ward41
JF-Expert Member
- Apr 3, 2022
- 735
- 2,467
Wengi wetu tunamkumbuka TB Joshua na huduma yake ya ki kanisa.
TB Joshua aliaminika na watu wengi sana Africa na duniani kama nabii wa Mungu.
Mimi kama mfatiliaji sana wa biblia, TB Joshua alikuwa nabii wa uongo. TB Joshua amechangia pakubwa sana kuharibu ufalme wa Mungu.
Biblia inasema wazi kwamba siku za mwisho manabii wengi wa uongo watatokea na kudanganya wengi (Mathayo 24:11).
Haya mahubili ya mafuta ya upako, maji ya upako muasisi mkubwa kizazi hiki ni TB Joshua. Hawa manabii wa mafuta, maji ya upako wamemuiga TB Joshua.
Hawa manabii wanafanya Mambo machafu sana sirini. Tuhuma dhidi ya TB Joshua Sina mashaka nazo maana alikuwa nabii wa uongo.
Maelekezo ya Yesu juu ya maombi ni kwamba tuombe kwa jina la Yesu. Ukiomba nje ya hapo umepotoka.
Tusome maandiko wenyewe kuliko kulishwa matango poli na hawa manabii wa uongo.