeye ndie anayewaua ili atawale? Nani anawaua na kwa nini? tuanzie hapo.
 

Ni kweli hii hali ya kung'ang'ania madaraka inachukiza. Especially kwenye nchi zenye utata kama Burundi na Rwanda. Hatua yake haikuwa na busara hata kidogo. Lakini mimi binafsi nadhani tatizo ni sisi wananchi wa Africa ndio tunawalea hawa watu. Sioni kwa nini watu wanashindwa kumbwaga Museveni au Mugabe kwenye uchaguzi wao wenyewe. Wapiga kura tukiamua kufanya mabadiliko Africa itabadilika. Ila as long as majority yetu bado inawapigia kura kina Nkurunzinza, tutaendelea kutawaliwa nao tu.
 

1. Rwanda's involvement in Burundi. The way you put it ni kuwalaumu Watutsi bila kuangalia vyema root course.

Kwa nini Watutsi wakimbilie Rwanda au coordinators kuwa watutsi? Mkimbizi hukimbilia ambapo atakuwa safe. Hata Tanzania bara pakitokea shida ni very simple Maasai kukimnilia Kenya na Mpemba Pemba. Hii ni kwa sababu upande utakaokimbilia unayohakika na usalama wa maisha yako.

Pili Rwanda kuweka vikosi mpakani ni hatua ambayo kwa mtazamo wangu ni sahihi since uwepo wa vita au FDRL Burundi kunastabilize amani ya Rwanda kwenyewe. Wala hili sio geni kidunia.

Pili la kutungua ndege, unakubali ilitunguliwa na askari halali wa serikali ila unahoji mbona hawakuwa na plan ya whatafter. Hili si sahihi, kwa mujibu wa statements ya baadhi ya waliokuwa Peacekeeping mission walikiri after ile bombing vikosi vya serikali vilianza kumove into action. Pia swala la kuwa RPF walikuja instantly kwa kuwa walijua tukio prior to its happening nadhani ni kuignore kuwa since 1990 RPF walikuwa stationed kijeshi na walikuwa wanafanya raids kwenye mpaka wa Rwanda na Uganda.

Suala la warrants za kumkata Kagame by French and Spain nadhani ni unafiki wa kisiasa. Madai ya Nyamwasa hayo nadhani yapo fully biased. Baada ya kuasi nchi ndio anatoa ushahidi, intentions zake ni malicious towards Kagame. Maake ukiangalia vizuri utagundua hata yeye mwenyewe hujifanya hajahusika na RPF bali ni Kagame pekee. Seriously Kagame pekee bila hao majenerali wenzie??

Tatu, kuhusu Niyombare na wengineo ni kielelezo cha failure ya utawala Nkurunzinzah. Ukiona watu wapo ready kukutoa madarakani na unapingwa jitathmini kama unafaa.

Pia nimeona issue ya location ya maandamano. Maandamano ni contagious yanaweza kuanzia ndani ya nyumba yasipodhibitiwa yaweza kusambaa nchi nzima. I think Burundu millitia iliyadhibiti and this is obvious kwani wote tuliona. So you cant expect it to have spread nchi nzima.

Sorry natumia simu sikuweza kujadili points zote kwa pamoja.

Japo nadhani tukubaliane Burundi kuna tatizo Nkurunzinzah wants to be Kagame lakini hana strength wala influence ya kuwa Kagame. Hata Kagame aweza kuwa ana matatizo yake kama issue ya Congo na madini au sakata la Fred Rwigyema but as a leader he is pretty outstanding.

Mwisho help me with this book kama unacho Mimi natafuta kitabu cha Stephen Kinzer: a thousand hills: rwandas rebirth and the man who dreamed it
 
Umemetetea sana Nkurunzinza na kujaribu kuonyesha yeye hana kosa...suala la msingi hapa ni kwamba mtu amekaa madarakani miaka 10 hiyo tayari inatosha...hajafanya kitu cha maaana ukuiangalia Burundi iko hoi taabani kiuchumi...mshauri aachw madaraka mtu mwingine aingie amani itawale
 


Wewe "mtanzania". Usiingize rwanda kwenye masuala ya burundi. Nenda kamsaidie Nkurunziza manake naona the Hague inamuandalia one way ticket.
 
Hatimaye balaa la BURUNDI linatuwa ktk mgongo wa TANZANIA !!

Mwisho wa siku Taifa la waungwana (TZ) lina beba wakimbizi wakiwemo na majambazi/majangili kuzagaa nchini humu!! (ktk kila msafara wa mamba, kenge hujipenyeza!!)

Wakati hapohapo Tanzania inamkumbatia Dictator Nkurunziza....... "THINK"
jMali dushe lowestein
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…